Jumatatu, 28 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  24 Rabi' II 1447 Na: H 1447 / 019
M.  Alhamisi, 16 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chahitimisha Kampeni yake ya Kimataifa: “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”

(Imetafsiriwa)

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimeendesha kampeni ya kimataifa ya kuinua ufahamu wa kimataifa na kuleta muanga wa kimataifa kuhusu mgogoro wa kutisha wa kibinadamu uliosababishwa na mzozo nchini Sudan ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mitatu na nusu sasa. Mzozo huu usio na maana, kati ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF) vinavyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (“Hemedti”), umesifiwa kama “Vita Vilivyosahaulika” kutokana na kutopokea uangaziaji wa vyombo vya habari na uangalizi wa kimataifa unaostahili.

Kampeni hiyo iliyopewa kichwa cha “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu” ilishughulikia mada zifuatazo:

1. Mgogoro wa kibinaadamu uliosababishwa na mzozo ambao umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, na umesababisha janga kubwa zaidi la kuhama makaazi na njaa duniani, huku njaa ikitumika kama silaha ya vita na pande mbalimbali, pamoja na utekaji nyara, mateso, unyanyasaji wa kijinsia unaoripotiwa kuenea;

2. Historia ya jinsi Uislamu ulivyoingia Sudan kwa njia ya uenezaji wa amani na kuunda maisha ya kisiasa, kimahakama, kiutawala na kiuchumi ya nchi hiyo, na kuwatengenezea watu wake maisha yenye mafanikio, kwa mfano chini ya Usultani wa Funj;

3. Umuhimu mkubwa wa siasa za kijiografia wa Sudan, kama vile eneo lake la kimkakati linalopakana na Bahari Nyekundu – njia muhimu ya biashara ya baharini duniani kote, pamoja na ardhi yake ya kilimo yenye rutuba na maliasili – ikiwemo mafuta, gesi asilia, dhahabu na urani. Haya yote yameifanya kuwa tunu kwa dola za kimataifa na kikanda ambazo zimeshindana kwa ajili ya kutawala na kudhibiti nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono makundi mbalimbali ndani ya vita – vilivyopita na vya sasa;

4. Jinsi dola za Magharibi za kikoloni, kama vile Uingereza, Ufaransa na Amerika, zilivyoweka kihistoria msingi wa mizozo nchini Sudan kupitia sera yao ya kikoloni ya ‘gawanya utawale’ ambayo ilikuza mivutano na migawanyiko kati ya jumuiya mbalimbali za kikabila, na kidini – yote hayo ili kulinda maslahi na ushawishi wao nchini humo. Uingiliaji huu wa kisiasa wa nje ulisababisha Sudan kuwa katika hali ya mizozo ya kudumu tangu wakati wa uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Uingereza hadi leo;

5. Maisha yalivyokuwa chini ya udikteta wa Omar al-Bashir – ugaidi, ukandamizaji wa kikatili, matatizo makubwa ya kiuchumi na vita vya wenyewe kwa wenyewe yalivyokabiliana nayo chini ya utawala wake pamoja na ghiliba zake za Shariah ili kuhalalisha unyanyasaji wake kwa wale wanaopinga utawala wake. Na jinsi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo (“Hemedti”) walivyokuwa wasaidizi wake na ni mabaki ya utawala wake;

6. Siasa za mizozo ya zamani ya Sudan kama vile Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Kaskazini-Kusini na mzozo wa Darfur na jinsi zilivyokuwa matokeo ya utawala wa kikoloni wa Uingereza, uingiliaji wa Marekani ndani ya ardhi hiyo, na utawala wa Omar al-Bashir – ambayo yote yalichochea migawanyiko kati ya watu kwa manufaa ya kisiasa;

7. Siasa za mzozo wa sasa wa Sudan ambao kwa kweli ni mzozo wa madaraka kati ya vibaraka wa Amerika (al-Burhan na Hemedti) na Uingereza (Forces for Freedom & Change) kwa ajili ya kutawala nchini Sudan kufuatia kuondolewa madarakani kwa Omar al-Bashir mwaka wa 2019. Mapigano hayo pia yamechochewa na dola mbalimbali za kikanda kama vile Imarati, Saudi Arabia, Urusi na China ambayo inaunga mkono upande mmoja dhidi ya mwengine kwa  ajili ya utajiri wa ardhi wa nchi hiyo na umuhimu wa kimkakati;

8. Jinsi Khilafah pekee inayoweza kuleta izza kwa Sudan. Hoja hii ilielezea jinsi Muundo wa Makubaliano ni bidhaa iliyochochewa na ukoloni kulingana na imani na thaqafa ya Kimagharibi, yenye lengo la kuunda dola ya kidemokrasia, ya kifederali, ya kibunge, ya kisekula ambayo sheria zinatungwa na watu badala ya kuvuliwa kutoka kwenye Qur’an na Sunnah. Hii inataka kuwaweka mbali Waislamu wa Sudan na Dini yao na itaipelekea tu Sudan kwenye njia nyingine ya kufeli na mgawanyiko kama ilivyokuwa katika nchi za magharibi pamoja na ardhi za Kiislamu. Bali ni Dola ya Khilafah pekee kwa njia ya Utume ndiyo ambayo inatabikisha Sheria na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukamilifu wake inayoweza kukomesha uingiliaji wa kikoloni nchini Sudan na kuleta mafanikio katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na nyanja zote za maisha, kuondoa migawanyiko na kuunganisha watu wake na jeshi, na kuunda viongozi wa kisiasa ambao ni walinzi wa raia wao.

Kampeni hiyo ilijumuisha ushiriki mkubwa wa mitandao ya kijamii duniani katika lugha na nchi mbalimbali, ikiwemo uchapishaji wa makumi ya makala, mamia ya machapisho na mabango kwenye mitandao ya kijamii, na video kadhaa, zikiwemo zifuatazo:

“Jinsi Uislamu Ulivyoingia Sudan”

https://www.dailymotion.com/video/k3hfUPAabl5GIYDJkJU  

“Vita vya Sudan: Dhahabu, Silaha na Siasa za Jiografia”

https://dai.ly/k2G7j01TKZtlGMDRRK8

"Khilafah Pekee ndiyo Itakayoiletea Sudan Izza"

https://dai.ly/k1itSmPUE2cOeHDU5wQ

Pia ilijumuisha mijadala kwa Kiarabu na Kiingereza ikieleza sababu na matokeo ya mzozo wa sasa, na jinsi mfumo wa Khilafah, badala ya muundo wa kidemokrasia, ungeweza kutatua matatizo mengi yanayoikabili Sudan.

Ingawa kampeni sasa imehitimishwa, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kitaendelea kuhamasisha kuhusu siasa, ajenda na matokeo ya mzozo wa Sudan pamoja na njia za kumaliza mateso ya watu wake, kutatua matatizo yao na kujenga mustakabali mwema wa ardhi yao chini ya dola ya Khilafah.

Nyenzo zote za kampeni zinaweza kupatikana katika:

https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/kampeni/4806.html

Facebook: Ht-cmo-ws

Instagram: WomenShariah5

X: @WSCMOHT1924

Link ya video ya kampeni:

https://htmedia.htcmo.info/CMO_WS/2025/08/SDN_Camp_Trailer04082025En.mp4

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal: 24]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu