Alhamisi, 20 Rajab 1442 | 2021/03/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  26 Shawwal 1441 Na: 1441 / 69
M.  Jumatano, 17 Juni 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Huku Makafiri Wakijidhoofisha Wenyewe kupitia Mizozo ya wao kwa wao, Simamisheni Khilafah Kuikomboa Kashmir na Msikiti wa Al-Aqsa

Jioni ya tarehe 16 Juni 2020, karibu vikosi ishirini vya India viliuawa na Wachina, wakati wa taharuki ambazo zinatoa fursa nzuri ya kusimamisha tena Khilafah nchini Pakistan. Ijapokuwa Waislamu wa Pakistan walishangilia kushindwa kwa Dola ya Kibaniani, Uislamu unahitaji hatua kubwa zaidi kutoka kwao zenye athari ya kieneo na kiulimwengu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

(تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ“Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili” [Surah al Hashr 59:14] Makafiri wameungana kwa uadui dhidi ya Waislamu, kama ilivyo wazi uvamizi wa kikatili wa Dola ya Kibaniani kwa Kashmir na mateso ya kikatili ya China kwa Waislamu wa Uighur wa Turkistan Mashariki. Lakini, wakati huo huo, Makafiri wanatofautiana katika maoni yao, ushuhuda na tamaa zinazo pelekea mgongano mkubwa kati yao. Kieneo, Modi anafuata mpango wa Amerika wa kuidhibiti Uchina, ambapo inatia dhiki katika vikosi vyake vyenye maandalizi duni. Kimataifa, bwana wa Modi, Amerika, anagongana na China katika kumbi nyingi, katika wakati ambao uchumi wake unadhoofika, huduma yake ya afya inaporomoka, jeshi lake linatamani kupunguza mizigo yake na watu wake wamegawanyika vikali kwenye safu za ubaguzi wa rangi na kisiasa. Hakika ni wakati muafaka wa kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume (saw), ambayo itaunganisha na kuhamasisha vikosi vya jeshi la Ummah wote ili kuzikomboa Ardhi za Waislamu zilizo vamiwa. Lakini, badala yake, serikali ya Bajwa-Imran inaendelea katika utiifu wa kiupofu kwa Amerika, hivyo basi kupoteza kila fursa ambayo Mwenyezi Mungu (swt) inaiwasilisha na kuwasukuma Waislamu katika umasikini mkubwa na utovu wa usalama.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Uislamu umetuwajibisha sisi na usimamishaji ubwana wa Uislamu katika uwanja wa kimataifa. Hivyo basi, dola ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) pamoja na Khilafah Rashidah baada yake (saw), zilinyakua kikamilifu fursa hiyo wakati himaya za Kirumi na Uajemi zilipo dhoofika na mizozo ya wao kwa wao. Wale walio hukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) walizishinda himaya hizi, na kuziunganisha nyingi ya ardhi zao na ardhi kubwa za Waislamu, huku watu wao wakiingia katika Uislamu makundi kwa makundi. Khilafah Rashida sio tu sehemu ya historia yetu tukufu, kuikumbuka kwa ari, ndio umbile la pekee la Kisiasa la Umma wa Kiislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) amewaahidi wale walio amini na wakatenda matendo mema kwamba watarithi ukhalifa (uongozi) duniani,

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa waliokuwa kabla yao” [An-Nur: 55]. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara njema ya kurudi wa Khilafah kwa Njia ya Utume, baada ya utawala wa kukandamiza, ambao tunaishi chini yake, «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha kitakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” [Ahmad]. Hivyo basi sote natuwasiliane na vijana wetu katika vikosi vya majeshi, tuwahimize wao kama aMusab ibn Umayr (ra) alivyo wahimiza wanaume wa vita wa Yathrib, kupeana Nussrah yao kwa ajili ya kusimamisha Uislamu kama dola. Wakati huo, apendapo Mwenyezi Mungu, chini ya uongozi weneye maono wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Takbiri za kusherehekea ushindi zitasikika katika bonde la Srinagar na Msikiti wa Al-Aqsa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-pakistan.com/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu