Jumatatu, 24 Rajab 1442 | 2021/03/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ripoti ya Habari 11/09/2020

Katika mwendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan mashariki, magharibi, na marefu na mapana ya nchi kupinga uhalifu wa usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi na kuondoa dhimma, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan – eneo la Omdurman – iliandaa kisimamo cha kulaani mnamo siku ya Jumamosi Oktoba 31, 2020 katika eneo la mashahidi la Umm Derman – chini ya anwani: Usawazishaji mahusiano ni khiyana na yeyote anayeufanya ni msaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini.

Chini ya anwani "Tunakuitikia, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan waliandaa maandamano katika mji wa Gadharif mnamo siku ya Jumanne 03 Novemba 2020 saa saba adhuhuri mbele ya Uwanja wa Tahrir na karibu na Msikiti wa Kale, kupinga mashambulizi juu ya bwana wetu Muhammad (saw) ya maadui wa Uislamu.

"Mgogoro wa Uchukuzi: Suluhisho na Tiba" kwa hotuba hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan eneo la Dukhainat, mnamo siku ya Alhamisi 5/11/2020, ilifanya hotuba yake ya kawaida katika soko la Kalakila Lafah / eneo la ndani la Al-Shuqilab na Al-Fatih, iliyowasilishwa na Bw. Abdel Fattah Ahmed Daou Al-Bayt.

Mnamo siku ya Ijumaa, Novemba 6, katika Soko la Sabreen, chini ya anwani: "Serikali ya Mpito, iliyogubikwa na aibu na fedheha, yapokea pigo kubwa kutoka kwa Trump kwa kurefusha vikwazo dhidi ya Sudan", Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - Omdurman Kaskazini – ilitoa hotuba kubwa ya umma.

"Katika kumbukizi ya mazazi yake (saw), Kumnusuru kwake kutakuwa kwa namna gani?" chini ya anwani hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - Omdurman Kaskazini – ilifanya muhadhara mnamo siku ya Jumapili katika Msikiti wa Kale eneo la Souk 42 Al-Thawra baada ya swala ya Maghrib.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 13 Novemba 2020 17:09

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu