Jibu la Swali: Mashambulizi ya Droni na Yanayojiri katika Vita nchini Sudan
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Siku za hivi karibuni zimeshuhudia maendeleo ya ajabu katika vita. Droni zilishambulia Port Sudan, mji mkuu wa utawala, kwa siku sita mfululizo, na kushambulia uwanja wa ndege wa kiraia, kambi ya anga, na maghala ya mafuta, na kusababisha mgogoro wa mafuta kote nchini. Droni pia zilishambulia mji wa Kassala kwenye mpaka wa Eritrea upande wa mashariki, pamoja na miji mingine. Haya yote yalisababisha vikosi vya jeshi kuondoka kuelekea upande wa El Fasher na kuzingatia kulinda Sudan mashariki, kama BBC ilivyoripoti mnamo tarehe 10/5/2025. Je, hii ina maana kwamba shambulizi la mashariki mwa Sudan linalenga kuliondoa jeshi kutoka Darfur, na kuiacha ikiwa chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) pekee? Je, matukio haya ni utangulizi wa Jukwaa la Jeddah (kongamano la mazungumzo)? Au kuna malengo mengine?