Jumamosi, 11 Jumada al-awwal 1447 | 2025/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  5 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 023
M.  Jumatatu, 27 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Wewe Ndiye Uliyewaletea Waislamu Njaa, Masoud Pezeshkian!
(Imetafsiriwa)

Iran ilitangaza kufilisika kwa benki yake kubwa zaidi ya kibinafsi, Benki ya Ayandeh, ambayo ina matawi 270 nchini Iran, baada ya madeni yake kupanda zaidi ya dolari bilioni tano, na kinachoshangaza ni ukosoaji wa rais wa Iran Masoud Pezeshkian kuhusu kushindwa kwa utawala akisema: “Tuna mafuta na gesi lakini tuna njaa”!

Je, inawezekana kwamba kauli hii imetolewa na rais wa dola inayomiliki utajiri mwingi sana – mafuta, gesi, kemikali, madini na kilimo – na ambayo, kwa jiografia yake, ukubwa wa idadi ya watu na rasilimali, inaweza kuwa miongoni mwa nchi kubwa duniani, na watu wake wanaweza kuwa miongoni mwa matajiri zaidi duniani? Ikiwa rais, mwenye mamlaka na amri, anasema hivi, je wananchi wa kawaida watasema nini?!

Mfumo wa utawala nchini Iran – kama serikali zengine katika ardhi za Waislamu – ndio ulioufanya Ummah kuwa na njaa, na ndio uliowezesha dola kubwa kunyakua rasilimali na utajiri wake; ndio ulioondoa mfumo wa Uislamu kutoka kwa utawala, ukakubaliwa utawala wa mifumo ya ukafiri, na ndio uliohalalisha mfumo wa riba nchini Iran.

Tatizo kubwa nchini Iran na katika nchi zote za Waislamu sio kufeli kwa utawala; bali ni mfumo wa utawala unaotekelezwa. Watawala wabaya wanalazimisha mfumo wa kibepari pamoja na ubaya wake wote juu ya Waislamu, na miongoni mwa mabaya zaidi ni mfumo wa riba, ambao ni tangazo la vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ambao huangamiza utajiri na kushusha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

Anayehusika na kufeli huko kwa utawala ambako rais wa Iran anazungumzia ni rais mwenyewe, kwa nini watu wa Iran wana njaa – Ewe Masoud Pezeshkian – huku mkiwa na mafuta na gesi na rasilimali nyingine na madini? Je, haya si matokeo ya sera zenu za kuyumba? Je, si kwa sababu ya kuwa mbali kwenu na kuhukumu kwa Uislamu?

Hayo hayo yanasemwa kuhusu ardhi zengine za Waislamu: watawala wao ruwaibidha hufuja utajiri mkubwa wa Ummah, huwawezesha makafiri wakoloni kuuteka, huunyima Ummah rasilimali hizo, na kisha mmoja wao huja kuhalalisha sababu ya njaa kwa kusema ni kufeli kwa utawala!

Enyi Waislamu: Ujinga wa watawala hawa wanaosimamia mambo yenu umedhihirika kwa kila mtu kwa kuona na ufahamu, na hawafai kuyasimamia. Ni wakati wenu kuwazuia; hii ndiyo hukmu kuhusiana na mtu mjinga: kumzuia kutumia pesa na kumwekea uangalizi. Mpeni bay’ah Khalifa mmoja anayewatawala kwa Shari’ah ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, anayefuta mfumo wa riba katika ardhi zenu ili Mola wenu afurahishwe nanyi na Mtume Wake (saw), anayeregesha utajiri wenu ulioporwa, na kurudisha hadhi na heshima yenu. Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakulinganieni mufanye kazi pamoja nayo ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu