Jumatano, 09 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Makongamano Yenye Malengo ya Kufuta Kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa Yanafanyika Wakati Damu ya Watu wake Ikimalizwa
(Imetafsiriwa)

Milipuko ya mabomu inateketeza miili ya watoto mjini Gaza, njaa inatafuna mabaki yao, mizinga inasaga saga uhai na nyumba za watu walio na msimamo thabiti, na ndege zinanyesheza lava zao kwenye hospitali na hema za waliohamishwa. Kutokana na hali ya uhalifu huu, kongamano lililokongamana jana usiku, 22 Septemba 2025, jijini New York, lililoitishwa na Ufaransa na Saudi Arabia, lilitaka kutambuliwa kwa “Dola ya Palestina”.

Hakika kongamano hilo lilifanywa ili kujadili kutambuliwa kwa dola ya Palestina huku damu yetu ikitiririka kwa wingi na mauaji ya kinyama ni makali zaidi. Ni kongamano lililoitishwa na nchi ambazo zinashuhudia mauaji, njaa, watoto kuchomwa moto, na mauaji ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili, bila ya kuisaidia Gaza na watu wake, hata kwa tama la maji. Je, kuitishwa kwa kongamano hilo ni wito wa mwamko baada ya muda wa kutotilia maanani? Au je, kuitishwa kwake katikati ya mauaji ya halaiki ya watu wa Palestina ndio dhurufu sahihi zaidi ya kufuta kadhia yao na kumwaga damu yao?

Kongamano hili ni kama dazeni za utambuzi, makongamano na maazimio kabla yake, ambayo hayakuzuia uhalifu na uvamizi wa Mayahudi. Utambuzi wa sasa ni kama vile Rais wa Ufaransa alivyosema kwamba kutambuliwa kwa dola ya Palestina kunafungua njia ya mazungumzo yenye manufaa kati ya Wapalestina na ‘Waisraeli’. Kila mtu anajua nini maana ya mazungumzo na Mayahudi, lakini hilo, yaani, kongamano hilo, limebeba ndani yake sumu hatari, hata kama linachukua ukandamizaji wa watu wa Palestina kama kifuniko na anwani yake, na kuvaa guo la kutetea haki zao. Suala la kuitambua dola ya Palestina si lolote bali ni lango la kufilisi kadhia ya Palestina jambo ambalo limethibitishwa na maneno ya kongamano hilo lililotajwa hapo juu.

Hii ni pale lilipolifanya umbile hilo, usalama wake, na kuendelea kuwepo kwake kuwa msingi wa suluhisho, na lilipoyafanya mapambano ya watu wa Palestina kuwa aina ya ugaidi wa kulaaniwa. Hii ilikuwa ni kuunda ile inayodaiwa kuwa kijidola cha mgeni, kilichonyang'anywa kila kitu, kilichoundwa na jicho ovu la Magharibi, bila ardhi, silaha, rasilimali, usalama, au hadhi. Kiliundwa kulingana na saizi ya umbile nyakuzi ili kuihifadhi na kudumisha uwepo wake, na ilitumika kama kifaa cha bei rahisi kwake. Ilipaswa kuwa bei ndogo ya kuzika na kuachana na kadhia ya Palestina, na daraja ambalo kwalo treni ya uhalalishaji mahusiano inaweza kupita.

Taarifa ya mwisho ya kongamano hilo pia imebeba wito muovu wa ukaliwaji kimabavu wa Palestina kwa kuleta misheni ya kimataifa iliochochewa na mradi wa mratibu wa Marekani na polisi wa Ulaya ili kuusimamia Ukanda wa Gaza!

Ama Marekani inataka tu iwe dola isiyo na jeshi (inayojitawala) katika sehemu ya sehemu ya Palestina yenye udhibiti wa umbile la Kiyahudi juu yake!! Bila kujali hamu ya “Mamlaka ya Palestina na watawala vibaraka” kuiita dola ya Palestina, hiyo haibadilishi chochote kuhusu uhalisia wake. Amerika haitaki iwe dola huru hata juu ya sehemu ya sehemu ya Palestina. Badala yake, zaidi ni kama utawala wa kivyake usio na silaha, isipokuwa kwa kile ambacho ni muhimu kwa polisi wa ndani kama chombo cha kukandamiza watu wa Palestina, na chini ya udhibiti wa Kiyahudi.

Ni moja ya kinaya za enzi hizi kwamba dola za kikoloni kama vile Ufaransa na Uingereza, ambazo zilianzisha umbile hilo la kuchukiza karibu miaka themanini iliyopita, ndizo zinazotaka suluhisho la dola mbili, kwa sababu tu zina nia ya kulimakinisha, na kwamba mwangwi wa sauti zao ni watawala wasaliti ambao hapo awali waliisalimisha Palestina mwaka 1948 na 1967, na kuiachia umbile hilo kama tonge rahisi lililoloweshwa ndani ya damu ya watu wake. Leo wanakuja, baada ya utambuzi wao wa umbile hilo halifu kufanyika pasi na kujali, kudai makombo katika sura ya dola ya Palestina, na kuwasilisha jambo, kwa sherehe, kama ushindi na faida!

Enyi Ummah wetu, umma bora uliloletwa kwa ajili ya wanadamu: Msikiti wa Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarkiwa hazitakombolewa na watawala wa Jordan, Misri, Hijaz, Uturuki, au Pakistan. Watawala hawa wamezoea uhaini. Iwapo wanafikiri wataizika kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa chini ya kile kinachoitwa “suluhisho la dola mbili,” wajidanganya. Palestina imekuwa johari ya Uislamu tangu Mwenyezi Mungu (swt) alipoinasibisha na Nyumba Yake Tukufu kwa fungamano moja, pale Alipomchukua Mtume Wake (saw) katika Safari ya Usiku kutoka Msikiti Mtakatifu hadi Msikiti wa Al-Aqsa.

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ]

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka [Al-Isra: 1]

Kwa hiyo, kamwe haitakubali kugawanywa, kwa sababu itikadi ya Kiislamu inakataa kwa wafuasi wake kuiacha. Ama masuluhisho ambayo ukoloni unatafuta kulazimisha, na masharti ambayo unataka kuweka, na watawala wasaliti wanayakuuza, hatima yao ni kutoweka, na hatima ya umbile la Kiyahudi ni kusagwa sagwa, ili Palestina irudi takatifu na safi kwenye ardhi za Uislamu. Funzo la Makruseda haliko mbali.

[فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]

Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa. [Al-Isra: 7]

Enyi Waislamu:

Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu (swt), watu wa Ardhi Iliyobarikiwa hawatadhurika na wale waliowaangusha. Wana miadi ya ushindi mtukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Al-Qawi Al-Aziz. Ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa unategemea ukombozi wa Umma wa Kiislamu kutokana na tawala za vibaraka ambazo zimeukandamiza. Waislamu wataendelea kubaki katika hali mbaya isipokuwa wakukute vumbi la udhalilifu, wapambane na madhalimu, na kuwahutubia watoto wao wa kiume na kaka zao ndani ya vikosi vya vikosi na majeshi ili kuchukua hatua mara moja kusimamisha Khilafah Rashida, ambayo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume Wake (saw). Huu ni ulinganizi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenu, na ndio ambao Hizb ut Tahrir inakulinganieni kwake. Basi mnusuruni Mwenyezi Mungu, naye atakunusuruni na ataifanya imara miguu yenu.

Yeyote anayefikiri kwamba usalama upo katika kukaa kimya kuhusu uhaini amekosea. Tawala hizi za kihalifu zitaendelea kututia katika aina mbalimbali za udhalilifu, na zitawavisha watoto wetu vazi la hofu, njaa na mateso. Hakuna wokovu kwa Waislamu duniani wala Akhera isipokuwa wafanye kazi usiku na mchana kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu duniani na kuangusha tawala za kihalifu. Mwenye kuchelewesha kheri hii hana wa kumlaumu ila nafsi yake atakaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) bila ya udhuru. Inatosha kwenu katika suala hili yale aliyosimulia Muslim kutoka kwa Abu Dharr, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume (saw) katika yale aliyoyahadithia kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwamba amesema:

«يَا عِبَادِي إِنَّمَا هِيَ أَعْمَالُكُمْ أُحْصِيهَا لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إِيَّاهَا، فَمَنْ وَجَدَ خَيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، وَمَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذَلِكَ ‌فَلَا ‌يَلُومَنَّ ‌إِلَّا ‌نَفْسَهُ»

“Enyi waja wangu, hakika sikuhisabuni ila kwa vitendo vyenu, kisha nitakulipeni, basi mwenye kupata kheri basi amshukuru Mwenyezi Mungu, na mwenye kupata jengine kando la hiyo, asimlaumu yeyote ila nafsi yake”.

Ewe Mwenyezi Mungu, tufikishie kheri hii kutoka kwetu, na uzifungue nyoyo za Waislamu kwa hayo na kwayo, na utujaalie kutoka Kwako mamlaka yenye kunusuru. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

H. 1 Rabi' II 1447
M. : Jumanne, 23 Septemba 2025

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu