Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 571
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maelfu ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Indonesia walifanya matembezi yanayounga mkono Palestina mnamo Oktoba 18 na 19, 2025, chini ya kauli mbiu “Palestinaingali chini ya Uvamizi.” Huko Bandung, zaidi ya waandamanaji 15,000 walikusanyika mbele ya jengo la Gedung Sati, wakinyanyua bendera za Rayah zenye tamko la Tawhid na mabango yenye kauli mbiu kama vile “Tumeni majeshi ya Kiislamu, yakomboe Palestina!”, na “Suluhisho la mwisho kwa Palestina ni kupitia jihad na Khilafah,” na “Palestina itakombolewa kupitia Khilafah na Jihad.”
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari “Kuweni Waangalifu, Vita Bado Havijakwisha!”
Serikali ya Misri ilitangaza kusherehekea utekelezwaji wa mpango wa Trump mjini Gaza. Sisi alimwalika Rais wa Marekani kusherehekea kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa mpango wa Gaza: [Rais Trump wa Marekani alisema mnamo Alhamisi kwamba mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru mnamo Jumatatu au Jumanne ya wiki ijayo, na kwamba bado analenga kuzuru eneo hilo kusherehekea hafla hii... “Ni muhimu kutaja kuwa Rais Sisi wa Misri alikuwa amemwalika Trump kushiriki katika sherehe ambazo zitafanywa nchini Misri ili kuadhimisha kutiwa saini kwa makubaliano, akiyachukulia kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo yanazifisha taji juhudi za Misri, Marekani, na wapatanishi katika kipindi cha hivi karibuni.” (CNN Arabic, 9/10/2025)]
Al-Waqiyah TV: Lau Wangekuwa Wakweli kwa Mwenyezi Mungu ﷻ... watawala wetu hawangekuwa na kiburi!
Al-Waqiyah TV: Kwa Mukhtasari... Kuwadhibiti Wanaodhulumiwa... Kwa Dhulma Zaidi?!