Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  13 Shawwal 1441 Na: 1441/65
M.  Alhamisi, 04 Juni 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Vitisho Vitupu Badala ya Hatua ya Kijeshi Inaipa Nguvu Dola ya Kibaniani katika Uadui. Ni Khilafah Pekee Ndio Itakayo Walazimisha Maadui Zetu Kurudi Nyuma

Kwa kubwaga jukumu lake kimakusudi juu ya Uvamizi wa India Kashmir, serikali ya Bajwa-Imran inajifunga tu na vitisho vya kujibu mashambulizi juu ya mashambulizi katika Mpaka wote wa Udhibiti. Mnamo 3 Juni 2020 Mkurugenzi Mkuu wa ISPR aliitahadharisha Dola hiyo ya Kibaniani "kutocheza na moto," kupitia kutekeleza ukiukaji wa kijeshi. Lakini, vitisho vitupu vilishindwa kuuzuia ukiukaji huo wa kijeshi wa mwaka mmoja ambao Dola ya Kibaniani tayari umeufanya katika eneo Lililo Kaliwa la Kashmir. Ikiwa na imani kamili kwamba serikali ya Bajwa-Imran itashikamana kiupofu na sera iliyo elekezwa na Amerika ya udhibiti, Mnamo 5 Agosti 2019 Dola ya Kibaniani iliitangaza Kashmir kama eneo la India, ikikiuka waziwazi Maazimio ya Umoja wa Mataifa pasi na majibu yoyote kutoka kwa Umoja huo. Ilhali, serikali ya Bajwa-Imran inazidi kulilia usaidizi kwa sanamu la jiwe la Umoja wa Mataifa, ikimpatia Modi muda wa kumakinisha mguu wake, kwa kulifungia bonde la Srinagar, akifanya harakati za kijeshi katika eneo hilo na kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza idadi ya Waislamu ambao ndio wengi katika Kashmir Iliyo Kaliwa. Kana kwamba haina lolote isipokuwa vijiti vya kuchokoa meno mikononi mwake, serikali ya Bajwa-Imran imekuwa ikitazama tu huku Dola ya Kibaniani ikiimarisha kambi yake eneo la Daulat Beg, maili nane tu kutoka kwa Barabara Kuu ya kistratejia ya Karakorum, kupitia kuipandisha daraja hadi ya Brigedia na kuiunganisha na mtandao wake wa barabara za ndani kupitia barabara ya Darbuk-Shyok-Daulat Beg. Na sasa, kwa kupata nguvu kutokana na msimamo dhaifu wa kudumu wa serikali ya Bajwa-Imran, Dola ya Kibaniani inasubutu kutoa madai ya kuivamia Gilgit-Baltistan pamoja na Azad Kashmir (Iliyo kombolewa). Kupitia kujifunga kimakusudi na kuihami Azad Kashmir, serikali inaupa nguvu uunganishaji wa Dola ya Kibaniani wa Bonde Lililo Kaliwa, ikitoa njia ya kutambuliwa kwake.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Kupitia kujifunga kwake na kuihami Azad Kashmir, serikali ya Bajwa-Imran inampa Modi uhuru wa kumakinisha mshiko wake dhaifu juu ya Kashmir Iliyo Kaliwa, ikiyazuia majeshi yetu yaliyo tayari na yenye uwezo wa kuvunja mshiko huo. Inafanya hivyo hata ingawa majeshi yetu nguvu yao ni mfumo wao, Uislamu, kupitia hamu ya kupata shahada na kuungana na Waislamu wa Kashmir Iliyo Kaliwa kama ndugu moja. Inafanya hivyo hata ingawa majeshi ya Dola ya Kibaniani wamedhoofishwa na imani yao batili kwa Hindutva, ambayo imepelekea mgawanyiko mkubwa katika safu zao, kupitia utabaka na jinsia, huku ikiwafanya kuwa waoga kutokana na kupenda kwao kuishi. Inafanya hivyo hata ingawa makafiri wa China sasa wanagongana na makafiri wa Dola ya Kibaniani, ambapo ni fursa muwafaka kwa majeshi yetu kuikomboa Kashmir Iliyo Kaliwa. Inafanya hivyo hata ingawa msaidizi wa Dola hiyo ya Kibaniani, Amerika, imelazimika kusalimu amri nchini Afghanistan, huku mkurupuko wa virusi vya Korona, mporomoko wa kiuchumi, ghasia za kabla ya uchaguzi na ubaguzi wa rangi wa kitaasisi yakiiangusha hadi chini kwake nyumbani. Sasa ni wakati wa kukomesha khiyana kwa Kashmir Iliyo Kaliwa kutoka na serikali iliyo kosa maono, zembe na dhaifu kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume (saw), ambayo itahukumu kwa yale yote aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu (swt), ikiwalazimisha maadui zetu kurudi nyuma. Hivyo, tuwatakeni vijana wetu katika majeshi watoe Nusra kwa Hizb ut Tahrir ili kurudishwa mara moja kwa ngao, Khilafah, ili nyoyo zetu zinazo vuja damu zipone kupitia vikosi vyetu kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir Iliyo Kaliwa na kwa kupitia takbira zao za furaha wakati wa kuruzukiwa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum 30: 4-5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu