Uamuzi wa Kesi ya Mauaji ya Shahzaib ni Uthibitisho wa Kushindwa kwa Idara ya Mahakama ya Pakistan Idara ya Mahakama ya Shariah ya Khilafah ndio Suluhisho Pekee
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Oktoba 18, benchi la majaji watatu wa Mahakama ya Upeo ilimwondolea mashtaka mshtakiwa Shahrukh Jatoi, kwa mauaji katika kesi maarufu ya mauaji ya Shahzeb. Ingawa hukumu hii ilizua shutuma za umma, haikuwa isiyotarajiwa. Katika makumi ya hukumu za awali, zikiwemo kesi za Nazim Jokhi, Raymond Davis, Abdul Majeed Achakzai, mahakama zimewapa wakoloni na watu wengine wenye nguvu njia ya kutorokea kupitia mianya mbalimbali ya kisheria.