Vichwa vya habari 15/04/2020
- Imepeperushwa katika Vichwa vya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Polisi wamewakamata zaidi ya madaktari 150 na wafanyikazi wengine wa matibabu nchini Pakistan katika jiji la Quetta, tukio hilo lilitokea baada ya madaktari kuandamana dhidi ya ukosefu wa vifaa vya kisawa sawa vya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona wakati wa kutibu wagonjwa.
Janga la virusi vya korona ndio janga mbaya zaidi la kiulimwengu tangu Vita vya Pili vya Dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa - Antonio Guterres alisema siku ya Jumanne, akieleza namna janga hilo litakavyochochea mizozo duniani kote.
Mwishoni mwa wiki, Amerika iliipiku China kwa idadi ya watu waliofariki kwa mkurupuko wa virusi vya korona, uongozi wa kiulimwengu umeonekana kutokuwepo katika muundo wa utawala wa kiulimwengu.
Kuendelea kusambaa kwa virusi vya korona kumepelekea michezo ya kivita kucheleweshwa, lakini sio kwa Amerika na Umoja wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwani wanajeshi 4,000 wa Amerika na wapiganaji wa UAE walichanganyika na kufanya mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka mara mbili ya Ghadhabu Asili.
Janga linalozidi kukuwa la virusi vya korona linatishia zaidi uchumi wa Amerika kuliko zama nyingine zozote tangu hatua za mwanzo za Muanguko Mkubwa miaka 90 iliyopita.
Katika hatua ya kijinga inayofanana na uongozi wake, Mwana wa Mfalme wa Saudi Mohammad Bin Salman, anayejulikana kama MBS, alibuni janga la mafuta wiki hii lililoshinikiza masoko ya fedha na linaweza kuwaharibia wazalishaji mafuta wa Amerika.
Hii ni kufuatia msururu wa kuwakamata wanawa wafalme wa ngazi za juu, Mwana Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman aliwaweka chini ya ulinzi wana wafalme wakuu.
Maafisa wa Uturuki walisema kwamba mtu mmoja alijeruhiwa vibaya baada ya vikosi vya usalama vya Ugiriki kutumia silaha za moto kuwapiga wahamiaji waliokua wamekusanyika katika mpaka mnamo Jumatano.
Makubaliano ya amani yalisainiwa kati ya Taliban na Amerika kwa mbwembe na nderemo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha na Kabul.