Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni mkubwa Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Waislamu kwa Jumla na Mashababu (wa Hizb ut Tahrir) Hasa katika Sikukuu ya Idd Al-Adha 1446 H sawia na 2025 M
- Imepeperushwa katika Hotuba
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Idd hii inawasili na uvamizi wa Kiyahudi, unaoungwa mkono na Marekani na silaha zake, bado unaendelea dhidi ya Gaza Hashim na Palestina yote. Na watawala katika nchi za Waislamu wanatazama yanayotokea, mbora wao ni yule anayepatanisha kana kwamba yuko kundi lisilofungamana na upande wowote, bali yuko karibu zaidi na Mayahudi. Si ajabu kwamba Marekani, makafiri wakoloni na umbile lao, dola ya Kiyahudi, wanatushambulia. Ni maadui wa Uislamu na Waislamu, sio kuanzia leo bali wa miaka iliyopita.