Jumatatu, 24 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/05/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  17 Dhu al-Qi'dah 1447 Na: H.T.L 1447 / 21
M.  Jumatatu, 04 Mei 2026

Kama Sehemu ya Kampeni ya “Waislamu Dhidi ya Uhalalishaji Mahusiano”
Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon Yafanya Msururu wa Ziara
(Imetafsiriwa)

Kwa kuzingatia mamlaka ya Lebanon kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja ambayo hakika yatapelekea katika amani na uhalalishaji mahusiano na umbile nyakuzi na halifu la Kiyahudi, na kama sehemu ya kampeni ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon kuwatembelea wanasiasa, mamufti, wasomi, nyanja ya kisiasa, na watu mashuhuri, wajumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano na kamati za shughuli za kikanda walifanya ziara. Hizi zilianza katika mji wa Sidon kusini mwa Lebanon kwa ziara ya Mbunge Dkt. Osama Saad, Katibu Mkuu wa Shirika Maarufu la Wananasseristi, na ziara ya Mufti wa Sidon na wilaya zake, Sheikh Salim Sousan. Hii ilifuatiwa na ziara katika mji mkuu, Beirut, kwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Shia, msomi Sheikh Ali Al-Khatib.

Ziara hizi zilisisitiza msimamo wazi na wa kukatikiwa wa Hizb ut Tahrir wa kukataa mazungumzo, maridhiano, na utambuzi wa umbile la Kiyahudi. Zililenga umuhimu wa kutabanni msimamo wazi kuhusu mwenendo wa mamlaka katika mwelekeo huu chini ya jina lolote, kama vile amani, kukomesha vita, kupunguza hasara, au ahadi za kiuchumi. Katika dhurufu zozote hakuna mtu yeyote anayeweza kuidhinisha kuendelea kwa ukaliwaji wa kimabavu wa Jerusalem na viunga vyake na wale walioinyakua, bila kujali hoja yoyote. Hii ni pamoja na uhalifu wa umbile hili na uvamizi wake dhidi ya Gaza, Lebanon, na Iran, unaofanywa waziwazi bila kizuizi chochote, hasa kwa usaidizi wa wazi wa Marekani.

Wajumbe hao walisisitiza kwamba Lebanon, kama nchi zengine, ni sehemu ya ardhi za Kiislamu, ambazo kimsingi zinapaswa kuwa chini ya dola moja kwa Ummah mzima chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Bila umoja huo, Lebanon na zengine zitabaki kuwa uwanja wa kudanganywa na dola za kikoloni za kikafiri, ya kwanza miongoni mwao Amerika na wakala wake, umbile la Kiyahudi.

Wajumbe hao pia walisisitiza umuhimu na wajibu wa mapambano ya kisiasa dhidi ya mwelekeo wa mamlaka ya Lebanon ya kujadiliana na umbile la Kiyahudi. Hili linapaswa kufanywa na makundi yote ya kisiasa yanayotambua uhalifu wa umbile la Kiyahudi na hayakubali uvamizi wake. Duara za kisiasa zinazopinga njia hii, pamoja na wanazuoni na watu mashuhuri, lazima zifanye kazi ili kuanzisha rai jumla ya umma ambayo inaimarisha msimamo huu dhidi ya watawala wanaoegemea upande na Amerika.

Wajumbe walifafanua kwamba ingawa Hizb ut Tahrir inaona kupigana na Mayahudi ili kuwafukuza kutoka katika ardhi zote zinazokaliwa kama faradhi, ya kupongezwa, ya lazima, na yenye mizizi mirefu katika kumbukumbu na historia ya Ummah, pamoja na dini yake, pia inawaambia wale wote wanaopigana na Mayahudi: suluhisho la kweli na kamili litakuja tu kupitia umoja wa Waislamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hapo ndipo tu umbile hili nyakuzi litaondolewa, ushawishi wa Amerika utakatiliwa mbali, na njama zake zitarudishwa juu yake. Ummah wa Kiislamu utarudi ukiwa na nguvu na heshima, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt), na hili haliwezi kupatikana na wale wanaojadiliana na Amerika na umbile lake halifu au kupatana nao au kukubali kuendelea kwao kuwepo katika ardhi za Waislamu.

Kwa kumalizia, wajumbe hao walisisitiza mwendelezo wa mawasiliano na watu wote mashuhuri wa umma na wanasiasa ili kufikia lengo la kampeni ya Hizb ya “Waislamu Dhidi ya Uhalalishaji Mahusiano”, kwani sisi ni Ummah mmoja wenye adui mmoja. Wanamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aupe Ummah huu afueni na ushindi wa karibu:

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum:4–5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu