Jibu la Swali: India, Pakistan, na Usitishaji Mapigano
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Trump alitangaza kwa mshangao jana, Jumamosi, katika chapisho kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Kijamii (Truth Social platform), kwamba "Baada ya usiku mrefu wa mazungumzo yaliyopatanishwa na Marekani, ninafurahi kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubali kusitishwa kwa mapigano kamili na mara moja, "na kuzisifu nchi zote mbili kwa kutumia busara na akili kubwa." (Al Jazeera, 11/5/2025) ... ni upi ukweli katika uhasama na mzozo huu? Je, Mkataba wa Maji wa Indus ni nini haswa ambao India imeusitisha kwa muda? Je, Marekani inahusika katika kuanzisha shambulizi hilo na pia kulisitisha?