Afisi ya Habari
Kenya
H. 28 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: 1446/10 H |
M. Jumanne, 24 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji ya Polisi: Hulka ya Kibepari ya Ukatili na Kutojali Sheria
(Imetafsiriwa)
Maafisa watatu wa polisi nchini Kenya wameshtakiwa kwa mauaji ya mwanablogu mwenye umri wa miaka 31 aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi mapema mwezi huu. Kifo cha Albert Ojwang kimezua hasira nchini Kenya huku maandamano yakifanyika kudai haki.
Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya, tungependa kuangazia yafuatayo
Chini ya tawala za kisekula za kiliberali kama vile Kenya maafisa wa usalama ni muendelezo wa muundo wa enzi ya ukoloni ambapo Waingereza waliutumia kudhibiti idadi ya watu na kukomesha upinzani. Katika miaka ya 1950, Wakenya walipoanza kudai haki yao ya kujitawala, polisi na vyombo vyengine vya usalama vilivyosimamiwa na Uingereza vilikusanya makumi ya maelfu ya Wakenya na kuwanyonga zaidi ya elfu moja.
Inavyoonekana, jeshi la polisi linawaona raia wa kawaida kama tishio linalowezekana kwa serikali inayotawala njia ambayo ilianzishwa hapo awali ili kutekeleza utawala wa kikoloni-sio kulinda raia.
Kimfumo, tawala za kisekula za kiliberali huona manufaa na maslahi kuwa kipimo kikuu kipaswacho kutukuzwa zaidi hata kuliko maisha ya binadamu na mali, Kwa vipimo hivi ndio hufanya ufisadi, kutojali sheria na kutekwa mamlaka ya dola na genge la watu fulani kama ada ya kisiasa. Kwa kuzingatia hili, mauaji ya vyombo vya dola bila kuadhibiwa ndiyo njia pekee ya kuzuia sauti yoyote ya upinzani na juhudi za kufichua ufisadi mkubwa. Ni muhimu kubaini kwamba ukatili na utesaji unaofanywa na vyombo vya dola ni mtindo na tatizo la kiulimwengu wala haliko tu kwa Kenya.
Tunasisitiza kwamba uhai wa binadamu au tuseme uhai wote ni mtakatifu na hustahili kulindwa kikamilifu na serikali bila uoga au mapendeleo. Katika Uislamu, ulinzi wa maisha ya mwanadamu ni muhimu na unachukuliwa kuwa amana kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Uislamu unasisitiza utakatifu wa uhai, hivyo umeharamisha kuuwa huku ukitaka ulinzi wa maisha na heshima kwa wanadamu wote.
Tunasisitiza kwamba ni chini ya Khilafah Rashida pekee ambayo itasimamishwa hivi karibuni kwa njia ya Utume, jeshi la polisi litakuwa na jukumu la kudumisha utulivu wa umma, kutekeleza sheria, na kuchunguza uhalifu. Mateso ni marufuku kabisa na afisa polisi yeyote atakayepatikana na hatia ya kutekeleza unyanyasaji wa kimwili au mateso dhidi ya raia yeyote, Muislamu au asiye Muislamu, atawajibishwa. Kwa hivyo, vikosi vya polisi vitajitolea kikamilifu kudumisha sheria na utulivu na kulinda uhai na mali za raia.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |