Jumatano, 09 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  30 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 012
M.  Jumatatu, 22 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kutambuliwa kwa Dola ya Palestina
Kutambuliwa kwa Mayahudi Kunyakua 78% ya Palestina!
(Imetafsiriwa)

Uingereza, Canada, Australia na Ureno zililitambua ile inayoitwa “Dola ya Palestina,” na kufuatiwa na nchi kadhaa katika mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika kuanzia Septemba 22-30, 2025, na ulioongozwa na Ufaransa na Saudi Arabia. Utambuzi huu ulikaribishwa na watawala Ruwaibidha (wajinga wasio na maana) wa Waislamu, pamoja na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Waarabu. Jambo la kushangaza ni kwamba, ilikaribishwa pia na mashirika ya Kipalestina, ambayo yanaona kuwa ni matunda ya uthabiti wao, kana kwamba Palestina imekombolewa na na umbile la Kiyahudi kung'olewa!

Enyi Waislamu: Moja ya mahitaji muhimu ya ufahamu wa kisiasa ni kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa msingi wakati wa kuhukumu mambo na vitendo. Haijuzu kwa Muislamu kutoa hukumu juu ya jambo au kitendo ambacho kiko mbali na itikadi ya Kiislamu. Kanuni ya msingi ni kuwa Muislamu asisahau kuwa suluhisho la dola mbili maana yake ni utambuzi wa umbile la Kiyahudi na kwamba lina haki kwa ardhi iliyobarikiwa, na jambo hilo limeharamishwa katika Shariah, kwani ni ardhi ambayo maswahaba watukufu waliinywesha kwa damu yao safi, pamoja na mujahidina waliowafuata kwa uadilifu. Ina msikiti wa tatu kati ya misikiti miwili mitakatifu, ambayo Waislamu husafiri kutoka sehemu zote za dunia kuiendea, na ni mahali pa Safari ya Usiku ya Mtume (saw). Palestina ni ardhi ya Kiislamu, na haijuzu kwa Muislamu kuiacha hata shubiri moja.

Enyi Waislamu: Je, mnatarajia mkuu wa ukafiri, Uingereza, na nchi nyingine za makafiri - zilizoitambua ile inayoitwa Dola ya Palestina - kutuma majeshi kuikomboa Palestina?! Uingereza ndiyo iliyoivunja Khilafah, ikatoa Azimio la Balfour, ikaweka Palestina chini ya Mamlaka, ikawezesha uhamiaji wa Mayahudi kutoka nchi mbalimbali za dunia kwenda humo, ikaweka dola kwa ajili ya Mayahudi huko, ikagawanya ardhi za Waislamu na kupandikiza watawala vibaraka juu yao ambao kazi yao kuu ilikuwa ni kulinda na kumakinisha umbile la Kiyahudi, na nyengine ni kudumisha kugawanyika kwa ardhi za Waislamu. Ama nchi zengine za kikafiri zilizoitambua Dola ya Palestina, zinalitambua umbile la Kiyahudi kwa 78% juu ya yake, ikiwemo kuisambazia mahitaji na mashini ya kijeshi ambayo kwayo inawauwa Waislamu huko Gaza, Ukingo wa Magharibi na kwengineko.

Je, mnatarajia umbile la Kiyahudi litakupeni fadhila kwa kuruhusu kuanzishwa kwa dola ya Palestina kwenye sehemu ya ardhi ya Palestina? Je, hamjui kwamba suluhisho la dola mbili, likipatikana, litakuwa ni kijidola dhaifu, kisicho na nguvu za kijeshi sawa na Mamlaka ya Palestina iliyopo hivi leo, ambayo si chochote zaidi ya kitengo cha usalama cha umbile la Kiyahudi, au eneo tu linalojitawala kwa maelekezo ya dola zilizotajwa na Biden? Na kwamba nchi kadhaa duniani hazina majeshi binafsi. Je, mutakubali kwamba matokeo ya mihanga yenu na uthabiti wenu yawe ni mamlaka ya uchungaji chini ya mishale ya Mayahudi?!

Kejeli hii inatukumbusha kejeli ya tamko la Yasser Arafat la kuanzishwa kwa Dola ya Palestina mnamo tarehe 15 Novemba 1988, nchini Algeria. Ilikuwa dola kwenye karatasi, lakini matunda ghafi ya mazungumzo ya Oslo yalikuwa mamlaka ndogo chini ya mishale ya Mayahudi.

Enyi Waislamu: Msisahau tunachowakumbusheni kila mara: suluhisho pekee sahihi na halali kwa kadhia ya Palestina ni kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu ili kuikomboa Palestina yote na kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka uwepo.

Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, mbebaji wa mradi mtukufu wa Khilafah, inakuombeni mufanye kazi nayo na inatoa wito kwa majeshi ya Waislamu yainusuru katika kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Ndani yake imo izza yenu na ndani yake liko suluhisho la matatizo yenu yote.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu