"Uvumilivu" wa Watawala wa Ghuba Unajumuisha Vipengee na Sheria zote Isipokuwa Uislamu na Waislamu!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Chini ya kichwa cha urongo cha "Uvumilivu", watawala wa Imarati walizindua hekalu jipya la moja ya dini za kikafiri katika eneo la Jebel Ali. Hapo awali walitotora hisia za Waislamu walipofungua makanisa kadhaa kwa ajili ya Wakristo, na pia sinagogi la Mayahudi. Yalikuwa yameundwa na wizara iitwayo Wizara ya Uvumilivu mnamo 2016 ili kupigia upatu ufunguzi wa mahekalu ya ziada ya makafiri chini ya kichwa cha “Uvumilivu.”



