Jumamosi, 10 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  23 Jumada I 1444 Na: 1444 / 10
M.  Jumamosi, 17 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kubakia kwa Hali Halisi ni Sababu ya Kuendelea kwa Migogoro nchini Jordan na Kurudi kwa Ummah kwenye Chombo Chake cha Asili ndiko Kutakakoikomesha
(Imetafsiriwa)

Pindi Jordan ilipoanzishwa miaka mia moja iliyopita ndani ya ugawanyaji wa Sykes-Picot mikononi mwa wakoloni Makafiri wa Kiingereza na Wafaransa, ilizingatia vigezo vya kikoloni ambavyo vinafanikisha maslahi na matarajio ya nchi za kikoloni katika eneo hili ili matokeo ya ugawanyaji huu ulingane na malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu ya nchi za kikoloni za Magharibi na kudumu kwa ushawishi wake juu ya eneo hili kisiasa, kiuchumi na kiusalama, na kuwaunganisha watu wa ardhi hizi za Kiislamu na kupora mali zao katika njia ya kuridhia kujisalimisha kwa malengo haya. Kwa hivyo, ilikuwa ni lazima kwamba vijidola hivi viundwe kwa maelezo na viwango vinavyotawala udhibiti wa wakoloni makafiri na kuhakikisha wakati huo huo kwamba watu wa nchi hizi hawawezeshwi kujikomboa kifikra, kisiasa na kiuchumi, na kuhakikisha kwamba wasirudi tena kwenye dola yao yenye kuwaunganisha na umoja, kwa hivyo ilikuwa ni lazima kuwe na pembejeo bandia na maadili ya kishetani ambayo Mwenyezi Mungu kamwe hakuyateremsha, ili kufikia matokeo kwa msingi wa miundo ya Sykes-Picot ambayo ilianzishwa na hatma ambayo watu wamefikia leo katika udhalilifu na uduni, uporaji wa mali zao na kujisalimisha kwa maadui zao, na ya muhimu zaidi ni:

1. Mgawanyiko na mtawanyiko wa dola ya Kiislamu katika vijidola vingi chini ya majina ya dola ya kitaifa, ambazo bendera za kitaifa zilitengenezwa kutoka mwanzo ambazo zilichorwa na mikono ya wakoloni ili kuzibadilisha na bendera ya Umma unayounganisha; bendera ya hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kila nchi ilizungukwa na uzio mzito wa mipaka unaozuia umoja wake kwa kisingizio cha ubwana wa kindoto, na historia bandia ya kitaifa ikaundwa kwa kila nchi, ikitenganishwa na historia yake tukufu ya Kiislamu iliyotawala kwa karne nyingi tangu ushindi wa Kiislamu mikononi mwa Maswahaba watukufu, kisha walinzi wakapandikizwa kwa umbo la watawala na mistari ya aina ile ile iliyotengenezwa chini ya usimamizi wa Kafiri mkoloni na kuiangalia kila mara, kulinda ubunifu huu bandia ili kuhifadhi magofu yake angamivu ya kikoloni.

2. Imeeneza sumu yake ya kithaqafa kwa uvamizi wa taratibu na ulaghai muovu ili kuwatenganisha watu na mfumo wao wa Kiislamu na kuutenga mfumo wake katika utawala na imani yake. Badala yake, hivi karibuni imeshambulia msingi wa imani yao na maadili yake, na kuyafanya maadili yake potovu kuwa miongoni mwa mahitaji ya mgao katika katiba zake zilizotungwa na binadamu kama vile demokrasia, yaani, kuweka sheria mikononi mwa watu chini ya jina potofu la kuwatawala watu, na usawa wa wanawake na wanaume (CEDAW), haki za watoto, mambo yasiyo ya kawaida, mikopo yenye riba, mikataba ya kupora mali, mikataba ya amani pamoja na maadui, kufungua nchi na kuruhusiwa kwake kwa mkoloni wa Magharibi.

3. Kila kijidola kiliunda dori na kazi inayolingana na kazi iliyokabidhiwa, kwa hivyo nchi zenye utajiri wa mafuta zilikuwa zikiwekeza nchini Amerika na Uingereza, kupora mafuta yao na kumpa kipaumbele junta anayetawala kwa utajiri, na ikapandikiza umbile la Kiyahudi nchini Palestina, na kukabidhiwa kulinda usalama wake na kisha kuliwezesha kiuchumi na kuliingiza ndani ya mwili wa Ummah, ndani ya tawala za nchi zinazoizunguka Palestina, kama vile Jordan Misri, Lebanon na Syria, na kwa sababu hiyo uanzishwaji wa Jordan ulikuwa sawa na dori yake katika kulitambua umbile la Kiyahudi na kuhitimisha nalo mikataba ya kiusalama na kiuchumi ili kuliongezea uwezo kwa kisingizio cha umasikini wake uliokithiri, na ndiyo iliyoasisiwa pia kutengwa na mizizi yake ya Kiislamu na Kiarabu, na kuwa katika huruma ya misaada, ruzuku, mikopo yenye riba, na mzigo wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na misaada ya Marekani, ili hoja endelevu ya utawala huo iwe ni kuweka rehani uamuzi wake wa kisiasa kwa Kafiri mkoloni, licha ya utajiri ulio chini ya ardhi ambao Mwenyezi Mungu ameujaalia nchi hii.

Kutokana na matokeo ya hali hii isiyo ya kawaida ya kijiografia na kisiasa, mfumo wa kisiasa nchini Jordan unapitia migogoro ya mara kwa mara ya ndani kila wakati - na kila wakati inatafuta tu kuleta utulivu wa utawala wake – mgogoro wa hivi punde zaidi ni mgomo wa madereva wa malori na kukatizwa kwa harakati zengine za usafiri kama vile mabasi na teksi, ambazo ziligeuka kuwa mgomo mkubwa wa maduka katika majimbo kadhaa ya Jordan, sababu yake ikitajwa kuwa ni kupandisha bei ya bidhaa zinazotokana na mafuta, kama vile dizeli na mafuta ya taa, ambapo watu wanalipa bei ya juu zaidi ya bidhaa hizi duniani, ambapo waziri mkuu alikadiria kuunga mkono kama anasa ambayo serikali haitaifanya, licha ya matumizi mengi ya anasa ya serikali hii fisadi, na katika mambo ambayo umma hauungi mkono kama vile kuondoa maadili ya Uislamu, imani na mfumo wake, na kuruhusu maadili ya maovu yaliyoingizwa kutoka Magharibi Kafiri, urafiki na ushirikiano wa kimkakati na maadui wa Ummah na kuyasalimisha maamuzi yake kwa maagizo yake ya kudhalilisha.

Nchi imepitia migogoro ambayo inaharibu uthabiti wa kisiasa wa serikali, na hivi karibuni mmoja wao anayumba na suluhisho la viraka, hadi kufuatiwa na mwengine, mkali zaidi na wenye nguvu. Kwa hiyo kutokana na mgogoro wa chama cha walimu, ukamataji, kuonewa mara kwa mara, na kunyamazisha midomo kwa ajili tu ya kutoa maoni, ukosefu wa ajira uliofikia 50% miongoni mwa vijana, na madeni ambayo yamefikia 114% ya pato la taifa, licha ya kodi kubwa, na Maagizo ya IMF ambayo yamepelekea uchumi wa nchi kwenye shimo, na misaada ya Amerika, ambayo imefikia kilele chake kwa badali ya jeshi na ushawishi, na makubaliano ya gesi, kawi na maji na umbile la Kiyahudi, na bei ya juu ya mahitaji msingi, pamoja na kueneza uasherati na uchafu na kupenya kwa sheria za maadili za Kimagharibi zinazopingana na maumbile na maadili ya Kiislamu ya watu.

Utawala wa Jordan unashughulikia migogoro hii kwa masuluhisho ya haraka, ya kivipande kutoka ndani ya uhalisia na dhurufu zilizoianzisha, na wakati wa kutatua kila tatizo, unalenga kuleta utulivu kwa utawala wake na si kutatua matatizo ya wananchi. Pindi mambo yanapokuwa magumu, hauleti madhara kwa utawala kupindua serikali na kuteua nyengine, kwani kiasili haina mamlaka ya kiutendaji kwa kutengwa na mielekeo ya utawala, iwe ya usalama au ukoloni wa Marekani Magharibi na Uingereza. Sera ya utulivu wa kiasi wa serikali hivi karibuni inarudi na migogoro mikubwa zaidi kuliko watangulizi wake, ambayo watu hulipa gharama yake kwa nguvu zao, heshima na maisha ya watoto wao, mradi tu masuluhisho ni kama mangati na uhadaifu, na hayaelekezwi kwenye mzizi wa tatizo.

Haiudhuru utawala kujificha nyuma ya vyombo vya ulinzi na usalama vya dola, vya kiserikali na bunge unapowakabili wananchi ili kuwaingiza wananchi katika tukio la kipuuzi na la ajabu, na kuacha mambo yaende kwa siku nyingi hadi kufikia makabiliano baina ya wananchi na watoto wao katika idara za usalama, ambayo husababisha majeraha na uharibifu wa mali. Kwa hivyo, mgogoro hugeuka, kama ilivyo katika kila mgogoro, kutoka kwa kufeli kwa dola kutawala, kusimamia, na kujibu matakwa ya watu, hadi kuwa rai jumla na mwavuli ambao kivuli chake kinahalalisha ukandamizaji na unyanyasaji katika harakati zote maarufu za matakwa, bila kusahau Mradi wa Ummah wa mwamko na kurudi kwenye utawala wa Kiislamu.

Mzizi wa tatizo ni kwamba Jordan, ambayo ni sehemu ya Umma wa Kiislamu, kama zilivyo dola zote za Sykes-Picot, kama tulivyotaja hapo juu, ilitenganishwa na nchi mama yake, yaani, dola ya Kiislamu, katika zama za udhaifu wake na kuanguka kwake, ambayo ni milki yake kimfumo, na kuiunganisha na watu wa nchi jirani kupitia fungamano la mfumo wa Kiislamu bila ya kuzingatia mipaka yoyote, na suluhisho la matatizo yake na matatizo yake litakuwa ni kuregea kwake, na nchi zote za Ash-Shaam, kuwa sehemu ya dola ya Khilafah, hivyo itakuwa ni sehemu yake nayo ni sehemu yake, kwa hiyo itaondoka katika ukandamizaji wa watawala, utawala wao, ufisadi wao, na kujitiisha kwao chini ya ukoloni hadi kwa uadilifu na utekelezaji wa Uislamu. Kwa hiyo migogoro yake yote itatatuliwa, na watu wake watafurahia heshima, hadhi na uadilifu, na hakika Waislamu wote watafurahia utajiri na mali ya umma katika nchi zao, badala ya kuporwa na Marekani na Ulaya, na badala ya kutegemea misaada ya adui Marekani na Uingereza yenye nia mbaya, na itasimama kwa fahari na utu dhidi ya adui umbile la Kiyahudi badala ya makubaliano ya aibu na udhalilifu, hata kama hilo litaonekana kwa baadhi, ni vigumu kufikiwa. Hata hivyo, mwendo wa matukio na hali ambazo watu huzishuhudia kutokana na ufumbuzi usio na msaada ni utatuzi wa muda tu unaozidisha migogoro na kurefusha suluhisho ambalo Mwenyezi Mungu alilitaka kwa Umma huu, kisha hautashinda isipokuwa kwa kumnusuru kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammed:7]

Enyi Waislamu, Enyi Watu wa Jordan: Hali za sasa za watu wanaoishi katika nchi za Kiislamu na ugumu wa maisha ambao watu wengi wanauhisi katika nyanja zote za maisha, kama vile elimu, afya, huduma, kutengwa kwa watoto, udhalilishaji na uchokozi wa maadui wa Ummah dhidi ya nchi yake na uporaji wa rasilimali zake, ni muendelezo wa yale aliyoyaanzisha mkoloni Kafiri. Na kiongozi wake ni Uingereza na kisha Amerika baada ya kupinduliwa Dola ya Khilafah, na inachotaka ni kuendelea kwa machafuko, wasiwasi, njaa, umasikini, na ufisadi wa serikali na watu wake wa ndani, ili kutekeleza mipango yake katika nchi za Kiislamu na kufikia maslahi yake. Muhimu zaidi, kwa hakika, ni utayari na hofu ya mwamko wa Ummah, ambao uko karibu kwa kusimamishwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itasimama msimamo halisi mbele ya maadui wa Ummah, ambayo itaondoa mipaka iliyowekwa na ukoloni, na ambayo itarudisha mali yote iliyoibiwa kwa Ummah ili kuifurahia, itatatua matatizo yake, na kuelekeza hasira yake. Na kuandaa majeshi yake kule kunakotakiwa kuelekezwa, nao ni maadui wa Umma wanaosimama katika njia ya ukombozi wake, ukombozi wa matukufu yake, na utekelezaji wajibu wa kubeba ulinganizi unaomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu