Jumamosi, 04 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/05/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: 1446 / 19
M.  Jumapili, 25 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Yalazimisha Watu Kusherehekea Uhuru Unaodaiwa Sambamba na Mauaji ya Kikatili ya Halaiki!

(Imetafsiriwa)

Je, watu wa Jordan wanasherehekea uhuru unaodaiwa wakati jana, daktari Muislamu mwenye msimamo thabiti huko Gaza alipoteza watoto wake tisa wote kwa wakati mmoja, kutokana na kombora lililorushwa na ndege ya jeshi la mauaji ya halaiki nyumbani kwao, katika mandhari ya kinyama isiyo na kifani katika historia ya mwanadamu?

Je, hisia za udugu wa Kiislamu zimekufa ganzi kwa mandhari ya kuhuzunisha ya kuendelea kwa Mayahudi katika kuua, kutia njaa na uharibifu? Badala ya kuwanusuru, kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyoamrisha.

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia [Al-Anfal: 72]

Inaonekana kwamba Umma umekubali kuishi na (wazo la) kusubiri majeshi yake yasonge, na hata kushiriki na waliofiwa, mayatima, na wenye njaa. Mwenyezi Mungu amekufanyeni Umma mmoja , tofauti na watu wengine.

[وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ]

Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi. [Al-Mu’minun: 52]

Hapana, Wallahi damu ya watu wengi wa Jordan inachemka katika mishipa yao kwa hamu kubwa na kutamani kuwanusuru ndugu zao katika Dini, na serikali inajua hili na inaogopa ghadhabu zao. Badala yake, inataka kuelekeza hisia zao kwenye kile kinachoitwa uhuru wakati ardhi yake imejaa kambi za kijeshi za wakoloni makafiri, ambao uchumi wao umewekwa rehani kwa benki ya dunia ya kikoloni, na ambayo haisubutu kufanya uamuzi mmoja huru kwa manufaa ya Ummah, huku ikitazama kwa masafa ya pua na mdomo matendo ya umbile halifu la Kiyahudi kana kwamba ni kivutio cha watalii. Mauaji ya halaiki ambayo umbile la Kiyahudi linayafanya kwa kiburi kama hicho, lisingesubutu kuyafanya kama isingejisikia salama kutokana na adhabu.

Kwa hivyo ni nani anayesherehekea fataki katika anga ya Jordan chini ya uhuru huu unaodaiwa, wakati anga juu ya Gaza imejaa makombora ya uharibifu na mauti? Na ni nani anayejaza kurasa rasmi za vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya kiuchumi ya Jordan tangu uhuru wake, huku ikikabiliwa na madeni ya wakoloni, ukosefu wa ajira na umaskini, kuuza mali yake kwa uwekezaji wa kigeni wa wakoloni, na kuifikisha nchi kwenye ukingo wa kiu ya ufisadi unaoendelea, lakini ikatumia hiki kama kisingizio cha kuhalalisha mahusiano na umbile ngeni kupitia mikataba mbalimbali?! Je, sio ndio serikali na watawala wake?

Wazo la uhuru ni mwito wa kikoloni wa kuugawanya na kuuvunjavunja Ummah mmoja wenye Dini moja, unaofungamana na fungamano la kimfumo na imani. Mfumo mmoja wa serikali ulitekelezwa tangu Mtume Muhammad (saw) alipoanzisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina, na katika historia yote ya dola ya Kiislamu, hadi 1924 M, ilipopinduliwa na mhalifu wa zama hizo, Mustafa Kemal. Baada ya hapo, wakoloni wa makafiri walipata fursa ya kugawanya ardhi za Waislamu katika zaidi ya maumbo hafifu ya kitaifa hamsini yenye mipaka ambayo uwezekano wa migogoro uko. Waliwapandikiza watawala waliojitengezea juu yao, ambao waliwatii katika chochote walichotaka. Ili kudumisha uwepo wao madarakani, walianzisha fahamu ya kitaifa ya dola ya kitaifa na kuunda kwa kila mmoja historia ya kirongo iliyotengwa na historia yake angavu kama sehemu ya historia ya dola yao ya Kiislamu.

Serikali inayotawala ndio iliyounda sherehe ghushi za uhuru na kuziweka kwa watu ambao hisia zao zimejaa chuki kwa kushindwa kwao kuwasaidia ndugu zao mjini Gaza. Inajaribu kuutengenezea Ummah utukufu wakati wa utawala wake ambao unaweza kujidai wenyewe, ingawa bado haujatimia. Hili linafanywa kwa njia ya mawazo potovu yenye msingi wa utaifa wa msingi ambao unauweka wakfu kama badali ya fungamano la kimaumbile na kimfumoi la Ummah, ambalo linahusisha kurudi kwenye utukufu wake wa zamani; kutaka kupata radhi za Mola wake Mlezi kwa kutumia sheria yake, kuwanusuru ndugu zake katika imani, kuiregesha ardhi iliyokaliwa kutoka kwa wakaazi wake, na kuwafukuza wakoloni makafiri, kambi zao na makampuni yao. Mwenye kusherehekea uhuru ni yule ambaye ana nia ya kuweka mipaka na kuzuia umoja wa Waislamu, kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote. Ni yule anayeichukulia mikataba yake na umbile la Kiyahudi na Amerika kuwa muhimu zaidi kuliko kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa na kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Serikali inayowatia hofu watu kwa kuwafunga mdomo na kumkamata yeyote anayelingania Uislamu kama itikadi na dola na yote yanayoamrishwa na amri za Mwenyezi Mungu, yanayogongana na misimamo ya dola na wale wanaodai utiifu kwa "nchi," ambao wamejaa katika vyombo vya habari rasmi, na wanaofasiri na kuunga mkono madhalimu. Inahofiwa kuwa maneno hayo ya Mwenyezi Mungu (swt) yatawahusu wao:

[رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا]

Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. [Al-Ahzab: 67].

Haya yote yatazidisha azma na chuki ya Ummah, na utaandika katika kumbukumbu zake matendo yaliyowaleta kwenye unyonge na udhalilishaji huu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ، وَيُنْتَقَصُ فِيهِ عِرْضُهُ إِلا خَذَلَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَتُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ إِلا نَصَرَهُ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ»

“Hatomtelekeza Muislamu Muislamu mwengine katika sehemu ambayo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika mahali ambapo angetaka msaada wake; na hakuna Muislamu ambaye atamsaidia Muislamu mahali ambapo heshima yake itavunjwa na utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia mahali ambapo angetaka msaada wake.”

Angalia umesimama wapi katika mazungumzo haya, na serikali inatumia nini katika masuala ya sherehe feki ili kumakinisha uhuru wa uongo, na kuwasaliti ndugu na dada zako katika Uislamu.

[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعاً وَلاَ تَفَرَّقُواْ وَاذْكُرُواْ نِعْمَةَ اللهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاء فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَاناً وَكُنتُمْ عَلَىَ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. [Aal-i-Imran: 103]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu