Ijumaa, 20 Rajab 1447 | 2026/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hofu Halisi ya Magharibi: Ulimwengu wa Kiislamu Ulioungana

(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano ya hivi karibuni ya Fox News na Sean Hannity, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alifufua usemi maarufu wa “Uislamu wenye msimamo mkali,” Khilafah inayopanuka, na vitisho kwa Magharibi. Maoni yake hayarudii tu miongo miwili ya ujumbe wa baada ya 9/11 lakini pia yanafichua jambo la kina zaidi - hofu ya msingi ya ulimwengu wenye nguvu wa Kiislamu ulioungana.

Hannity aliunda maswali yake katika muktadha wa fikra ya “Amerika Kwanza” inayopigiwa debe na Trump. Ili kuelewa jibu la Rubio, mtu lazima akumbuke enzi ya kihafidhina mamboleo ya miaka ya 2000, wakati sera ya kigeni ya Marekani ilizunguka uvamizi, mabadiliko ya utawala, ujenzi wa taifa na “kuiingiza demokrasia” Mashariki ya Kati. Hili lilifanyika na linaendelea kutekelezwa chini ya kivuli cha kukuza mfumo wa kiliberali huku ikipanua ushawishi wa Marekani duniani na kulinda mradi wa Kizayuni na udhibiti wake wa kikanda.

Amerika ilitumia matrilioni ya dolari kwenda Iraq na Afghanistan, lakini ikakabiliwa na vikwazo, fedheha, na sifa ya kimataifa iliyochafuliwa na vita visivyokwisha. Na bado, matamshi ya MAGA ya leo, licha ya kudai kukataa uhafidhina mpya wa enzi ya Bush yanaakisi mantiki hiyo hiyo - hofu ya Uislamu, hofu ya maumbo ya Kiislamu “yanayopanuka”, mazungumzo ya WMD, kuwadhalilisha wapinzani wa kisiasa wa kijiografia na kutengeneza uuungaji mkono wa umma kwa ajili ya kuingilia kati. Lugha ya hivi karibuni inayotumika kuhusu Venezuela inayonasibisha serikali yake na “magaidi wa dawa za kulevya” wanaohusishwa na “Uislamu wenye msimamo mkali” ni mfano kamili wa ujumbe wa neocon uliofufuliwa chini ya chapa tofauti lakini matarajio yaleyale ya kibeberu.

Waenezaji wa hofu wa Rubio “Uislamu wenye msimamo mkali” kama nguvu ya mapinduzi iliyojikita katika udhibiti wa kimataifa. Anasema, “hawataridhika kamwe na Khilafah yao ndogo...wanataka kupanuka... kudhibiti eneo zaidi...wana miundo huko Magharibi, Marekani, Ulaya...” Na bado, haoni unafiki wa ubeberu wa Marekani unaodumisha zaidi ya kambi 750 za kijeshi kote ulimwenguni, maelfu ya wanajeshi nchini Japan, Korea Kusini, Ujerumani, Italia na ulimwengu wa Kiislamu na unaendelea kuunga mkono upanuzi wa eneo la umbile la Kizayuni ambalo kimsingi hufanya kazi kama kambi ya operesheni ya Amerika katikati ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kote katika ulimwengu wa Kiislamu, upinzani dhidi ya nguvu za Marekani umekuwa ukizingatia sera yake ya kigeni ambayo huweka au kuunga mkono tawala za kimabavu, hutengeneza mapinduzi, huteka na kushambulia ardhi za Waislamu, hutekeleza vikwazo vya kiuchumi, huingilia utawala, hulazimisha usekula na kupinga Uislamu. Athari za jumla za sera hizi zinaonekana nchini Afghanistan, Iraq, Libya, Pakistan, Palestina, Somalia, Sudan, Yemen na kwengineko. Maelfu wameuawa, mamilioni wamehamishwa, miundombinu imevunjwa, na kuanguka kwa uchumi si mambo ya kufikirika, bali ni mambo halisi yaliyopo. Kuuonyesha upinzani wa matokeo kama hayo kama uadui dhidi ya “uhuru” ni kujikweza kwa udanganyifu.

Kupinga Khilafah

Kwa zaidi ya karne moja, itikadi ya kimkakati ya Kimagharibi imekuwa ikipinga kuibuka tena kwa mamlaka ya kisiasa ya Kiislamu yaliyomo ndani ya Khilafah. Upinzani huu hautokani tu na kutokuwa na utulivu kithaqafa au wasiwasi kuhusu msimamo mkali. Badala yake, unaendeshwa na hali halisi ya siasa za kijiografia, kiuchumi, na kimfumo. Khilafah kihistoria ilifanya kazi kama dola kubwa na kufutwa kwake kuliwezesha udhibiti wa Magharibi wa ulimwengu wa Kiislamu. Kusimamishwa kwake upya kunatishia mfumo wa sasa wa kimataifa kupitia jiografia yake ya kimkakati, rasilimali nyingi, ukubwa wa idadi ya watu, na uhuru wa kifikra.

Tawala za kimabavu katika ulimwengu wa Kiislamu ni sehemu ya mpango wa Magharibi wa kuzuia kusimamishwa tena kwa Khilafah. Hasira ya umma dhidi ya serikali za Kiislamu haitokani na msimamo mkali wa kinadharia, bali kutokana na uzoefu wa maisha chini ya utawala wa kimabavu unaoungwa mkono na udhibiti wa kikoloni wa kigeni.

Katika muktadha kama huo, kuitazama Marekani kama dola ya uharibifu sio matokeo ya kufundishwa siasa kali; badala yake, ni usemi wa busara wa ukandamizaji endelevu. Maoni ya Rubio yanaonyesha hofu hii kubwa zaidi ya Ummah ulioungana kweli. Yanafichua wasiwasi juu ya mmomonyoko wa udhibiti wa Marekani na uwezekano kwamba kambi kubwa ya kihadhara inaweza kujipangia njia yake yenyewe. Kuelewa hili ni muhimu. Kuogopa kuhusu “Uislamu wenye msimamo mkali” na vitisho vya usalama katika muktadha huu sio kuhusu kuwalinda raia au hata hofu ya dini. Badala yake, ni kuhusu kuhifadhi himaya.

Kuunganisha Ummah na Hizb ut Tahrir

Kusimamishwa tena kwa Khilafah sio “Uislamu wenye msimamo mkali.” Badala yake, ni sehemu ya Uislamu wa kawaida. Khilafah ni uongozi wa kisiasa wa Ummah wa Kiislamu wa kimataifa unaotabikisha Uislamu. Ni faradhi, sio khiyari. Kukosekana kwake ni dhambi.

“Wao (wanazuoni) walikubali kwamba ni faradhi kwa Waislamu kumteua Khalifah, na kwamba faradhi yake ni kupitia wahyi, sio akili. (Imam an-Nawawi, Sharh Sahih Muslim)

Hizb ut Tahrir imekuwa mstari wa mbele kwa miongo kadhaa katika juhudi za kusimamisha tena Khilafah na kuunganisha Ummah. Hizb ut Tahrir inajitokeza kama chama cha kisiasa cha Kiislamu cha kimataifa kinachotofautishwa na uthabiti wa ruwaza yake na kina cha misingi yake ya kifikra. Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1953, mjini al-Quds, Jerusalem, Hizb ut Tahrir iliibuka na lengo moja na kutengeneza fasihi za kina zinazoelezea muundo wa Khilafah, mipangilio yake ya idara, mifumo yake ya kiuchumi, ya kimahakama, na ya kisiasa na rasimu ya katiba.

Kazi hizi hazikutolewa kama mazoezi ya kitaaluma au uvumi wa kifalsafa, wala kama kuomba msamaha tu kwa wakosoaji wa Uislamu. Badala yake, zimekusudiwa kama muundo wa kivitendo wa utabikishaji ulio wazi. Mwelekeo huu wa vitendo unaonyesha ruwaza inayotazama mbele, sio kumbukumbu za zamani za kusikitisha, bali imani katika uwezo wa Uislamu wa kutoa masuluhisho kwa sasa na mustakabali. Ruwaza yetu ni kufufua mfumo mpya wa kimataifa unaozingatia haki, uwajibikaji, na mwongozo wa kiwahyi, unaojumuishwa ndani ya kuregea kwa Khilafah Rashida, inshaAllah.

Leo, Hizb ut Tahrir inafanya kazi kama chama cha kisiasa cha kimataifa kuanzia Amerika hadi Australia. Katika mazingira tofauti ya kitamaduni na kisiasa, imedumisha uthabiti wa kifikra na nidhamu ya mbinu. Licha ya kukabiliwa na mateso, vikwazo, na kutengwa na vyombo vya habari katika sehemu nyingi za dunia, hizb imeendelea kuelezea ujumbe wake kwa uvumilivu na azma, ikihamasisha kupitia njia zisizo za vurugu za kifikra na kisiasa ili kusimamisha Khilafah katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa miongo kadhaa, Hizb ut Tahrir imechangia pakubwa katika kuinua mazungumzo ndani ya Ummah wa Kiislamu, haswa kwa kuzingatia upya fikra ya kisiasa kuzunguka lengo la kusimamisha tena Khilafah. Urithi wake haupo tu katika misimamo ambayo imeichukua, lakini katika kusisitiza kwake kwamba Waislamu wafikirie zaidi ya siasa za jazba na marekebisho ya muda mfupi, kuelekea ruwaza kamili iliyojikita katika Uislamu wenyewe. Katika ulimwengu unaotafuta njia badali za mfumo wa sasa wa ulimwengu unaofeli, Hizb ut Tahrir inaendelea kuwasilisha wito thabiti, wenye maadili, na wenye msingi wa kifikra wa kuunda upya ulimwengu kuelekea mustakbali wa haki na wenye heshima kwa Ummah na ubinadamu kwa jumla.

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “...na kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume.” (Musnad Ahmed)

H. 1 Rajab 1447
M. : Jumapili, 21 Disemba 2025

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu