Jumatatu, 09 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Demokrasia Huhakikisha Sheria kama FATF, Ambazo Zinadhoofisha Usalama Wetu kwa Ajili ya Maslahi ya Wakoloni

Habari:

Mnamo Jumatano, 16 Septemba 2020, serikali ya PTI iliweza kupitisha miswada minane muhimu, ikiwemo mitatu inayohusiana na Jopo Kazi la wakoloni la Utendakazi wa Kifedha (FATF). Miswada hiyo ilipitishwa katika kikao cha pamoja cha bunge. Miswada hii inayohusiana na jopo kazi la FATF ilikataliwa katika Bunge la Seneti lililotawaliwa na wanachama wa upinzani lakini ikaidhinishwa katika kikao cha pamoja cha Bunge huku thuluthi ya wabunge wa upinzani wakikosa kuhudhuria.

Maoni:

Pakistan iliwekwa katika "Orodha ya Kijivu" na FATF mnamo Juni 2018 na inaendelea kuwemo ndani ya orodha hii. Pakistan imeshindwa kuzingatia majukumu iliyopewa na FATF ya kukomesha ufadhili wa ugaidi. Serikali ya PTI imeshughulika na kuleta miswada kwa ajili ya uidhinishaji wa Bunge ili kuiridhisha FATF. Serikali hii imefanya hivyo hata ingawa Amerika inaitumia FATF kukata usaidizi wowote kwa wapiganaji wa uhuru katika Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, ili Modi aweze kuumakinisha mshiko wake dhaifu.

Hivyo, India imekuwa changamfu juu ya jopo la FATF. Msimamo wake ni kuwa Pakistan haizingatii matakwa ya FATF na hivyo inapaswa kuwekwa katika "Orodha Nyeusi." Watawala wa Pakistan wamekuwa wakiwasilisha mandhari hii kama njama iliyo zalishwa na India ili kuidhoofisha Pakistan. Hivyo wanasema kuwa ni utiifu pekee kwa FATF ndio ambao utatibua njama hiyo ya India.

Mwanzoni, vyama vya upinzani vilisema kuwa serikali inapaswa kutojisalimisha kwa FATF zaidi ya matakwa yake, kwani inahujumu ubwana wa dola na haki msingi za raia. Lakini, kimsingi, wanaikubali FATF na wakati muhimu wa kuidhinisha ulipowadia, thuluthi ya wanachama wa upinzani hawakuwepo, ikiruhusu miswada ya kikoloni kupitishwa kwa wingi wa idadi ya kura kumi.

Chini ya Demokrasia, vyama vyote, tawala na upinzani, viko tayari kutumikia maslahi ya Amerika. Demokrasia iko katika Ulimwengu wa Kiislamu ili kutumikia matarajio ya wakoloni, ima ya kithaqafa, kiuchumi, kijeshi au yanayohusiana na sera ya kigeni. Aina hii ya uwepo ilithibitishwa na Waziri Mkuu, Imran Khan, hivi majuzi alipoonyesha hamu yake ya kuwanyonga wabakaji hadharani, kwa haraka akiongeza kuwa hili kamwe haliwezi kukubaliwa na Magharibi.

Hadi Khilafah kwa Njia ya Utume itakaporegeshwa, dola za wakoloni zitahujumu maslahi ya Uislamu na Waislamu, kutokana na kuwa katika Demokrasia sheria hutungwa kwa mujibu wa matamanio na matakwa ya wanadamu, kuliko kuvuliwa kutoka katika Quran na Sunnah. Katika Khilafah, si mtawala, Khalifah, wala baraza la ushauri, Baraza la Ummah, wala mahakama, ndio wenye kutunga sheria. Wote hawa hucheza dori katika kuhakikisha kuwa sheria zote zinavuliwa kutoka katika Quran na Sunnah pekee. Hivyo basi, Khilafah kikamilifu na kwa njia ya kudumu hufunga milango ya unyonyaji wa wakoloni. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَاَنِ احۡكُمۡ بَيۡنَهُمۡ بِمَاۤ اَنۡزَلَ اللّٰهُ وَلَا تَتَّبِعۡ اَهۡوَآءَهُمۡ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao.” [Surah Al-Maidah 5:49].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 25 Septemba 2020 06:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu