Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 13 Safar 1447 | Na: H 1447 / 007 |
M. Alhamisi, 07 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Je, bado mna matumaini kwa Watawala wenu Ruwaibidha?!
(Imetafsiriwa)
Umbile la Kiyahudi bado linatekeleza uhalifu wake dhidi ya watu wa Gaza, hivyo makumi ya mashahidi huongezeka kutokana nao kila siku. Pia bado linapiga mzingiro wake juu ya Gaza, hivyo watu wake wanakufa kwa njaa, kwa kuwa hawana chakula, vinywaji, dawa, au makao, licha ya jitihada fulani za kupeleka misaada kwao kwa uoga! Lakini mamia ya maelfu hawapati tonge ambalo kwalo wanaweza kuzuia njaa zao au kunyamazisha njaa ya watoto wao, kwa hiyo wamekuwa wanakufa kwa njaa mbele yao na mbele ya macho ya ulimwengu wote bila msaidizi au mwenye kuwanusuru.
Tumeshuhudia watu wengi wa dunia wakihamasika, wakitaka kukomesha vita vya Gaza na kuondolewa kwa mzingiro kutoka kwa watu wake, na kuwapa chakula na vinywaji. Hili halikuzaa chochote isipokuwa fedheha zaidi kwa serikali zao, kwa hiyo baadhi yao walidai, kwa uoga, kuondolewa kwa mzingiro kutoka kwa watu wa Gaza, kwa hilo kufanana na binadamu yeyote wa kawaida asiyejiweza, kana kwamba wao si wenye uamuzi wa kisiasa!
Ama kuhusu ardhi za Waislamu, zinazungumzia hali zao na hakuna ubaya, hasa ardhi zilizo jirani ya Palestina, kwa kuwa watawala wao wasaliti wa ruwaibidha (wajinga na watepetevu) wanazuia chochote kuingia Gaza, licha ya kutamani kwa watu wa ardhi hizo jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuwasaidia kaka zao na dada zao mjini Gaza.
Ama kuhusu majeshi ya ardhi hizo, badala ya kutekeleza wajibu wao wa Sharia katika kupambana na umbile la Kiyahudi na kuwaondolea mateso watu wa Gaza, baadhi yao husimama kwenye mipaka ili kuwazuia Waislamu wasivuke na kuwasaidia watu wa Gaza! Kana kwamba wanasubiri amri kutoka kwa watawala hao ruwaibidha ambao wamejitwika ulinzi wa umbile la Kiyahudi!
Na swali ambalo daima linajitokeza, mbele ya mateso ya watu wa Gaza: Ni je, Waislamu au majeshi yao bado wana matumaini yoyote kwa watawala hao ruwaibidha?! Je, wanangoja ndani yao kuchochewa ushujaa wa al-Mu‘tasim?! Jibu liko katika kauli yake (swt):
[إِنَّ اللهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ]
“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Ar-Ra’d:11].
Na msingi katika kubadilisha yaliyomo ndani ya nafsi ni mifumo inayotekelezwa juu yao, ambayo ni mifumo ya khiyana inayokengeuka kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu, na kukata baina yao mafungamano ya udugu wa Kiislamu, na kuchochea ndani yao hisia za utaifa ambazo Mwenyezi Mungu Ameharamisha, na kuyafanya yale yanayotokea mjini Gaza ya mauaji, uharibifu, kuzingirwa na njaa kana kwamba hayatokei katika ardhi za Waislamu; na kana kwamba hayatokei kwa kaka na dada zao Waislamu!
Enyi Waislamu, na Enyi Majeshi katika Ardhi za Kiislamu:
Wakati umefika wa nyinyi kutatua suala lenu na kuchukua uamuzi wenu wenyewe kutoka kwa watawala wa ruwaibidha ambao kafiri mkoloni amewaweka juu ya shingo zenu, kwani wao hawazingatii juu yenu udugu wala ahadi, wala hawajali kuchunga mambo yenu, wala kuhifadhi maslahi yenu, wala kuwanusuru nyinyi na kuwanusuru ndugu zenu na dada zenu mjini Gaza. Na imekuwa ni faradhi juu yenu kuwaondoa, na kumpa bay’ah Khalifa anayekutawalani kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw), na anayeyapeleka majeshi kuwanusuru Waislamu, na kurudisha izza na heshima yenu kwenu. Na hakuna mbele yenu isipokuwa Hizb ut Tahrir, chama waanzilishi ambacho hakiwadanganyi watu wake, mmiliki wa mradi wenu wa mwamko kwa msingi wa Uislamu. Basi mnusuruni Mwenyezi Mungu, Yeye atakunusuruni na ataiweka imara miguu yenu.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |