Alhamisi, 13 Shawwal 1441 | 2020/06/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bustani za Peponi

(Imefasiriwa Kutoka Al-Waie)

(Kuhusiana na Hirizi na Dua kwa Ajili ya Ponyo)

Imepokewa kutoka kwa Sahl ibn Saad (ra), kuwa Mtume (saw) alisema,

«لَيَدْخُلَنَّ الْجَنَّةَ مِنْ أُمَّتِي سَبْعُونَ أَلْفًا، أَوْ سَبْعُمِائَةِ أَلْفٍ مُتَمَاسِكُونَ، آخِذٌ بَعْضُهُمْ بَعْضًا (صفًا واحدًا بعضهم بجنب بعض). لاَ يَدْخُلُ أَوَّلُهُمْ حَتَّى يَدْخُلَ آخِرُهُمْ (أي أن دخولهم يكون في وقت واحد) وَجُوهُهُمْ عَلَى صُورَةِ الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ»

Watu elfu sabini au elfu mia saba katika Ummah wangu (Abu Haazim ambaye ni mpokezi wa hadithi hii hakumbuki kama Sahl ametamka elfu sabiini au elfu mia saba) wataingia Peponi, pamoja, wameshikana (yaani kila mmoja amemshika mkono mwenziwe, huku wakienda kwa mstari mmoja) na sio mmoja wao kuingia kabla ya mwengine (yaani, wote wataingia Peponi kwa pamoja) na nyuso zao zitang’ara kama mwezi mpevu” 

Ibn Abbas (ra) amepokea kutoka kwa Mtume (saw),

«عُرِضَتْ عَلَيَّ الأُمَمُ، فَرَأَيْتُ النَّبِيَّ وَمَعَهُ الرُّهَيْطُ (تصغير الرهط وهو الجماعة دون العشرة). وَالنَّبِيَّ وَمَعَهُ الرَّجُلُ وَالرَّجُلاَنِ. وَالنَّبِيَّ لَيْسَ مَعَهُ أَحَدٌ؛ إِذْ رُفِعَ لِي سَوَادٌ عَظِيمٌ (العدد الكبير الذي يُرى من بعيد) فَظَنَنْتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي، فَقِيلَ لِي: هٰذَا مُوسَىٰ وَقَوْمُهُ، وَلٰكِنِ انْظُرْ إِلَى الأُفُقِ. فَنَظَرْتُ، فَإِذَا سَوَادٌ عَظِيم، فَقِيلَ لِي: انْظُرْ إِلَى الأُفُقِ الآخَرِ؛ فَإِذَا سَوَادٌ عَظِيمٌ (جاء في رواية عند البخاري:« فرأيت سوادًا كثيرًا سد الأفق). فَقِيلَ لِي: هٰذِهِ أُمَّتُكَ، وَمَعَهُمْ سَبْعُونَ أَلْفًا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ وَلاَ عَذَابٍ». ثُمَّ نَهَضَ فَدَخَلَ مَنْزِلَهُ. فَخَاضَ النَّاسُ (تكلموا وتناظروا وانتشر الصوت) فِي أُولٰئِكَ الَّذِينَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ وَلاَ عَذَابٍ. فَقَالَ بَعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمُ الَّذِينَ صَحِبُوا رَسُولَ اللّهِ صلى الله عليه وسلم، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمُ الَّذِينَ وُلِدُوا فِي الإِسْلاَمِ وَلَمْ يُشْرِكُوا بِالله، وَذَكَرُوا أَشْيَاءَ، فَخَرَجَ عَلَيْهِمْ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: «مَا الَّذِي تَخُوضُونَ فِيهِ؟» فَأَخْبَرُوهُ. فَقَالَ: «هُمُ الَّذِينَ لاَ يَرْقُونَ (لا يقرؤون على غيرهم بالرقية). وَلاَ يَسْتَرْقُونَ (لا يطلبون من أحد أن يرقيهم، لقوة اعتمادهم على الله)، وَلاَ يَتَطَيَّرُونَ (مأخوذة من الطير، وأصله التشاؤم بالطير الذي كان منتشرًا في الجاهلية، ولكنه يعمُّ كل تشاؤم بمرئي أو مسموع أو زمان أو مكان)، وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ» (وهذا هو الأصل الجامع الذي تفرعت منه الأفعال السابقة وهو التوكل على الله وصدق اللجأ إليه)». فَقَامَ عُكَّاشَةُ بْنُ مِحْصَنٍ. فَقَالَ: ادْعُ الله أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: «أَنْتَ مِنْهُمْ» (وفي رواية البخاري قال النبي صلى الله عليه وسلم:«اللهم اجعله منهم») ثُمَّ قَامَ رَجُلٌ آخَرُ فَقَالَ: ادْعُ الله أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: «سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ». ولمسلم من حديث عمران: «وَلاَ يَكْتَوُونَ» (لا يطلبون من أحد أن يكويهم من باب العلاج)» وهي عند البخاري من حديث ابن عباس.

“Mitume na Ummah zao walionyeshwa kwangu; Mtume akiwa na watu kama kwamba hawafikii kumi, wakati Mitume wengine wakiwa na mtu mmoja au wawili tu, na pia kulikuwa na Mitume wengine wakiwa hawana hata mtu mmoja pamoja nao. Punde, Ummah wenye idadi kubwa umejitokeza (yaani, idadi kubwa ya watu wakaanza kukaribia kutokea mbali). Nikafikiria kuwa hawa ni Ummah wangu, lakini nikaambiwa kuwa alikuwa Musa na Ummah wake. Tena nikaambiwa angalia mbinguni. Nilipoangalia, niliona kundi jingine la watu lenye idadi kubwa zaidi, nikaambiwa kuangalia upande mwingine (Kama ilivyopokewa na Bukhari, idadi ya watu ilikuwa ni kama imejaza mbingu yote). Kisha nikaambiwa kuwa huu ni Ummah wa Mwenyezi Mungu (swt), na miongoni mwao kuna elfu sabini watakaoingia Peponi bila hesabu na adhabu. Kwa mujibu wa mapokezi, Mtume (saw) kisha akainuka kuelekea nyumbani kwake. Kisha watu wakaanza kujadili kuhusu alichokisema Mtume (saw) (mazungumzo yakakolea, na sauti zikapaa) yaani kuhusu hao watakaoingia Peponi. Baadhi walisema kuwa huenda wakawa ni masahaba wa Mtume (saw), wengine walisema huenda ni watu watakaokuwa wamezaliwa Waislamu na hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, na wengine walisema vingine. Juu ya hili Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akatoka nyumbani mwake na akauliza: Nini mnabishania? Watu wakamwambia Mtume (saw) kuhusiana na mjadala, ambapo Mtume akajibu: “Hawa ni watu wasiofanya ruqya au kutumia hirizi wala kuamini ushirikina (kwa sababu imani yao na kumtegemea kwao Mwenyezi Mungu ni yenye nguvu) na pia hawajiingizi katika masuala ya kishirikina, yaani kuzungumzia masuala ya kisirani mbaya anayetabiri ubaya (hili linatokana na neno “twayr”, ambalo asili ni kutabiri uzuri au ubaya, ambayo ni mambo yaliyoenea wakati wa kipindi cha ujahiliya, na hujumuisha namna zote za vitu, ima ziwe zinahusiana na yanayoonekana au kusikilikana, au kuhusiana na muda au mahala) na wakawa wanamtegemea Mola wao na Muumba Mwenyezi Mungu (swt), wakimuamini Yeye tu (huu ni msingi mpana kutokana nao matendo yote na sifa bainifu zinastawishwa, yaani, kutaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kujisalimisha Kwake kwa unyenyekevu). Aliposikia haya, Ukaashah bin Mihsan alisimama, na akamwambia Mtume (saw): Niombee kwa Mwenyezi Mungu anijaalie niwe miongoni mwao. Akasema Mtume (saw): “Wewe ni miongoni mwao.” (Katika mapokezi ya Sahih Bukhari, Mtume (saw) alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu, mjaalie awe miongoni mwao” kisha akasimama mtu mwingine akasema: “Niombee kwa Mwenyezi Mungu anijaalie niwe miongoni mwao.” Akasema saw: “Amekutangulia Ukaashah”. Na kutoka kwa Muslim katika hadith ya Imran (ra), na katika hii imesemwa kuwa “Wala hawatii doa (kupitia moto, wenyewe au wengine, kwa ajili ya kutibu)”. Bukhari ameipokea hadithi hii kutoka kwa Ibn Abbas (ra).

Hadith imemuweka katika nafasi ya juu na ya heshima mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) akhera yule anayemtegemea Mwenyezi Mungu pekee. Mtu aina hiyo ataingia Peponi bila ya hesabu na adhabu, kwa kuwa anategemea kwa Mwenyezi Mungu tu badala ya kupulizia baada ya kisomo, au kujiingiza kwenye masuala ya ndege mbaya, ushirikina na uunguzaji (kwa chuma). Hii ni alama ya kiwango kikubwa cha Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt). Hadith pia imetaja ubora wa Mtume (saw) kwa kutaja wingi wa wafuasi wake, na ubora wa Ummah wake juu ya Ummah nyingine, na kutakuwa na watu kutoka katika Ummah wake ambao wanamtegemea zaidi Mwenyezi Mungu (swt) peke yake. Kuna daraja tofauti za Imani, na ya juu zaidi ni kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt).

Juu ya kuwa hukmu za kisharia juu ya kujipulizia baada ya kisomo cha Quran (Ruqya) kuwa imeruhusiwa, lakini ni bora zaidi kuyawacha mambo yako kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kujipulizia baada ya kisomo cha majina matukufu ya Mwenyezi Mungu (swt), au dua zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (saw), zote zinakubaliwa. Hata hivyo, ni muhimu kuamini kuwa matendo haya sio yenye kuathiri yenyewe, lakini kuwezekana kwake ni pindi tu akitaka Mwenyezi Mungu (swt). Wanachuoni wana rai ya kuwa hii pia ni dalili kutoka kwa Sunnah za Mtume (saw), alikuwa akisoma Ayah na kupulizia kwa mgonjwa. Katika Sahihi mbili (Bukhari na Muslim), pia kunapatikana Ushahidi wa Hadith iliyopokewa kutoka kwa Aisha (ra), ambapo imetajwa kuwa Jibriil (as) amefanya haya kwa Mtume (saw). Masahaba pia walikuwa wakisoma Ayah na majina matukufu (ya Mwenyezi Mungu) na kisha kupulizia, na kama hivyo alifanya Aisha (ra). Hii ni kama ilivyo kwenye Hadith iliyowafikiwa juu yake-Bukhari na Muslim-iliyopokewa kutoka kwa Abu Said (ra), ambapo Sahaba alisoma na kupuliza kwa kiongozi wa kijiji aliyekuwa mgonjwa. Alipoelewa hili, Mtume (saw) alimuuliza Abu Said (ra), «وما أدراك أنها رقية» “Umejuaje kuwa inaweza kufanyika namna hiyo?” Wanachuoni pia wamechukua rai hii kuwa kama mtu amefanya wema kwa mwenzake, basi kwanini atakiwe kuzuwia wema wake? Mtu mmoja alimuuliza Mtume (saw),

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Naweza kusoma na kupulizia? Mtume (saw) alisema (من استطاع منكم أن ينفع أخاه فليفعل) “Yeyote atakayeweza kati yenu kumnufaisha ndugu yake, basi na afanye.” Imepokewa na Muslim kuwa Mtume (saw) alisema: «لا بأس بالرقى ما لم تكن شركًا» “Hakuna ubaya kupulizia ikiwa hakuna shirki.” Kulingana na maneno ya Mtume (saw), “wasisome na kupulizia”, inamaanisha hawahitajii “kisomo na kupuliza” kwa jina jingine lolote lisilokuwa Mwenyezi Mungu (swt). Ina maana kuwa yeyote anayetaka kupata wema elfu sabini, yaani Pepo bila adhabu au hesabu, asisome na kupulizia, kwa sababu katika hadith, neno ‘istirqaa’ limetajwa. Hapa herufi alif, siin na tee zinaonyesha kutaka. Hii inamaana watu watakaoingia Jannah bila hukumu hawahitaji kupulizia baada ya kisomo, juu ya kuwa ni ruhusa, ambayo ni alama ya Imani kamili na kujisalimisha mtu kwa Mwenyezi Mungu (swt), na ni alama ya kutoshirikisha Imani yao kutoka kwa mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo, mtendaji wa kupulizia baada ya kisomo huamini kuwa inaruhusiwa, na kuwa kuna ponyo ndani yake baada tu ya Mwenyezi Mungu kutaka. Hivyo hivyo, huamini pia kuwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndio Mponyaji, na Yeye (swt) anajuwa hali halisi ya mtu; ni Mwenyezi Mungu (swt) anayetoa mafanikio katika kazi yake, na anatuliza ukali wa maumivu ya hali yake. Muislamu anayeachana na kupulizia maana yake ni kuwa anaridhia kile kinachomridhisha Mwenyezi Mungu (swt), ima atapona ama la, yaani mambo yake yote anayaegemeza kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Kulingana na Hadithi, maneno “لَاَ يَتَطَيَّرُون” (hili linatokana naطیر, lenye maana ya ndege), kumaanisha kuagua ndege wabaya kutokana na matendo ya ndege, kama ilivyokuwa tabia za kale za Uarabuni. Ilikuwa ni maarufu katika siku za zamani kama ndege akionekana kutokea kaskazini, au akiruka kurejea, Waarabu wakichukulia kuwa ni ndege mbaya (kisirani), na kama akielekea mbele, basi huchukuliwa kuwa ni dalili njema, na hii ndio sababu kwa nini ishara ya ndege ikajulikana kuwa ni  تَطَیُّرyaani inayohusiana na ndege. Hata hivyo, kimsingi hii huchukuliwa ni jumla kwa kila ishara ya ndege, ima iwe inahusiana na ndege ama la, kwa mfano, inaposikilikana sauti ya kuchukiza, na ikawa ni jambo la kawaida kuhusishwa na bahati ya mtu ya muda huu au ujao na ikawa watu wanatumia muda wa usiku na mchana wakiisubiria. Inatokezea pia likawa jambo linajulikana kwa watu, lakini likawa halina mashiko ya uhalisia, wakawa wameanza kuliamini kuwa ni kweli na baadaye kulichukulia kuwa ni ndege mbaya. Kwa mfano, kuchukulia baadhi ya siku kuwa zenye kunufaisha au kudhuru. Hukumu ya Uislamu juu ya kuchukua ubashiri kutoka kwa kitu chenye kuonekana, kusikika au kujulikana ni haram. Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abu Hurairah katika Sahihain inaonyesha uharamu wake. Mtume (saw) amesema:  «لا عدوى ولا طيرة» وعن أنس رضي الله عنه قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لا عدوى ولا طيرة ويعجبني الفأل» قالوا: وما الفأل؟ قال صلى الله عليه وسلم: «الكلمة الطيبة»

“Hakuna ushirikina, wala ndege mbaya” na kutoka kwa Anas (ra) kuwa Mtume (saw) alisema: “Hakuna ushirikina, wala ndege mbaya, na ninapenda al fa-al (chenye bishara njema)”. Masahaba wakauliza: Nini al fa-al? Mtume (saw) akajibu: “Tamko zuri”. Hadithi hii imewafikiwa juu yake. Kwa hivyo, Hadith inalaumu ndege mbaya. Kuamini ndege mbaya pia ni kinyume na Imani ya Tauhid (Umoja wa Mwenyezi Mungu (swt)), kutokana na kuwa mtendaji wa masuala haya anapoteza utegemezi wa Mwenyezi Mungu (swt) na badala yake kutegemea juu ya vitu vingine, na kujenga mahusiano na kitu kisicho na uhakika. Kulingana na hili la (وَلَايْكْتَوُونَ) “wala msichome kwa chuma”, inaonyesha kuwa hili na kutibu kupitia hii (kwa moto) linazuwia kufikia kupata wema wa elfu sabini.

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusiana na tendo la matibabu ya kuchoma; baadhi yao wanalipinga, na wengine wanalitaja kuwa linafaa. Hata hivyo, Ibn Abas (ra) amenukuliwa katika Sahihi mbili, hadithi ya Mtume (saw) inayosema: «الشفاء في ثلاث: في شرطة محجم، أو شربة عسل، أو كيٍ بنار، وأنا أنهى أمتي عن الكي» “Matibabu yapo katika vitu vitatu, katika kufanya hijama, au kunywa asali, au kuchoma kwa kutumia chuma kimoto, na mimi nimewakataza Ummah wangu kuchoma kupitia chuma kimoto.” Katika mapokezi mengine kwenye Sahihi mbili, imepokewa kuwa Mtume (saw) amemfanyia tiba ya kuchoma Saad ibn Muadh. Kutokana na Hadithi hizi ndipo kumepatikana ikhtilafu baina ya wanachuoni kuhusiana na hukmu juu ya matibabu ya kuchoma. Inaweza kutetewa, hasa katika mazingira ya kuhitajiwa, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi. Kile kinachoonyesha kuchukizwa kwake katika Hadithi ni kuwa kuiwacha ni jambo zuri zaidi. Ibn Qayyim (ra) amepangilia Ushahidi wote huu kwa vizuri. Amesema, “Kuna aina nne za Hadith: Moja inaonyesha (kuchoma kupitia moto) kumekuwa kukifanywa, hadithi nyingine inaonyesha kuwa Mtume (saw) ameichukia, ya tatu inamsifia yule anayeacha kufanya matibabu ya kuchoma, na ya nne inakataza. Hata hivyo, hakuna mgongano au kutopatana baina ya hadithi hizi. Kwa sababu kitendo cha Mtume (saw) cha kuchoma kwa Saad ibn Muadh kinajuzisha kuwa inawezekana kufanywa, lakini kwa kutokipendelea kwake Mtume (saw) hakuonyeshi ukatazo. Na kupongezwa kwa mwenye kuwacha kuifanya kunaonyesha kuwa ni bora zaidi kuiwacha. Kulingana na suala la kukatazwa, humaanisha ima kuchukiza au kwa kusababisha kwake (kuchoma kupitia moto) wakati hakuna ulazima (kwa kumtibia mgonjwa), kunakoweza kusababisha hofu ya ugonjwa kwa (baadaye). [Zad al-Ma’ad, Li Ibn al-Qa’im al-Jawzia]

Kulingana na kauli ya Mtume (saw) «وَعَل فض رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ» “na wanategemea kwa Mola wao pekee (swt)”, inarejea kwa uzuri wa kumtegemea Mwenyezi Mungu na nafasi yao ya juu. Haya ni maneno ambayo ni msingi wa sifa zote zilizotangulia; nayo ni, wale (elfu sabini watakaoingia Peponi bila hesabu au adhabu) hawataki hirizi au kujiingiza katika masuala ya ndege wabaya, na wanamtegemea Mwenyezi Mungu (swt) peke yake. Wanaepuka mambo haya kwa sababu wana Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt).   

Nini hasa Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt)? Hiyo ni kutegemea rehema za Mwenyezi Mungu (swt) katika jambo kwa ukweli na moyo safi, na kuchukuwa njia inayolazimu katika jambo hilo. Kuwa na kinaya kwa fikra ya kuwa Mwenyezi Mungu anamtosheleza kwani Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha, [وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُ] “Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha” Utegemezi juu ya Mwenyezi Mungu (swt) unahitaji kuwa mtu afanye bidii kufikia malengo, kwa kuwa kutotenda kunadhihirisha uvivu na sio kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt). Ibn al-Qayyim amesema: watu wamekubaliana ya kuwa kutegemea (juu ya Mwenyezi Mungu (swt)) hakugongani na utumiaji wa bidii (kwa ajili ya kufikia lengo). Kutegemea (juu ya Mwenyezi Mungu (swt)) kutakuwa ni sahihi pindi tu mtu atakapofanya bidii kwa ajili ya lengo husika. (Madarij As-Saalakin). Pia huruhusika kwa mtu kuelezea nia yake ya kuwa ametegemea juu ya Mwenyezi Mungu (swt) katika jambo kadha na kadha. Pili, pia ni dhihirisho la mapenzi na utiifu wa mtu kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:41

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu