Jumatatu, 09 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 23/09/2020

 Vichwa vya Habari:

Maandamano Yazuka Nchini Misri

Sekta ya Benki Yafichuliwa

Mbunge wa Ufaransa Aondoka katika Kikao cha Bunge kwa Sababu ya Hijāb

Maelezo:

Maandamano Yazuka Nchini Misri

Maandamano yamezuka wiki hii nchini Misri. Katika majimbo ya Al-Qanater, Qalyubia, waandamanaji waliandamana kupitia vichochoro ili kukomesha kushambuliwa na vikosi vya usalama. Katika kijiji cha Kadiya katika jimbo la Giza, waandamanaji wa Misri walilipindua lori la polisi, wakighadhabishwa na serikali kuvunja majengo huko. Yote haya yanajiri licha ya vikosi vya usalama vya Misri kumwagwa katika maeneo kadha wa kadha katika miji kote nchini, ikiwemo Uwanja wa Tahrir na Suez, huku vituo vya upekuzi vya kijeshi vikiwekwa katika sehemu za makutano na barabara kuu. Nyingi ya sababu za Mapinduzi ya Kiarabu zingali zipo na zimekuwa mbaya zaidi chini ya Abdel Fattah el-Sisi, ambaye ameonyesha kuwa mbaya zaidi kuliko watangulizi wake.

Sekta ya Benki Yafichuliwa

Nyaraka zilizovujia zinazohusisha takriban $2 Trilioni za miamala zimefichua namna gani baadhi ya benki kubwa za ulimwengu zimeruhusu wahalifu kutembeza pesa chafu kote ulimwenguni. Pia zimeonyesha jinsi mabwenyeye wa Kirusi walivyotumia benki kukwepa vikwazo ambavyo vilipaswa kuwazuia kuingiza pesa zao Magharibi. Ndio mpya zaidi katika msururu wa mivujo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ambayo imefichua mipango ya siri, ulanguzi wa pesa na uhalifu wa kifedha. Faili za FinCEN ni nyaraka zaidi ya 2,500, ambazo nyingi yazo zilikuwa ni faili ambazo benki hizo zilizituma Amerika kati ya 2000 na 2017. Inaibua wasiwasi kuhusu kile ambacho wateja wao watakuwa wanafanya. Nyaraka hizi ni baadhi ya zile siri zinazolindwa sana na sekta ya benki ya kimataifa. Matokeo yanajumuisha: HSBC iliruhusu matapeli kutembeza mamilioni ya dolari zilizoibwa kote ulimwenguni, hata baada ya kujua kutoka kwa wapelelezi wa Amerika kwamba mpango huo ulikuwa ni utapeli. JP Morgan iliruhusu kampuni moja kutoa zaidi ya $1bilioni kupitia akaunti moja ya London bila ya kujua ni nani aliyeimiliki. Benki hiyo baadaye ikagundua kampuni hiyo huenda ikawa inamilikiwa na majambazi walio katika orodho ya FBI ya Watu 10 Wanaosakwa Zaidi.

Mbunge wa Ufaransa Aondoka katika Kikao cha Bunge kwa Sababu ya Hijāb

Mbunge mmoja wa Ufaransa wa mrengo wa kulia aliamua hili lingekuwa kwa maslahi bora zaidi ya watu wa eneo bunge lake kutoka katika kikao cha bunge chenye kuchunguza athari za janga la maambukizi la COVID-19 kwa vijana nchini Ufaransa. Mbunge huyo, Anne-Christine Lang, aliondoka katika kikao hicho baada ya kuona ni jambo lisilokubalika kwa Maryam Pougetoux, mwakilishi wa UNEF (Muungano wa Kitaifa wa Wanafunzi nchini Ufaransa), amehudhuria huku akiwa amevalia hijab. Baada ya tukio hilo, Lang akaandika katika mtandao wa Twitter kwa Kifaransa: “...Siwezi kukubali kwamba mtu aje ashiriki katika kazi yetu katika Bunge la Kitaifa huku akiwa amevaa hijāb, ambayo kwangu, bado inasalia, kuwa alama ya kujisalimisha. Hivyo nikaondoka katika kikao hichi.”

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu