Enyi Ummah wa Kiislamu na Majeshi Yake: Ikiwa Hamkasirishwi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mambo Yake Matakatifu, Basi Mtakasirishwa na Kuchukua Hatua kwa ajili ya Nini?!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Jumatano, 27/5/2026, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vilirusha picha zinazoonyesha vikosi vya umbile la Kiyahudi vikimshambulia kikatili mwanamke mchanga wa Kipalestina huko Bab Hutta, moja ya malango ya Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, vikimnyang'anya kitambaa chake cha kichwani kwa nguvu kabla ya kumkamata. Tukio hili linajiri huku kukiwa na ongezeko la ukiukwaji wa sheria na hatua za usalama ulioongezeka kutoka kwa vikosi vya uvamizi katika milango ya kuingia katika Jiji la Kale la Al-Quds na malango ya Msikiti wa Al-Aqsa, sanjari na Idd al-Adha. Waliweka vituo vya ukaguzi na kuchunguza vitambulisho vya wapita njia, wakizuia idadi kubwa ya watu kuingia msikitini.



