Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa Kila Mwanamke wa Kiislamu:
Je Kuna Ujira Wowote wa Wema Isipokuwa Wema?
(Imetafsiriwa)

Hakika, Mwenyezi Mungu, utukufu ni wake, ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Ametakasika Utukufu Wake, Yeye ndiye mwenye fadhila bora, Yeye ambaye huwapa viumbe vyake baraka zisizo na mwisho. Ukarimu wake kwa viumbe vyake vyote umewatangulia, kwani Yeye ni Ar-Rahman (Mwingi wa Rehema), kisha akawachagua watu wa utiifu Wake, kwani Yeye ni Ar-Raheem (Mwingi wa Rehema). Yeye (swt) asema:

[ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُواْ]

“Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu.” [At-Tawba: 118] na Yeye (swt) asema:

[يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ]

“anao wapenda nao wanampenda.” [Al-Maida: 54].

Upendo wake umepita viumbe vyake na amewazunguka kwa upole katika amri yake. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kama ambavyo inapaswa kuwa kwa Utukufu Wake na Mamlake Yake Makuu.

Mtu mwenye busara ambaye huuangalia uumbaji wa Mwenyezi Mungu (swt) kwetu, na jinsi Yeye (swt) anavyoshughulikia mambo yetu kutoka pembe zote, kwa uangalifu na ukarimu, kwa kiwango ambacho moyo wa kiumbe huyeyuka kwa upendo kwa Muumba Mwenye kupenda Zaidi. Je! Ni ukarimu gani ulio mkubwa kuliko kule kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amekuumba bila ya kutoka katika kitu chochote, kisha akakupa akili ambayo alikunyanyua kwayo kutoka kwa viumbe vyake vyote. Halafu, ili usije ukapotea, Yeye akawatuma mitume kwako, lakini akaifanya akili yako iwe ndio nyenzo ya utambuzi Wake, na hakuliacha jambo hilo kwa mitume tu kukujulisha, lakini badala yake, aya zake zote ziliihutubia akili yako ili kukuongoza wewe, na akakutumia kiumbe Wake bora zaidi ili kuupeleke moyo wako Kwake (swt), na akakuwekea sheria zilizo na rehema kamili, haki, upendo na heshima.

Je! Ni wema gani mkubwa zaidi ya huu ambao mwanamke anaupokea kushinda kuwa Muislamu? Wadhifa unaomfanya kuwa malkia wa nyumba, na mwanamume anawajibika kwake, kwa hivyo usimamizi wake juu yake ni jukumu kubwa, na sio ruzuku ya heshima au fadhila. Kwa kiwango, kwamba hadhi ya mwanamume imeunganishwa kulingana na muamala wake kwa mkewe kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asemavyo: «خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِأَهْلِهِ» "Mbora wenu ni yule mbora wenu kwa mkewe", na pesa bora za mume ni zile azitumiazo juu ya mkewe, na uhusiano wake naye na kuwa mwema kwake ni sababu ya Mwenyezi Mungu kumuunganisha mja na vitu vingine vingi ambavyo haviwezi kutoshea hapa. Kuna fadhila gani nyengine kubwa zaidi ya hii, Ewe mwanamke wa Kiislamu?

Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye ametuzunguka kwa uangalizi wote huu, na kutaja maelezo yake katika kisa cha mtume kwa mwanamke mmoja,

 [كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ]

“ili macho yake yaburudike wala asihuzunike.” [Al-Qasas: 13], hakutuumba bure bure na bila ya lengo; kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt), Utukufu uwe kwake, ameeleza katika Kitabu Chake, kuwa ametuumba ili kututahini! Ndio, ametuumba ili kututahini, kisha ukarimu wake ukatupita, na Mwenyezi Mungu, Utukufu uwe kwake, alipomuumba Adam, malaika walimwambia"

[أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ]

“Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu”. Kisha Yeye (swt) akajibu:

[إِنِّي أَعْلَمُ مَا لاَ تَعْلَمُونَ]

“Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.” [Al-Baqara: 30].

Hivyo Ewe mwanamume na mwanamke wa Kiislamu, kuwa na imani Yule wa Pekee mwenye ihsan (mzuri mno katika muamala), na usiikhini.

Mwenyezi Mungu (swt) ameumba mauti na uhai ili kuona ni yupi kati yetu ni mwenye matendo mema. Mwenyezi Mungu (swt) atwambia:

 [وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ]

“Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo.” [Hud: 7].

Na Yeye (swt) asema katika Surah Al-Kahf:

[إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلاً]

“Kwa hakika tumevifanya vilioko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao wenye vitendo vizuri zaidi.” [Al-Kahf: 7]

Na katika Surah Al-Mulk:

[إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلاً]

“Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo.”

Na katika hadith ya Amir ul-Mu'minina (Kiongozi wa Waumini) Umar (ra) ambayo Imam Muslim imeipokea katika Sahih yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema wakati Jibril, (as), alipomuuliza kuhusu Ihsaan:  «أَنْ تَعْبُدَ اللَّهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ»“Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama ambaye wamuona; na ikiwa humuona basi Yeye yuakuona.”

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِنْ قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُوداً إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ وَمَا يَعْزُبُ عَنْ رَبِّكَ مِنْ مِثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِنْ ذَلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُبِينٍ]

“Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur'ani, wala hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kilicho wazi.” [Yunus: 61]

Na ikiwa ibada ni ya lazima nje ya Ramadhan, basi ni lazima zaidi ndani ya Ramadhan, hata Nafilah (amali zinazopendekezwa) inachukua mahali pa wajibu ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ukijikurubisha urefu ya shubiri moja, anajikurubisha kwake urefu wa dhiraa moja na Mwenyezi Mungu (swt) anaendelea kumwongoza Muumini na kumsamehe mpaka ajikaribishe kwa Mwenyezi Mungu kwa kile anachopenda (swt).

Ewe mja wa kike wa Mwenyezi Mungu (swt), ambaye Mwenyezi Mungu amtendea kwa wema tangu wakati wa kuumbwa kwako hadi leo na anaendelea kukupa wema na huruma: je! Kuna malipo yoyote ya wema isipokuwa wema?

Mwenyezi Mungu, Utukufu uwe kwake, kutokana na ukamilifu wa Neema Zake, anatuamrisha kumtii Yeye, Anatuongoza Kwake, na anatupa ilham, namna ya kujikurubisha Kwake, kisha anaitakabali amali njema, kuizidisha, na kulipa wema kwa wema.

Haya hapa baadhi ya maswali ambayo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, yatakusaidia kutambua msimamo wa miguu yako. Je, inafuata nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu - ambaye amewaamrisha wanawake katika Hija ya mtume ya kuaga (Hijjatul Wida), au utakengeuka kutokana nazo, Mwenyezi Mungu aepushe mbali?

Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake ni vipenzi zaidi kwako au wengine?

Je, unajifunga na maamrisho ya Mwenyezi Mungu hata ikiwa yanakwenda kinyume na matamanio na matakwa yako, ili nguo zako ziwe kama vile apendavyo Yeye na moyo wako uwe mtiifu Kwake, na maisha yako yametegemezwa juu radhi Zake, ili usiufanye ulimwengu huu kuwa ndio hamu yako kubwa wala kiwango cha elimu yako?

Je! Wewe ni mtu anayeshindana na wengine katika bidhaa za ulimwengu huu akitafuta kuzipata na kutumia pesa zake na wakati wake mwingi kutafuta kitu hiki, akitotilia maanani kujenga nyumba yake kesho Akhera?

Je! Unachukua sehemu yoyote kutoka kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika kuhifadhi, kutafakari, kusoma, kujifunza na kufundisha?

Je! Ulitumia muda wako na majirani wa kike na jamaa wa kike katika kusengenya na umbeya, au ulikuwa ni taa ya mwongozo na mikusanyiko yako ilikuwa ya vikao vya kumkumbuka Mwenyezi Mungu vilivyohudhuriwa na malaika?

Je! Unaheshimu ibada za Mwenyezi Mungu, huzichukulii sahali, na hulidharau dhambi, kama vile unyonyoaji kamili wa nyusi (an-nams) au kubeza na kudadisi heshima za watu, kama ilivyo kawaida ya baadhi ya wanawake?

Je, unatii amri Yake na kuomba msamaha kutoka Kwake unapofanya makosa? Je, unakubali ushauri na mwongozo pasi na kiburi na ushindani na kujifakhiri katika dhambi?

Je, ulichukua ahadi kuwa miongoni mwa wale wanaoiunga mkono dini ya Mwenyezi Mungu, ili uwe na hisa katika kujifunza elimu ya Kiislamu na kulingania dini ya Mwenyezi Mungu na kutawala kwake duniani, au ulipuuza faradhi hii kubwa na huku ulimi wako ukitamka, "Kuwalea watoto wangu ndio bora zaidi."

Je, kweli umeufanya ulezi wa watoto wako kuwa mradi ambao utawekeza kwa ajili ya Akhera, ili uamiliane nao kama baraka ambayo Mwenyezi Mungu amekuneemesha juu yako, na utakutana Naye Siku ya Kiyama na kumwambia: Ewe Mola, hii ndio baraka yako ambayo nimefanya kila niwezalo katika kuwalea, kwamba nimetoa ahadi yangu ya kuonyesha uchungaji na ihsan kwao hadi wakawa waja wako wema ambao walikuwa wakieneza wema?

Je, ulikuwa ukimsaidia mumeo kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na je, ulikuwa nguzo imara katika kusimamisha familia njema yenye manufaa kwa Waislamu, au ulikuwa umeshughulishwa na kujijenga binafsi na kubeba pamoja nawe cheche ya miito ghushi ya uhuru wa wanawake, usawa na wanaume, na kujitolea hoja?

Hii ni mifano. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atusaidie kufanya mema katika kazi yetu na aimakinishe dori yetu kama wanawake wa Kiislamu walio na jukumu katika dunia hii, ili tuwe miongoni mwa wale waliofuata maneno ya Mtume wetu (saw): «إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ إِذَا عَمِلَ أَحَدُكُمْ عَمَلاً أَنْ يُتْقِنَهُ» “Mwenyezi Mungu hupenda pindi mmoja wenu anapofanya jambo alifanye kwa njia nzuri.”

Wakati umewadia kwa kila mtu mtiifu kufanya kazi kwa bidii na kutoa kile awezacho.

Twamuomba Mwenyezi Mungu atusamehe mapungufu yetu na atusaidie kufanya yale yanayohitajika kwetu.

#رمضان_والإحسان

#Ramadan_And_Ihsan
#
Ramazan_ve_İhsan

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Bayan Jamal 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu