Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 27 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: H 1446 / 126 |
M. Jumatatu, 23 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Hindutva ya India Inaendelea Kutumia Shirika la Kitaifa la Uchunguzi kwa Kazi yake Chafu
Kwa mara nyingine tena kukizushia uongo chama cha kimfumo cha Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 14 Juni 2025, Shirika la Kitaifa la Uchunguzi (NIA) lilifanya uvamizi ulioratibiwa katika maeneo matatu huko Bhopal, Madhya Pradesh, na miwili huko Jhalawar, Rajasthan, kuhusiana na kesi ya Hizb ut Tahrir (HuT). Operesheni hiyo ililenga kukusanya ushahidi zaidi dhidi ya HuT. NIA ilidai kuwa uvamizi huu ulisababisha kukamatwa kwa "vifaa vya kidijitali na nyenzo za hatia" (vitabu na vifaa vya kuandikia tunavyodhania). Kabla ya uvamizi huu, Jharkhand (jimbo) ATS ilikuwa imewaweka kizuizini watu wawili kuhusiana na kesi ya Hizb ut Tahrir. Serikali ya India ilipiga marufuku kinyume cha sheria Hizb ut Tahrir mnamo tarehe 10 Oktoba 2024, ikitaja juhudi zake za kusimamisha "Khilafah" ya kimataifa kupitia ugaidi na itikadi kali.
Kama tulivyosema hapo awali, maafisa wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa India wameshindwa kuthibitisha tuhuma za "ugaidi" dhidi ya Hizb ut Tahrir na wanachama wake.
Serikali za India mtawalia, ukiwemo utawala wa sasa, zimelenga kwa kiserikali jumuiya za Kiislamu, Kikabila na Dalit (matabaka duni yasiyobahatika) kupitia sera za kibaguzi na sheria za kikatili. Sheria ya Uhaini, Sheria ya (Kuzuia) Shughuli zilizo Kinyume cha Sheria (UAPA), Sheria ya Usalama wa Taifa (NSA), na Sheria ya Majeshi (Mamlaka Maalum) (AFSPA) zimetumiwa kama silaha kukandamiza upinzani na kuwatisha makabila ya Waislamu na Madalit. Hatua hizi zinaimarisha hali ya hofu, na kuwadunisha Waislamu kuwa raia wa daraja la pili. Utawala wa sasa umezidisha ajenda hii, ukidhoofisha haki za kikatiba huku ukiitisha uthibitisho wa utiifu usio na uwiano. Licha ya ukandamizaji wa serikali, Waislamu wa India wanasalia kuwa wastahamilivu, wakipata nguvu kutoka kwa Aqida yao na urithi wao wa kihistoria, wakikataa kujisalimisha kwa simulizi za utaifa zenye kugawanya.
Utafiti wa hivi majuzi wa PUCL unaonyesha mienendo ya kutisha katika utumiaji wa Sheria ya (Uzuiaji) Shughuli Haramu ya India (UAPA), huku kukiwa na watu 8,371 waliokamatwa kati ya 2015-2020, lakini ni watu 235 pekee waliopatikana na hatia—asilimia 2.8 ya hatia. Cha kushangaza, 97.2% ya washtakiwa walikabiliwa na kifungo cha muda mrefu kabla ya kuachiliwa huru. Aliyekuwa Jaji Mkuu wa India D.Y. Chandrachud alionya dhidi ya kutumia sheria za kupambana na ugaidi ili kukandamiza upinzani, lakini serikali mtaliwalia zinaendelea kuwalenga Waislamu, na kuendeleza hali ya hofu na kufungwa. Kesi za hivi majuzi zinaonyesha mtindo unaorudiwa wa vitisho vya serikali dhidi ya Waislamu wa India kupitia sheria kali kama vile UAPA. Waislamu wengi wameteseka gerezani kwa miongo kadhaa kabla ya kuachiliwa huru, na baada ya maisha yao kuharibiwa vibaya. Kesi ya Tamil Nadu HuT inadhihirisha hili: licha ya madai mazito, karatasi ya mashtaka ilishindwa kuwasilisha ushahidi wa kuaminika ili kuthibitisha madai yao. Vitendo kama hivyo vinaonyesha matumizi mabaya ya serikali ya sheria za kupambana na ugaidi ili kulenga wachache, kukandamiza uhuru wa kuzungumza na kudumisha hali ya hofu.
Utawala wa India wa Hindutva (unaoungwa mkono na RSS) unaendelea kupurukusha umakini kutoka kwa kufeli kukubwa kwa utawala kwa kuzingatia kupita kiasi katika kulenga mashirika ya Kiislamu na watu binafsi kupitia sheria mpya kama Sheria ya Marekebisho ya WAQF, (kupiga marufuku) Sheria ya Talaq Tatu na nyenginezo. Taifa hili linakabiliwa na migogoro ya dharura zaidi: mfumo wa mahakama unaoporomoka chini ya kesi milioni 49 zinazosubiri, viashiria vya kiuchumi vinaonyesha tofauti za kutisha, na mapato ya kila mtu yakidorora hadi $2,880 (ikiorodheshwa ya 119 ulimwenguni) huku 1% ya matajiri zaidi ikidhibiti 58% ya mali ya kitaifa, kiwango cha ukosefu wa ajira cha 7.6% ikiwaacha mamilioni katika hali mbaya ya kiafya na mwisho mfumo fisadi na mbovu wa afya wa serikali ambao umesababisha vifo kutokana na uzembe mara nyingi hasa wa watoto wachanga.
Sambamba na hilo, unyanyasaji wa serikali dhidi ya jamii zilizotengwa katika (Manipur, Gujarat, Uttar Pradesh, MP, Uttarakhand) unaendelea bila kusitishwa kupitia ubomoaji usio halali wa nyumba, mauaji ya kiholela na mateso ya kizuizini- masuala ya kiserikali ambayo yanahitaji uangalizi wa haraka. Vipaumbele vya sasa vya serikali vinaakisi ukosefu hatari wa uwiano na mahitaji halisi ya taifa.
Tunasisitiza tena tunatumai kuwa Serikali ya India na NIA zitatumia akili na kutambua upumbavu wao wakati huu na kusahihisha mtazamo wao kuelekea HuT.
1. Hizb ut Tahrir (HT) ni shirika la kimfumo la kisiasa la Kiislamu linalofanya kazi katika nchi 50+, likiwa na rekodi ya kimataifa ya harakati ya amani inayotokana na mfumo wa Kiislamu.
2. Kutambuliwa na watetezi wa haki za binadamu kama vuguvugu lililojitolea kwa mapambano ya kifikra na kisiasa.
3. HT inaendelea na kazi yake miongoni mwa Umma wa Kiislamu—bila kuzuiwa na mifumo ya kisiasa, iwe demokrasia, udikteta, au falme duniani kote bila kujihusisha na shughuli zozote za kigaidi.
4. Misheni ya shirika hili —kusimamisha Khilafah katika Ulimwengu wa Kiislamu—inabaki bila kukatishwa tamaa licha ya upinzani wa serikali, ikipata nguvu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na azma isiyoyumba ya Waislamu duniani kote. Iko katika rekodi katika maandishi mengi ya M.K. Gandhi kwamba yeye pia aliunga mkono wito huu huu wakati wa mapambano yake ya Uhuru kutoka 1919-1922.
5. Njia ya Hizb ut Tahrir inaakisi Seerah (maisha/njia) ya Mtume (saw), ikisisitiza mazungumzo, mijadala ya kifikra, na uwazi wa kimfumo.
6. Fasihi yake ya kina—inapatikana mtandaoni, machapisho, na kwenye majukwaa kama Amazon.com—inakaribisha uchunguzi, ikithibitisha kujitolea kwake kwa mjadala wa uwazi na wa kikanuni. Kwa kuuwasilisha Uislamu kama badali kamili ya "Udhalimu wa Kibepari", Hizb ut Tahrir inawapa watu uwezo wa kuchagua njia yao-- kukataa kulazimishwa kwa kupendelea ushawishi wa akili.
7. Kama ilivyokuwa katika miongo iliyopita na mwaka huu pia Hizb ut Tahrir Iliendesha makongamano yake ya kila mwaka ya Khilafah duniani kote ikiwemo kongamano la kila mwaka la HuT nchini Marekani mnamo mwezi Aprili 2025 bila kuingiliwa, usumbufu au kukamatwa. Kwa nini NIA na Serikali ya India hawaoni hili, wakati katika kila jambo wao hutafuta maelekezo kutoka Marekani.
Sasa tunauliza raia wasomi wa ulimwengu - ni shirika gani la kigaidi linalouza vitabu vyake kwenye tovuti kuu za mtandaoni na kufanya makongamano ya wazi kwa miongo kadhaa? Hizb ut Tahrir, kama moja ya vyama vikubwa vya Kiislamu, inasimama kidete dhidi ya vitisho, ikijumuisha matarajio jumla ya Ummah kwa Khilafah.
Tunauhutubia Umma wa Kiislamu kwa jumla na Maulamaa hasa kwamba Hizb ut Tahrir inafanya kazi kwa ikhlasi kama mbebaji mwenge kwa ajili ya mwamko wa Waislamu duniani na inabakia kushikamana na njia yake ya Utume tangu ilipoanzishwa mwaka 1953 na Mwanachuoni, Hakimu na Mwanafikra - Sheikh Taqiuddeen Al-Nabhani Al Azhari (Mwenyezi Mungu amrehemu) kutoka ardhi iliyobarikiwa ya Palestina.
Mwisho, tunawakumbusha tena Waislamu wa India kuhusu baba zao waliotangulia ambao hawakuwa na uoga kama Sheikh Syed Ahmed Shaheed, Shah Waliullah Muhadith Dehlawi, Sheikh Ahmed Sirhindi na Sheikh-ul-Hind Mahmud ul Hasan Deobandi (Mwenyezi Mungu awarehemu wote) jinsi walivyopambana na maisha yao kurudisha utukufu wa Umoja wa Kiislamu na kuuacha ulimwengu wakijaribu. Simameni Enyi Waislamu na munusuru kazi ya kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili msiogope yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt).
Kwani Mwenyezi Mungu Al-Qawi asema:
﴿يُرِيدُونَ لِيُطْفِؤُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴾
“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Surah Saff: 8 – 9]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |