Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (466)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Maisha haya ya dunia ni kama dimbwi la hasara, ambalo ni wale tu wanaojua kukamata fursa ndio wataokolewa. Kwa sababu hii, Siku ya Kiyama inaitwa “Siku ya Majuto,” kwa sababu watu wengi wamezama katika hasara ya kidunia, na wameshindwa kutumia fursa za thamani walizopewa katika maisha yao. Walipoteza kwa urahisi nyakati za dhahabu alizozitoa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya mwamko na izza ya Umma.