Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yahuisha Ibada ya Takbira Katika Mwezi wa Dhul-Hijjah kwa Matembezi ya Kishindo katika Soko Kuu la Port Sudan
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya swala ya Alasiri mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 6 Dhul-Hijjah 1446 H, sawia na tarehe 2 Juni 2025 M, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walihuisha ibada ya takbira katika mwezi wa Dhul-Hijjah. Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alihutubia waumini katika Msikiti wa Ibn Mas’ud katika soko kuu la Port Sudan baada ya Swalah ya Alasiri, akiwakumbusha juu ya ubora wa siku hizi zilizobarikiwa za Dhul-Hijjah, na jinsi Maswahaba – Mwenyezi Mungu awe radhi nao – walivyozitukuza siku hizi kwa takbira na tahleel. Kisha akaanza kupiga takbira, ikifuatiwa na dua. Baadaye wote wakatoka kwa matembezi ya kishindo wakiwa wamebeba Rayah (bendera) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na alama kubwa isemayo: "Kuhuisha Ibada ya Takbira katika Mwezi wa Dhul-Hijjah."