Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hatimaye Theluji Imeyeyuka na Kudhihirisha Madhambi Makubwa ya Watawala Vibaraka na Makundi Yaliyowasalimisha kwa Maadui

Kwa hiyo Jifunzeni! Sitisheni Kazi zao kwa Kuungana nyuma ya Uongozi wa Kisiasa ulio Makini ambao utarudisha hadhi Yenu, kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu

(Imetafsiriwa)

Alfajiri ya 1/1/2017, Maamuzi ya Baraza la Usalama yalipitishwa: “Kwa pamoja kulipitishwa maamuzi ya makubaliano ya kusitisha vita ndani ya Syria ambayo yalipigwa jeki na Urusi na Uturuki. Maamuzi ya Baraza la Usalama liliomba kufanyike usambazaji wa haraka wa kibinadamu kwa wakaazi wa maeneo yanayohitaji…” (BBC Kiarabu alfajiri ya 1/1/2017). “Maamuzi ambayo ni nambari 2336, yalithibitisha kwamba Baraza la Usalama lilizingatia sana nakala ya Urusi na Uturuki pasina kuitabban na kuweka wazi kwamba inaunga mkono juhudi za Moscow na Ankara za kusitisha vurugu ndani ya Syria na kurudi katika mchakato wa kisiasa ili kusuluhisha mzozo…” (AlJazeera, 23:24 muda wa Makkah, 31/12/2016). Hivyo basi, Baraza la Usalama liliyakubali maamuzi ya makubaliano ya kusitisha vita ndani ya Syria ambayo yalijadiliwa na vibaraka wa Amerika katika mzozo wa Syria: Urusi, Uturuki na Iran na makundi ambayo yalishiriki katika mazungumzo huko Ankara. Kukubaliwa huko na Baraza la Usalama ni natija ya mpango wa usaliti na utelekezaji wa utawala wa Erdogan ambao unabeba madhambi kwa kuyasukuma makundi kujitoa kutoka Aleppo na kujisalimisha kwa utawala wa dhalimu, katika mpango wa kudhilalisha uliopangwa na Erdogan na Putin huko St. Petersburg mnamo Agosti 2016 ambao umepelekea leo kuwa na makubaliano mapya maovu yanayojumuisha sehemu tatu: kusitisha vita, kufuatilia ukiukaji na mazungumzo ndani ya Astana mnamo 23/1/2017 kwa msingi wa taarifa ya Geneva I.

Hatua hizi za usaliti zimepitia ngome tatu mpaka kufikia makubaliano haya yaliyofikiwa: Amerika imeipa Iran jukumu katika hatua ya kwanza na kwa chama chake na wafuasi wake, lakini wakafeli na utawala ukawa unakaribia kuanguka. Hatua ya pili, Amerika ikaipa jukumu muhalifu Urusi ambayo imetumia kila silaha ya ukatili lakini haikufaulu katika kuondosha upinzani uliokuwa umekita. Mwisho ikaingia Uturuki uwanjani, kwa sababu mtawala wake anadhibiti makundi mengi kaskazini. Akafuata njia ovu mpaka mwisho na kuchochea ngome za “ulinzi wa Frati,” na kuwatoa wapiganaji wengi kwa ajili yake kabla kuyaamrisha makundi yaliyobakia na yanayojihusisha naye kujitoa ndani ya Aleppo katika janga ambalo halijawahi kutokea kabla ndani ya nchi ya Waislamu; ikimaanisha kuwalazimisha watu kuhama kutoka katika nyumba zao kwa ajili ya nani? Kwa ajili ya yule aliyenadi miito ya mistari myekundi na mistari myekundu zaidi na kisha Aleppo ikasalimishwa kupitia mchakato wa kashfa na uliofichuka na Erdogan na wandani wake na makundi yake yaliyomuitikia yatabeba madhambi juu ya hilo. Makundi kisha yakajadiliana kuhusu kupoteza nchi yao na kukubaliana na maadui wake sio ndani ya kiza cha usiku bali mchana kweupe na kusahau au kujitia hamnazo ili kusahau damu iliyomwagwa na matukufu yaliyovunjiwa heshima na nyumba zilizovunjwa – watu wake, miti na mawe. Walisahau au walijifanya kusahau uhadaifu wao kwa watu ili kuwakomboa kutoka kwa utawala na vibaraka wake na kutoka katika ukandamizaji na uhalifu wake.

Ni moja katika maafa makubwa ambayo utawala wa Erdogan unayakalia katika meza moja na Putin, katika mpango wa kudhilalisha na uliojaa aibu, kuiuza Aleppo na watu wa Aleppo na yale yatakayokuja baada ya Aleppo na anayatizama kuwa ni ushindi na kumpongeza Putin kwa hilo! Ni moja katika maafa makubwa kwamba Iran inaongeza katika uhalifu wa Urusi na kuboresha maradufu uhayawani na ukatili wake na kushindana na Urusi katika mauaji na hesabu ya vifo!

Ni moja katika maafa makubwa kuikabidhi Aleppo kwa utawala wa dhalimu, kwa mujibu wa maamuzi ya Geneva kwamba yale makundi ambayo yaliuza Dini yao kwa bei rahisi lazima yagawanye usimamizi duni pamoja na vibaraka wa utawala na kufutilia mbali kazi yao ngumu waliyoifanya baada ya kukaribia kuuangamiza utawala! Ni moja katika maafa makubwa ambayo watawala ndani ya nchi za Waislamu wanakimbilia kuyakaribisha mazungumzo hatari na maovu ndani ya Astana na Geneva na kujihusisha na mipango yao badala ya kuwanusuru watu wa Ash-Sham; lakini hili litafanyika vipi ilhali wanafungamano la karibu la ukhaini… Mwenyezi Mungu awaangamize… namna gani wanajitia upotofu!

Enyi watu wa Ash-Sham: Theluji ya Aleppo imeyeyuka; madhambi ya watawala vibaraka na makundi, yamekuwa wazi kwa kila ambaye ana macho, hata kwa waliokuwa na ruwaza lakini walipoteza kuona, hakuna ukungu unaobakia machoni bali kuko wazi kama mchana kwa kila anayeweza kuona… Mulidanganywa na watawala hususan majirani na haswa Erdogan wa Uturuki na hususan yale makundi ambayo yaliikabidhi Aleppo na zaidi ya Aleppo kwa kupokea pesa kutoka kwa wasaliti wajinga… Enyi watu wa Ash-Sham mumeumwa kutokana na makubaliano ya kwanza yaliyotiwa saini na makundi na kutokana na kampeni ya kwanza ya kuhamishwa kwa lazima ambayo inabeba madhambi ndani yake, muliumwa na Erdogan kutokana na mstari mwekundu wa kwanza (ahadi) aliyoivunja na kutoka katika ahadi ya kwanza kwamba Hama haitorudiwa mara mbili, kisha ahadi yake ikapotea. Muumini haumwi kutoka katika tundu moja mara mbili, kwa hiyo inakuwaje kuwa mumeumwa mara kadhaa na watawala jirani na kwengineko? Inakuwaje mumeumwa kutokana na makundi yaliyokuwa yanapigana baina yao mbele ya macho yenu badala ya kupambana na yule waliyekuja kupigana naye na kutoa mwito wa kuungana lakini hawaungani, na wanadai kuwa wanapinga kugawanyika lakini wamegawanyika kwa kina na kwamba wanawachukia watu wenye pesa chafu lakini wanafikiria kuzichukua pesa hizo ni manufaa!

Makundi haya hayataweza kulinda ardhi yoyote mpaka yatakapo tambua maradhi na kuyatibu na tiba, tiba ni umoja wao sio kugawanyika. Lakini umoja sio tu kuzungumza kusikofuatiliwa na vitendo na hili halitowezekana mpaka makundi yaungane nyuma ya uongozi mukhlisina kwa msingi wa Uislamu, kusomwa kwa ayah hii tukufu hakutoshi:

(وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا) “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarakiane.” [Al-i-Imran: 103]. Lakini kuifikiria na kuiwaza ni jambo la dharura:

(أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآن)“Je! Hawaizingatii hii Qurán” [Muhammad: 24]

Kitakacho hakikisha umoja ni kujifunga katika kamba ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa hiyo makundi lazima yawe na uongozi wa kweli wa kisiasa ambao unajifunga na kamba ya Mwenyezi Mungu (swt), kuwaongoza katika mstari ulionyooka, msitari mkubwa wa Uislamu… Hivyo basi, kupelekea kuondosha mgawanyiko na kuzinyoosha safu. Lakini lau wataungana nyuma ya uongozi ambao haumuogopi Mwenyezi Mungu na kuwafuata watawala wasimuogooa Mwenyezi Mungu (swt), maradhi yatabakia na kuzidi na mgawanyiko utabakia na kuenea na kisha hawatomsitisha dhalimu yeyote na hawatomzuia muhalifu yeyote kama tulivyoona ndani ya Aleppo na kwingineko, na watakuwa ngazi zitakazotumiwa na watawala vibaraka ili kuwapa njia ya kupata makubaliano maovu licha ya kwamba wameonyesha umoja wao kama tulivyoona katika makubaliano ya Ankara, umoja wao unamaanisha “kutia saini kwa makundi yaliyoungana”

Mababu zetu wamepitia baadhi ya haya, baada ya kuachana na haki waliyokuwa wameibeba na kupatishwa tabu kama natija yake… Walijitenga na ukweli ulioletwa na Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), wakati wa Vita vya Msalaba, wakaipoteza Al-Quds na sehemu ya Isra’ na Mi’raj ya Mtume (saw) … na wakajitenga na ukweli wakati wa Matartar na kuipoteza Khilafah, Baghdad …na wakagawanyika na kutofautiana katika miaka ya mwanzoni ya karne ya mwisho na Khilafah ikapotezwa na Al-Quds ikapotezwa tena... Lakini wakati wa mwanzo na wa pili walifahamu maradhi na kuchukua tiba na kurudi tena kuwa taifa kubwa na kuifungua Konstantinia na kuwa mji wa Uislamu na wakalikaribia eneo la dhalimu Putin na kubisha milango ya Ulaya, mashariki na magharibi, kuanzia Vita vya Matoure katika milango ya Ufaransa hadi kwenye milango ya Vienna … Ni jambo linalowezekana kurudi kuwa na nguvu na ushindi kwa kutumia tiba sawia na kuwafurusha wakoloni Makafiri na wafuasi wao kutoka ndani ya Syria na ardhi nyingine za Uislamu na kuipata tena Al-Quds na kuliondosha umbile la Kiyahudi la kiuvamizi ndani ya Ardhi ya Baraka na kueneza kheri na sio tu katika ardhi za Uislamu bali pia katika maeneo mengine na kuweza kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kutawala na kupanuka.

Enyi Waislamu, Enyi watu wetu wa Ash-Sham, na kwa wanamapinduzi wote: Tunawapa tiba hii na tunawahutubia nayo, hakuna kupuuza au mbadala uliobakia, tumezidiwa na majanga kila upande, kwani hatujifunzi somo?!

أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَيَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿ “Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki?” [At-Tawba: 126]

Tunawahutubia kibinafsi na kwa makundi, na watu wenye nguvu na ulinzi wa majeshi na makundi …Tunawahutubia nyinyi na kuwalingania kwamba muungane nyuma ya uongozi wa kisiasa ulio na ikhlass, ili kuunusuru na kuupa nguvu kwa kusimamisha hukmu ya Uislamu, dola ya Kiislamu, Khilafah ya uongofu … Huu ndio ukweli tunaowalingania kutoka kwa chama ambacho hakiwawadanganyi watu wake, Hizb ut Tahrir ambacho mnakijua, kinafanyakazi nanyi na miongoni nanyi, mumeuona ukweli wake juu yenu na kinawashauri… Hizb ut Tahrir kinawalingania, majanga juu yetu yamezidi na sintofahamu kukithiri. Tunaweza kuuzima moto huu ili mambo yawe shuari na amani na kusitisha sintofahamu na usalama wetu ukarudi tena…

Kwa hiyo tunyosheeni mikono mikono yenu yenye nusra kwani tayari yetu tushainyoosha, tunaweza kupeana nguvu na kushinda katika pande zote na huo ndio ushindi mkubwa …

إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ﴿ “Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia” [Qaf: 37]

H. 3 Rabi' II 1438
M. : Jumapili, 01 Januari 2017

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu