Pongezi kutoka Kote Ulimwengu kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Al-Mubarak 1445 H
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Pongezi kutoka kote Ulimwengu kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Al-Mubarak 1445 H
Pongezi kutoka kote Ulimwengu kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Al-Mubarak 1445 H
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kitengo cha Wanawake “Iregesheni Ramadhan katika Njia Yake ya Mwanzo”
Karibu Ramadhan, mwezi wa ushindi, mwezi wa bishara njema, mwezi wa kujadidishwa imani na kutakasa nyoyo, mwezi wa utiifu na kushindana katika mambo mema. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetufikisha Ramadhan, mwezi huu mtukufu ambao tunahisi ndani yake maana ya rehema na umoja baina ya Waislamu. Karibu, Ramadhan.
Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mkesha huu wa Jumatatu, muandamo wa mwezi mpya kwa mujibu wa matakwa ya Shariah unathibitishwa, na kwa hiyo kesho, Jumatatu ni siku ya kwanza ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1445 H.
Filamu ya Makala “Palestina Yote ni Wajibu Ikombolewe!"
Katika mwezi wa Rajab Tukufu mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi kwetu kumbukumbu ya uchungu ya miaka 103 H na 100 M ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo iliasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw), na maswahaba zake watukufu (ra), na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H, sawia na 03/03/1924 M, na ardhi iliyobarikiwa (Palestina) ilipotea kwa kupotea Imam ambaye ni ngao, Khalifa wa Waislamu ambaye kwaye wanapigana nyuma yake na kujihami..
Kwa Majeshi katika Ardhi za Kiislamu: Je, hamna nyoyo za kuhisi, macho ya kushuhudia, na masikio ya kusikia? Je, hamuoni mito ya damu inayotiririka kutoka kwa watoto wa Waislamu huko Gaza?
Enyi Majeshi katika Nchi za Kiislamu, Inatosha!
Je, Munasubiri amri ya Watawala ndipo muinusuru Gaza Hashem?!
Katika mwezi Mtukufu wa Rajab wa mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi tena kumbukumbu uchungu ya 103 ya kuvunjwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume wote Muhammad, rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na maswahaba zake watukufu, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa Mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na 3 Machi 1924 M
Huku umbile halifu la Mayahudi (Wazayuni) likiendelea na ulipuaji mabomu wa kinyama na kikatili wa Gaza, wanawake na watoto ndio wanaohimili uzito wa mauaji haya ya halaiki ambayo yamesababisha vifo na majeraha kwa zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu elfu 72 hadi kufikia sasa