Afisi ya Habari	
				
				Afisi Kuu ya Habari
			
| H. 4 Jumada I 1447 | Na: H 1447 / 022 | 
| M. Jumapili, 26 Oktoba 2025 | 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watawala wa Waislamu Hawana Sifa za Kulinda Heshima ya Waislamu!
 (Imetafsiriwa)
Vyombo vya habari viliripoti kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alicheza densi kwenye zulia jekundu kwenye uwanja wa ndege nchini Malaysia mnamo Jumapili, 26/10/2025, alipopokewa na Waziri Mkuu wa Malaysia. Idadi ya Wamalaysia, wanaume na wanawake, walipunga bendera za Marekani na kucheza muziki wa kienyeji ili kumkaribisha mhalifu huyo muuaji ambaye mikono yake imejaa damu ya Waislamu wa Gaza.
Rais wa Imarati, Mohammed bin Zayed, alikuwa amefanya jambo hilo hilo hapo awali, wakati wa ziara ya Trump nchini Imarati mnamo 15/5/2025, wakati kundi la wasichana wadogo lilijipanga na kuchezesha vichwa kunakolingana na mdundo wa muziki wa kitamaduni.
Jinsi watawala hawa wanavyowaanika wanawake Waislamu mbele ya mhalifu wa kivita haina uhusiano wowote na Uislamu na haiwawakilishi Waislamu. Msimamo halisi ni ule wa watu wa Malaysia waliokusanyika katika Uwanja wa Merdeka (Uwanja wa Uhuru) jijini Kuala Lumpur saa 9:00 asubuhi, chini ya ulinzi mkali, wakiinua mabango dhidi ya Trump na umbile la Kiyahudi, na kuimba “Iacheni Huru, Iacheni Huru Palestina.” Huu ndio msimamo halisi wa Ummah wa Kiislamu dhidi ya wahalifu hawa, si kile ambacho watawala hawa ruwaibidha (wajinga wasio na maana) wanafanya.
Hadhara yetu ya Kiislamu, inayowakilisha jumla ya fahamu zetu kuhusu maisha, inaamuru kwamba wanawake ni heshima ambayo lazima ilindwe, si kwamba miili yao ionyeshwe ili kuwakaribisha wauaji wa watoto wa Waislamu. Muuaji huyu mhalifu anacheza densi, akifuatana na mkewe aliyevaa nguo zinazoonyesha umbo lake, wakiwakilisha hadhara yao ya Kimagharibi iliyojaa muozo, hadhara chafu na fisadi! Kama kungekuwa na mwanamume miongoni mwa watawala wa Waislamu, wasingempokea katika nchi zetu, wala wasingenyoosha mikono yao kushika mikono yake iliyojaa damu ya Waislamu!
Njia sahihi ya kuamiliana na wale waliotenda uhalifu dhidi ya Waislamu ni kile ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Makhalifa baada yake walifanya. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), alimtuma Muhammad ibn Maslamah kwa Ka'b ibn al-Ashraf ili amuue kwa sababu alikuwa amemdhuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa ulimi wake, kwani alikuwa mshairi kutoka kabila la Kiyahudi la Banu Nadir. Mayahudi wa Banu Qaynuqa' walipomshambulia mwanamke wa Kiislamu na kumuua Muislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliongoza jeshi kuwaadhibu. Makhalifa wa Waislamu waliomfuata Yeye (saw) walifuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wakiwakilisha izza ya Uislamu na Waislamu. Miongoni mwao alikuwa al-Mu'tasim, ambaye aliongoza jeshi lililoiteka Amuriyya kwa kuitikia kilio cha mwanamke wa Kiislamu. Hii ndiyo njia sahihi ya kuamiliana na mtu yeyote anayemdharau mwanamume au mwanamke wa Kiislamu au fahamu ya Kiislamu, anapaswa kukabiliwa na majeshi, sio kwa mapokezi makubwa au kwa kuwaanika wanawake wa Kiislamu!
Enyi Waislamu: Hamhitaji kukumbushwa umuhimu wa heshima, kwani tuna uhakika wa kuijali kwenu, na tuna yakini kwamba sisi na nyinyi tutatoa muhanga uhai na roho zetu ili kulinda heshima yetu. Lakini msiba wetu mkubwa ni watawala ruwaibidha (wajinga wasio na maana) ambao wamesalimisha nchi yetu na rasilimali zetu kwa wakoloni makafiri, wakakaa kimya kuhusu uhalifu wao dhidi ya watoto wa Waislamu, na hawakukomea katika kiwango hiki cha udhalilishaji na utumwa. Badala yake wanasalimisha utu na heshima yetu kwao. Ndiyo, dharau yao kwenu imefikia kiwango hiki, kwa hivyo mutakaa kimya kuwahusu hadi lini?
Afisi Kuu ya Habari
 ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari | Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info | Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info | 
 
			



