Alhamisi, 20 Safar 1447 | 2025/08/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  28 Muharram 1447 Na: 02 / 1447
M.  Jumatano, 23 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Njia ya Kujiondolea Dhambi ya Kuwatelekeza Waislamu wa Palestina, ni Kujitahidi Mchana na Usiku Kusimamisha Khilafah Rashida, na Kukusanya Majeshi

(Imetafsiriwa)

Kwa vile majeshi ya Waislamu hayakusonga kuinusuru Gaza, baba mwengine aliyedhulumiwa, Abu Umar, aliuawa shahidi, alipokuwa akiwatafutia watoto wake chakula. Alipokuwa akingoja kupokea msaada, risasi ya mdunguaji Myahudi muoga ilipenya kichwa chake. Yule rafiki aliyeuleta mwili wake alikuwa na njaa kwa siku tano, na akarudi kutoka kwenye kizingiti cha mlango wa shahada, labda kuuawa shahidi hivi karibuni. Hili sio tukio moja pekee. Makumi ya matukio kama haya yanashuhudiwa moja kwa moja kila siku, na Umma wa bilioni mbili.

Maswali uchungu hayakufungika na swali moja pekee. Wanaume, wanawake, na watoto wanaodhulumiwa wa Palestina wataendelea kuchinjwa hadi lini? Je, itachukua kafara ngapi zaidi za mashahidi ili kuhamasisha majeshi? Dada zetu wataendelea kupiga kelele na kulia hadi lini? Hadi lini Mayahudi wataendelea kukanyaga maisha, mali, na heshima ya Waislamu chini ya miguu yao? Tutatulia tuli hadi lini? Je, mpaka lini tutabakia kujifunga na kutoa Dua kwa wanaodhulumiwa na kuwalaani madhalimu?

Fauka ya yote, Siku ya Kiyama Waislamu waliodhulumiwa wa Palestina wanaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) na kulalamikia sio tu watawala wa Waislamu na majeshi yetu, bali sisi sote, je tutajibu nini? Tulikuwa wapi wakati watoto wao wanakufa? Walipokuwa wakipiga kelele, mbona sisi tulitulia tuli? Jibu letu litakuwa nini kwa malalamiko hayo? Mwenyezi Mungu (swt) atakapotuuliza Siku ya Kiyama juu ya kughafilika kwetu faradhi ya Shariah, tutajibu vipi? Je! maisha ya dunia yalitupendeza zaidi kuliko akhira? Je, ni mapenzi ya wazazi na watoto ambayo yalituzuia? Je, kazi na biashara zetu zilituzuia kutekeleza amri yake? Je, majibu yetu kwa maswali haya ni yapi?!

Kuna njia ya kuokoka na aibu na majuto Siku ya Kiyama, na kujitayarisha kwa hisabu yetu: Ni lazima tuvunje kimya chetu na kupaza sauti zetu leo. Yeyote anayetaka kuokolewa na hisabu kali Siku ya Hisabu lazima, kwa nguvu zote, adai kutoka kwa majeshi ya Waislamu kwamba wajikusanye mara moja katika kuwanusuru ndugu zao waliodhulumiwa huko Gaza, na kuwapindua wale watawala na makamanda wa kijeshi, ambao ndio kizuizi kikubwa zaidi katika njia ya Jihad katika kuwanusuru Waislamu wa Palestina.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Kukaa kimya na bila kusonga mbele ya dhalimu anayeshambulia ni aina ya usaidizi kwa mauaji ya ukandamizaji. Kwa hiyo, inukeni na mupaze sauti yenu. Watikiseni askari na maafisa wanyoofu katika vikosi vya jeshi. Wakumbusheni faradhi yao ya Shariah.

Waambieni kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha,

[انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ]

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu.” [Surah At-Tawbah 9:41]. Waambie kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amewafaradhisha kuwasaidia Waislamu wa Palestina. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَاِنِ اسْتَنْصَرُوْكُمْ فِی الدِّیْنِ فَعَلَیْكُمُ النَّصْرُ] 

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al-Anfal 8:72]. Waambieni wasipopigana kuwatetea Waislamu wanaodhulumiwa wa Palestina, wataulizwa. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na Watoto?” [Surah An-Nisa 4:75].

Waambie maafisa na askari kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha kufanya miungano, kuhalalisha mahusiano na wale wanaoikalia kimabavu ardhi ya Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahanah 60:9]. Waambieni kuwa kumtambua mvamizi hairuhusiwi. Badala yake, amri ya Mwenyezi Mungu (swt) ni kumfukuza mvamizi kwa njia ya vita. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ] 

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191].

Waambieni maafisa na askari kwamba mfumo wa sasa umewafungia kwenye kambi, huku kutoa Nusrah (msaada wa kijeshi) kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume ni faradhi ya Shariah juu yao. Ni Khilafah ndiyo inayounganisha Ummah chini ya bendera moja ya Rayah, Imamu mmoja, na jeshi moja. Inawalinda watoto wa Abu Umar, inalipiza kisasi kutoka kwa wauaji wake, na inakupeni heshima ya kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, eneo la safari ya usiku ya Israa ya Mtume (saw). Tunaomba mutimize bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na mstahiki uombezi wake, enyi wana wa Muhammad bin Qasim! Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَا تَقُوم السَّاعَۃُ حَتّٰی یُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْیَہُودَ فَیَقْتُلُہُمُ الْمُسْلِمُونَ»

“Kiyama hakitasimama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu watawauwa.” (Sahih Muslim)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu