Kupigania Utukufu wa Kijeshi na Kiraia Kumeifikisha Pakistan kwenye Ukingo wa Maangamivu. Uokovu Wetu Pekee ni kwa Utukufu wa Shariah, kupitia Kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa muda wa wiki kadhaa zilizopita, siasa za Pakistan zimeshikiliwa na ubabe, uhasama, machafuko na ukosefu wa utulivu. Sababu ya mgogoro huu wa kisiasa ni mapigano ya kindani ya makundi ya wenye ushawishi kati ya majaji, majenerali na wanasiasa. Hakuna kundi lolote linalojali matatizo halisi ya watu.