Jumamosi, 30 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Waislamu: Kufunga Vyumba vya Ibada ni Shambulizi kwa Uislamu
na Lazima Kukabiliwe kwa Upinzani Mkali, wa Pamoja wa Kisiasa
(Imetafsiriwa)

Baada ya mwelekeo hasi wa kisiasa kwenye vyumba vya ibada, idara ya Chuo Kikuu cha Copenhagen iliamua mwishoni mwa Novemba kufunga kile kinachoitwa “vyumba vya utulivu,” ambavyo Waislamu walikuwa wakivitumia kwa zaidi ya miaka ishirini, bila matatizo yoyote, na wanafunzi na wafanyikazi kuswali swala za kila siku. Uamuzi huu kwa mara nyingine tena umezua mjadala kuhusu vyumba hivi na kuhusu kama kunapaswa kuwepo na nafasi kwa Waislamu kutekeleza swala zao katika taasisi za elimu.

Mapema mwaka huu, Chuo Kikuu cha Kusini mwa Denmark huko Odense kilifunga “chumba chake cha kutafakari,” kufuatia utata kuhusu ukweli kwamba chumba hicho kilitumiwa hasa na Waislamu na hakikuchukuliwa tena kama “kisichoegemea upande wowote.”

Maamuzi haya yaliyotolewa na idara za vyuo vikuu hivyo bila shaka ni matokeo ya shinikizo la kisiasa dhidi ya Uislamu ambalo limeongezeka katika miaka ya hivi karibuni hasa kuhusu vyumba vya ibada. Shinikizo hili limetolewa na wanasiasa mashuhuri, akiwemo Waziri Mkuu, kupitia madai ya uongo yanayodai kwamba vyumba hivi vimetumiwa kufanya ukandamizaji dhidi ya wasichana wa Kiislamu na kile kinachoitwa kama “udhibiti wa kijamii.”

Waziri Mkuu, Mette Frederiksen, alitumia vibaya Siku ya Katiba wakati wa msimu wa kiangazi kutekeleza aina ya ubabe wa kimaadili na ufuatiliaji wa nguvu dhidi ya Waislamu. Aliliambia Shirika la Habari la Ritzau mnamo tarehe 5 Juni kwamba kuwepo kwa vyumba vya ibada katika taasisi kadhaa za elimu ni “matatizo makubwa,” akisema kwamba wanafunzi lazima “wawe huru kutokana na shinikizo la kidini.” Aliongeza: “Hili haliwezi kupatikana ikiwa, kwa mfano, kuna chumba cha ibada cha Waislamu ambacho udhibiti wa kijamii na ukandamizaji hutokea ndani ya taasisi za elimu.”

Wakati huo huo, alitangaza kwamba Mawaziri wa Shule na Elimu lazima wafafanue, kupitia mazungumzo na vyuo vikuu, kwamba vyumba vya ibada havipaswi kuwepo katika taasisi za elimu. Mbali na hayo, Waziri Mkuu alitaka kupanua marufuku ya niqab ya uso iliyotolewa mwaka wa 2018 ili pia kujumuisha taasisi za elimu.

Ikiwa bado kuna shaka yoyote kuhusu shambulizi la kisiasa dhidi ya vyumba vya ibada kuwa linalenga nini, Waziri wa zamani wa Uoanishaji, Kaare Dybvad Bek, alifafanua hilo katika taarifa yake kwa Shirika la Utangazaji la Denmark (DR) baada ya kufungwa kwa chumba katika Chuo Kikuu cha Kusini mwa Denmark, aliposema kwamba vyumba vya ibada “vinaunda nafasi kwa utamaduni wa kizamani ambao hauna uhusiano wowote na jinsi jamii ya Denmark inavyofanya kazi leo.”

Katika kivuli cha kauli hizo za kukera zilizotolewa kutoka ngazi za juu za kisiasa nchini, na “mazungumzo” yaliyofuata na taasisi za serikali, idara za vyuo vikuu huko Odense na Copenhagen zilijikuta zikilazimika kukanyaga utu wao wenyewe, pamoja na maadili ya ujumuishi na uanuwai wanaodai kushikamana nayo, na kugeuka kuwa vyombo vya ziada vya kiutendaji vya serikali katika vita vyake vya kimsalaba vya kisiasa dhidi ya kitambulisho na maadili ya Kiislamu.

Enyi Waislamu: Kufungwa kwa vyumba vya ibada katika vyuo vikuu si jambo la bahati mbaya wala si jambo la kiidara pekee. Badala yake, ni sehemu ya njia ya kisiasa inayoegemea kizuizi cha kimfumo cha haki za Waislamu na ni shambulizi dhidi ya Uislamu katika uwanja wa umma. Kwa miaka mingi, maadili na desturi zetu za Kiislamu zimetiliwa shaka, kuonyeshwa kama tatizo, na kufanywa shabaha ya sheria za kibaguzi na hotuba za chuki. Leo, zamu imefika ya swala—moja ya nguzo za Uislamu, ambayo haikubali kulegeza msimamo wowote.

Ni muhimu kusisitiza hapa kwamba suala hili haliwahusu wanafunzi Waislamu pekee, wala haliwakilishi mapambano ambayo wanatarajiwa kukabiliana nayo peke yao.

Kufungwa kwa vyumba vya ibada kunafuata mantiki ile ile ya kisiasa inayosimama nyuma Sheria ya Imam, marufuku ya niqab, mapendekezo ya kupiga marufuku hijab katika shule za msingi, na hatua zengine za kibaguzi zinazoelekezwa dhidi ya Waislamu nchini Denmark.

Ni mkakati ulio wazi kabisa: mipaka yetu inajaribiwa, mapigo yetu yanapimwa, na maputo ya majaribio yanazinduliwa. Ikiwa hatua hizi hazitafikiwa kwa jibu dhahiri na thabiti, zitakuwa za kudumu, na wanasiasa wanasonga mbele kuelekea hatua inayofuata ya kupiga marufuku au kulazimisha. Tunakabiliwa na mkazo wa taratibu na unaozidi kuwa wazi wa uwezo wa Waislamu kuishi kulingana na maadili yao.

Wakati huo huo, utamaduni hasi unaosumbua unajitokeza katika jamii kuelekea utendaji wa Waislamu wa ibada zao—hasa miongoni mwao ni swala—ukweli ambao tayari umekuwa dhahiri, kwa mfano, katika soko la ajira.

Enyi Waislamu: Jibu letu linapaswa kuwaje kwa majaribio ya kiserikali ya kukandamiza kitambulisho chetu cha Kiislamu?

Kama Waislamu, tuna mistari mekundu ambayo lazima ilindwe na haipaswi kukiukwa. Swala ni mojawapo ya mistari hii mekundu, na inapokiukwa, hii inahitaji jibu la wazi, la pamoja, na la umma kulingana na shutma, makabiliano, na kulaani.

Misikiti ya Waislamu, mashirika yao, na sauti zao za umma lazima zitambue kwamba zina jukumu maalum la kuonyesha msimamo mkali na wazi wakati sheria na maadili ya msingi ya maisha ya Kiislamu yanaposhambuliwa. Ikiwa hatutachukua hatua kwa pamoja wakati hata swala inapoanza kuhojiwa na kufanywa kuwa uhalifu, basi ni lini?

Pia ni muhimu kukumbusha kwamba maadili na sheria za Uislamu haziwezi, na hazipaswi, kulindwa kwa kutegemea maadili ya batili ya kisekula kama vile “uhuru wa dini” au kile kinachoitwa maadili ya kiliberali, ambayo kimsingi hayaendani na Uislamu. Lazima pia tukumbuke kwamba majaribio ya kinafiki ya wanasiasa na wengine wenye mamlaka kuzuia kujitolea kwetu kwa Uislamu si kitu ila ni dhihirisho la kufilisika kiakhlaki na kutokuwa na uvumilivu mkubwa kwa Uislamu na Waislamu.

Kwa hivyo, lazima tuendelee kwa mujibu wa Uislamu pekee kama msingi wa kitambulisho chetu, na vile vile kama msingi wa hatua yetu ya kisiasa na ushirikiano na jamii.

Na kwa kizazi cha vijana cha Waislamu haswa, tunawasilisha ujumbe ulio wazi: Shikamaneni imara na Uislamu wenu msafi, na musihisi kamwe kwamba lazima muombe msamaha kwa sehemu yoyote yake. Msilegeze msimamo kitambulisho chenu, bila kujali changamoto munazokabiliana nazo. Lindeni maadili yenu na kujitolea kwenu kwa Uislamu kwa kuimarisha uhusiano wenu na Mwenyezi Mungu (swt), kupitia umoja na mshikamano, na kwa kupinga kila jaribio la kukuvueni Dini yenu.

Wekeni Uislamu juu ya kila kitu, na Mwenyezi Mungu (swt) atakupeni mafanikio na ushindi, katika dunia hii na Akhera:

[هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيداً عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ]

“Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.” [Surat Al-Hajj:78].

H. 16 Jumada II 1447
M. : Jumapili, 07 Disemba 2025

Hizb-ut-Tahrir
Denmark

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu