Vichwa vya Habari: 10/08/2022
- Imepeperushwa katika Vichwa vya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Serikali ya Bangladesh ilipandisha bei ya mafuta kwa asilimia 42 hadi 51, ambalo ndilo ongezeko kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Serikali ya Bangladesh ilipandisha bei ya mafuta kwa asilimia 42 hadi 51, ambalo ndilo ongezeko kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Makubaliano yalitiwa saini jijini Istanbul kati ya Urusi na Ukraine kupitia upatanishi wa Umoja wa Mataifa (UN) na Uturuki kwa ajili ya kuregesha mauzo ya nafaka kutoka bandari za Ukraine.
BP imeripoti faida yake kubwa zaidi ya robo mwaka kwa miaka 14 baada ya bei ya mafuta na gesi kupanda.
Bangladesh yakabiliwa na miaka mingine mitatu ya kukatwa kwa umeme huku taifa hilo linaloendelea likitatizika kupata mahitaji ya muda mrefu ya gesi asilia na bei yake iko nje ya soko la hapo kwa hapo.
Majeshi ya Misri, Jordan, Hijaz na Uturuki yanawatazama Mayahudi wakiupiga mabomu Ukanda wa Gaza, lakini hawahamasiki, kana kwamba jambo hilo haliwahusu!
Rais Erdoğan anakwenda Sochi mnamo Agosti 5 kukutana na kiongozi wa Urusi Putin. Erdoğan na Putin watajadili ukanda wa nafaka, vita vya Ukraine na Urusi, uwezekano wa operesheni ya Uturuki Syria na Kiwanda cha Nyuklia cha Akkuyu.
Benki ya Uingereza mnamo Alhamisi ilitetea uamuzi wake wa kuongeza viwango vya riba kwa haraka zaidi katika kipindi cha miaka 27,
Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba al-Zawahiri awe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) anawahuisha pamoja Naye, akiwaruzuku wote, na kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amjaalie daraja za juu kabisa za Pepo na starehe, kama ambavyo Yeye (swt) amruzuku shufaa kwa familia yake.
Baraza la mawaziri la federali lilikuwa limeidhinisha agizo mnamo Alhamisi la kuuza hisa za makampuni ya mafuta na gesi na mitambo ya kuzalisha umeme inayomilikiwa na serikali kwa Imarati ili kukusanya dolari bilioni 2 hadi bilioni 2.5 ili kuepusha kushindwa kulipwa madeni.