Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
| H. 27 Rajab 1447 | Na: H 1447 / 21 |
| M. Ijumaa, 16 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mikutano na Matembezi ya Kulaani Yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh: Enyi Watu! Pingeni Mpango wa Kupeleka Jeshi Letu Gaza chini ya Kikosi Kilichopendekezwa na Trump, na Takeni Msimamo Wazi kutoka kwa Wagombea katika Uchaguzi Ujao
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh, iliandaa mikutano na matembezi mengi ya kulaani leo, Ijumaa (16 Januari 2026), baada ya swala ya Ijumaa, katika majengo mbalimbali ya misikiti jijini Dhaka na Chattogram, dhidi ya mpango wa kupeleka vikosi vya nchi hii kwa “Kikosi cha Kuleta Utulivu wa Kimataifa” kilichopendekezwa na Trump huko Gaza. Ili kupinga mpango huu mbaya wa Marekani, na kuwataka wagombea na vyama vya kisiasa katika uchaguzi ujao kuelezea msimamo wao kuhusu suala hili, watu waliimba kaulimbiu mbalimbali, ikiwemo: “Kikosi cha Trump huko Gaza – hatukikubali”. “Kutuma wanajeshi kwa kikosi cha Trump - Watu hawakubali”. “Viongozi wanaomtii Trump - Watu hawawataki”. “Watawala, watumishi wa Amerika - Imetosha, Imetosha”, “Watawala, wanaoisujudia Amerika - Hatutaki tena, Hatutaki tena”. “Amerika au Palestina? - Palestina! Palestina!”. “Dunia itakuwa salama - Chini ya Khilafah”. “Palestina itakuwa salama - Chini ya Khilafah”.
Wazungumzaji katika mikutano ya kulaani walisema kwamba: licha ya maombi ya mara kwa mara kutoka kwa watu, mamlaka tawala za Bangladesh hazikupeleka vikosi vya jeshi kuwasaidia Waislamu katika kukomesha mauaji ya halaiki yaliyofanywa na umbile la Kiyahudi, ambalo linafanya kazi kwa usaidizi wa Marekani; ilhali, kwa amri ya Amerika, sasa wanapanga kutuma wanajeshi kwa “Kikosi cha Kimataifa cha Utulivu” kilichopendekezwa na Trump - ambacho kwa hakika ni kikosi cha uvamizi huko Gaza kilichoundwa kutumikia maslahi ya umbile la Kiyahudi. Wakati ambapo uvamizi wa Marekani - nchini Venezuela na kote ulimwenguni - umeigeuza Marekani kuwa adui wa wanadamu, na wakati watu wa Bangladesh wanapopinga kiburi cha Donald Trump, umma unakataa kwa ukaidi uamuzi huu wa kijinga wa serikali ya mpito. Kuwa mshirika katika mpango wa Amerika wa kuwafukuza Waislamu kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na kuliimarisha umbile nyakuzi la Kiyahudi ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[لَا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ]
“Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu.” [Surah Aali-'Imran: 28].
Kupinga usaliti huu ni wajibu wa Kiislamu kwa Waislamu. Watu lazima wawatake wagombea na vyama katika uchaguzi ujao waseme waziwazi msimamo wao dhidi ya dola za kikoloni na za kikafiri za Magharibi. Zaidi ya hayo, vyama vya kisiasa na wanasiasa wanaoichukulia Amerika kama washirika lazima wakataliwe moja kwa moja.
Wazungumzaji, kwa kuwahutubia Maafisa Wenye Ikhlasi wa Vikosi vyetu vya Jeshi, walisema: Ni wajibu wenu wa kiimani kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na kukataa miungano yote ya kijeshi na dola za kikafiri za kikoloni. Miungano kama hiyo inawalazimisha Waislamu kupigana chini ya uongozi wa vikosi vya kikafiri, chini ya bendera ya ukafiri, kwa madhumuni ya kulinda umbile la Kikafiri—ambayo yote ni haramu. Mapigano hayaruhusiwi kwa Muislamu isipokuwa chini ya uongozi wa Muislamu na chini ya bendera ya Uislamu. Imam Ahmad na an-Nasa’i wanasimulia kutoka kwa Anas (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لاَ تَسْتَضِيئُوا بِنَارِ الْمُشْرِكِينَ» “Msichukue mwanga kutoka kwa moto wa Washirikina”. Ili kuweka damu yenu safi kutokana na vita hivi vya ukafiri, ni lazima mujiweke chini ya uongozi wa Khilafah na, ili kufikia lengo hili, ni lazima mukabidhi mamlaka kwa Hizb ut Tahrir—chama cha kisiasa chenye nia njema kinachofanya kazi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah ijayo itawapa uwezo wa kuzuia uvamizi wa Marekani, na kisha mngurumo wenu pekee utatosha kuwalinda Waislamu wa Palestina na wanadamu wanaodhulumiwa kote ulimwenguni.
[إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنْ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمْ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ...]
“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa...” [Surah At-Tawbah: 111]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |



