Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442/15 H
M.  Alhamisi, 08 Julai 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uzinduzi Rasmi wa Kampeni ya Kiuchumi ya Hizb ut-Tahrir / Kenya Chini ya Kauli Mbiu:

Msoto wa Kiuchumi: Uislamu Ndio Jibu.

Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya imezindua rasmi kampeni ya kiuchumi itakayodumu kwa mwezi mmoja. Kampeni hii itaanza tarehe mosi ya mwezi mtukufu wa DhulHijja 1442 Hijria sawasawa na tarehe 11 Julai 2021 na kutamatika  Agosti 11.

Kampeni hii inalenga kuangazia uhalisia wa mfumo wa Kiuchumi wa Kibepari na jinsi ulivyosababishia umma majanga ya kiuchumi. Aidha, inalenga kuweka wazi uhalisia wa mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu na athari yake katika kipindi cha karne 13 pindi Uislamu ulipokuwa na utawala wake wa Khilafah pia na vipi pindi itakaposimama hivi karibuni kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu SWT itaweza kutatua matatizo ya kiuchumi na mengineyo.

Kwenye kampeni hii, Hizb ut-Tahrir / Kenya itaandaa msururu wa amali ikiwemo mihadhara mbalimbali katika maeneo mbalimbali, mazungumzo ya mitaani, semina na wasomi na mufakirina miongoni mwa amali nyengine.

Mwisho, tunatoa mwito kwa jamii kwa jumla na hasa Umma wa Kiislamu kushiriki nasi katika kampeni hii tukufu ambayo ndani yake hatutarajii lolote ila malipo kwa Mwenyezi Mungu SWT. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) afanikishe kampeni hii na ifanye kuwa ni yenye kuleta kheri kwa Umma wote wa Kiislamu.

Fuatilia Kampeni hii kwa Hashtag:

Kiswahili: #MsotowaKiuchumi_Uislamundio_Jibu

Kiingereza: #EconomicHardships_IslamIsTheSolution

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir

Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu