Jumanne, 07 Sha'aban 1441 | 2020/03/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ukoloni wa Kithaqafa ya Urusi Katika Asia ya Kati

Nyuma ya pazia ya mgogoro unaoendelea wa idadi ya watu nchini Urusi, Kremlin imechangamkia upanuzi wa thaqafa yake ndani ya Asia ya Kati, ikiwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika hili na kutumia ushawishi wake kwa tawala za eneo hilo. Kwa mfano mnamo Januari 15, 2020, Bunge la Chini laTajik liliidhinisha makubaliano baina ya serikali za Urusi na Tajikistan juu ya ujenzi, vifaa na kitengo cha kiufundi cha shule tano za lugha ya Kirusi.

Naibu Waziri wa Elimu na Sayansi wa Tajikistan Rakhmatullo Mirboboev, akiwasilisha nyaraka kwa Wabunge, alisema kuwa shule hizo zenye uwezo wa kuchukuwa hadi wanafunzi 1200 kila moja zitakuwa Dushanbe, Kulyab, Khujand, Bohtar na Tursunzade. Kwa mujibu wa nyaraka iliyosainiwa na Rakhmon na Putin mnamo Aprili 2019, baada ya kufunguliwa shule hizo, masomo yake yataendeshwa kwa mujibu wa viwango vya masomo vya Urusi.

Upanuzi wa thaqafa na lugha kutoka upande wa Urusi kwa watu wa Asia ya Kati, ulioanza tokea wakati wa uvamizi wa kaisari wa Urusi, unaendelea hadi leo. Na mamlaka za Urusi za hivi sasa zimekuwa daima zikitumia namna na mbinu mpya katika muelekeo huu. Na, lau hapo awali watu wa Turkestan walikuwa chini ya mamlaka halisi ya Urusi, hivi sasa, japokuwa ni rasmi watu wa eneo wameshapata uhuru kutoka kwa Urusi. Kwa hakika, nchi za Asia ya Kati ziko katika ushawishi kamili au ulio na nguvu wa ukoloni wa Urusi. Kiasili, waungaji mkono wa utawala wa Urusi katika nchi hizi wanaweka mazingira yote kwa ajili ya utanuzi wa thaqafa na lugha ya Urusi katika eneo.  

Kwa mfano, mnamo 2017 pekee, walimu 30 wamewasili Dushanbe kutoka Urusi. Mwishoni mwa 2018, walimu wengine 48 kutoka maeneo tofauti ya Urusi wamekwenda kufanya kazi Tajikistan, na kupangiwa kazi katika shule 20 za miji tofauti ya jamhuri. Farit Mukhametshin, naibu mwenyekiti wa kamati ya Baraza la Shirikisho la mambo ya nje ya Bunge la Shirikisho la Urusi katika mkutano wa kimataifa wa udugu uliofanyika Tashkent Disemba 22, 2018, alisema kuwa Baraza la Shirikisho limezingatia na kuzichukuwa sheria mbili zinazohusiana na uenezaji wa lugha nathaqafa ya Kirusi nje ya Urusi chini ya kisingizio cha upendo wa kidugu kwa nchi za kigeni. Kwa kutegemea matokeo ya mikutano kama hiyo, Bunge Dogo linasisitiza juu ya maendeleo ya mchakato kwa ajili ya kubuni fikra ya “Shule za Kirusi Nje ya Nchi”, kupitia mjumuisho wa mpango wa kitaifa wa Urusi juu ya sera ya kigeni. Hii inamaanisha uwekezaji wa rasilimali fedha kuunga mkono shule za Kirusi nje ya nchi. Na tumepokea marejesho mzuri kutoka serikali ya Urusi, ambayo imeahidi kuwa mnamo 2021 kuanzisha utekelezaji wa mpango tofauti “Shule za Kirusi Nje ya Nchi” – kama mpango wa dola” – alisema wakati huo. Pia alikumbusha kuwa wakati wa ziara ya Rais Putin nchini Uzbekistan, zaidi ya maafisa wa juu 80 wa vyuo vikuu vya Urusi waliitembelea nchi, wakati wa ziara ambapo kiasi cha mikataba mia moja ilitiwa saini kuzipatia nchi kile kinachoitwa “msaada” kwa kila mmoja katika mchakato wa elimu. Bila shaka, yote yanayoitwa “msaada” yatakuwa ni kwa upande mmoja: Urusi bila shaka itakazania miradi yake ya elimu nchini Uzbekistan.

Zaidi ya hayo, katika nchi za Asia ya Kati, kutokana na propaganda endelevu na maoni juu ya ubora wa taifa la Urusi, rai jumla ya wazi imeanza kujengeka katika akili za watu kuhusu elimu ya watoto wao katika shule za Urusi, kwa baadhi hata hili limegeuka kuwa suala la ufakhari na alama ya elimu. Bila kuelewa ya kuwa lugha ya Kirusi kwa kiasi fulani ilizingatiwa kuwa ni ishara ya kuwa nyuma, na matumizi ya matamshi ya Kirusi katika mazungumzo yameanza kumaanisha kiwango cha juu cha mtu cha elimu, ambapo leo hii unaweza kusikia lugha ya Kirusi ikizungumzwa miongoni mwa vijana katika mitaa ya miji mikubwa. 

Katika moja ya kazi za utafiti, mwanasayansi wa Kirusi, aliye na Ph.D katika sayansi ya siasa, Fedor Frolov ameelezea mpangilio wa thaqafa na upanuaji wa lugha ya Urusi: “Mgongano juu ya watu hufanyika kupitia thaqafa na lugha, ambayo huweka mazingira mageni ya kithaqafa na kilugha na kumakinisha sifa zisizokuwa za kikabila katika shughuli za kimaisha. Mchakato huu huleta kitisho cha kuvunja utengano wa mchakato wa utambulisho binafsi wa raia pamoja na dola.” “Dhumuni la sera ya Urusi katika nyanja ya lugha na thaqafa ni usimamizi na kufanya utanuzi wa thaqafa na lugha ya Urusi kote nchini na Soviet ya zamani (ikijumuisha Asia ya Kati) kuanzisha na kudhibiti mchakato wa utambuzi wa watu wa maeneo haya pamoja na Urusi, ili kuiimarisha lugha na thaqafa ya Kirusi.” – mwanasayansi huyu anazingatia hayo.

Wataalamu wanaamini kuwa ni muhimu kutenganisha kwa uwazi baina ya kujifunza lugha ya kigeni ili kujenga mahusiano na watu wengine, na utanuzi wa lugha, ambao unatishia kuleta upotovu wa kithaqafa na kupotea kwa watu wa Asia ya Kati katika utambulisho wao siku za mbeleni. Pia iangaliwe kuwa usomaji wa lugha ya kigeni uzingatiwe na watu wetu kuwa ni uchukuwaji wa elimu tu, ambapo hutakiwa ufanyike kupitia msingi mmoja pekee wa thaqafa ya Kiislamu. Hivyo, mtu lazima awe muangalifu kwani pamoja na kusoma lugha ya Kirusi, kanuni za thaqafa ya Kirusi na fikra za Kirusi za kimaisha zinapenyezwa kwa watoto wetu, kama ilivyokuwa wakati wa Usovieti. Na zaidi ni kuwa, elimu ya lugha ya Kirusi isiwe ndio alama ya ufakhari au kigezo cha elimu miongoni mwa watu.

Wafuatilia wako makini: Urusi hivi leo ndani ya Asia ya Kati haitekelezi tu ukoloni wa kijeshi-kisiasa na kiuchumi, unaodhihirishwa kwa ufunguzi wa vituo vya kijeshi, udhibiti kamili wa madikteta wa ndani na uingiliajikato wa nchi zetu katika miradi ya kiuchumi ya kimaeneo, lakini pia utanuzi wa kithaqafa, ukilenga kubadilisha ufahamu wetu, kugeuza fikra za kizazi kijacho, ili kikuwe katika kutamani kumuigiza mkoloni wa Kirusi na kupenda kuwa kama yeye.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Umar Farsy

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 27 Februari 2020 09:55

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu