Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
| H. 22 Jumada I 1447 | Na: BN/S 1447 / 07 |
| M. Alhamisi, 13 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Abbas, Akizungumza kutoka Pango la Maadui wa Uislamu jijini Paris, Anathibitisha Dori ya Kihalifu ya Mamlaka ya Palestina katika Kutekeleza Sera za Marekani na Mayahudi Zinazolenga Kufuta Kadhia ya Palestina na Kuwakata Watu wa Palestina na Watoto Wao kutoka katika Uislamu na Umma wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Katika mkutano kati ya Abbas na Macron jijini Paris mnamo Jumanne, 11 Novemba 2025, ambapo kuundwa kwa kamati ya pamoja ya Ufaransa na Palestina ya kuandika katiba ya dola ya Palestina kulitangazwa (Al Jazeera Mubasher), Abbas anaonekana kupata msukumo kutoka kwa historia ya dola zilizo katika eneo hili zilizopitisha katiba za Magharibi kama msingi wa sheria zao. Wamewachukua Wamagharibi kama mabwana zao, badala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Abbas hakuweza kufanya chochote ila kugeukia Paris na kuwaomba mabwana zake kuandika katiba ya dola iliyo kwenye karatasi—dola ambayo hawezi kuingia au kutoka bila idhini ya Mayahudi. Hawezi hata kulinda mji wake mkuu wa utawala, Ramallah, kutokana na uvamizi wa Mayahudi, na vikosi vyake havisubutu hata kuonekana mbele yao. Walowezi wanawatisha watu wa Ukingo wa Magharibi, wakichoma misikiti yao na kuharibu kila kitu kilicho njiani mwao—mazao, miti, na mifugo. Na dola ya Abbas na vyombo vyake vya usalama vinaangalia kutoka mbali, bila kuchukua hatua hata moja kuwalinda watu, maisha yao, au mali zao.
Kisha Abbas hakuishia hapo. Zaidi ya kusisitiza kwake kuhusu dola ya Palestina isiyo na nguvu za kijeshi na kupokonywa silaha kwa wapiganaji wa upinzani mjini Gaza—isipokuwa silaha zinazotumika kuwaua Wapalestina, kama alivyofanya hapo awali huko Jenin, Tulkarm, Tubas, na kwengineko—aliahidi kusitisha malipo kwa wafungwa na familia za mashahidi, na kumfuata yeyote anayetishia usalama wa umbile la Kiyahudi. Udhalilishaji na unyenyekevu huu si kitu chengine ila ni kufuata maagizo ya Trump na Magharibi, na njia ya kulilinda umbile la Kiyahudi lililonyakua ardhi ya Palestina.
Akiongeza chumvi kwenye jeraha, Abbas alidai kwamba Mamlaka ya Palestina inaendelea na kuendeleza mitaala ya elimu kulingana na viwango vya UNESCO (Al Jazeera Mubasher). Lakini viwango vya UNESCO ni vipi? Je, ni viwango vya Uislamu au viwango vya maadui wa Uislamu?
Viwango vya UNESCO vinawavua watu wa Palestina maadili yao ya Kiislamu na kuyabadilisha na maadili ya uovu, ukafiri, upagani, uzinzi, na uasherati. Viwango hivi vinalenga kuwabadilisha wana wa Palestina kuwa vivuli vya wanaume tu, na kuwalazimisha wanawake na wasichana wetu kuishi kulingana na mila za Kimagharibi, mbali na usafi, staha ya mwili, na adabu. Viwango hivi vinabadilisha hadhi ya Uislamu kwa utumwa, na utamaduni wa kusalim amri, udhalilifu, na uduni kwa utamaduni wa jihad, kuunusuru Uislamu, kuamrisha mema, na kukataza maovu.
Jambo hilo haliishii tu na uhalifu wa kubadilisha mitaala ili kuwafurahisha maadui wa Uislamu. Mamlaka ya Palestina ilifungua shule kwa vyombo vyote vinavyotiliwa shaka ili kukuza fikra ya kijinsia, upotovu, na uhuru wa Kimagharibi, pamoja na sheria zinazovunja familia na kuwachochea watoto kuasi wazazi wao. Nguvu hizi zote zinawatafuna watoto wetu kama mchwa wanaotafuna fimbo ya Suleiman, hadi watoto wetu wafe, miili yao ikiwa haina roho ya Uislamu.
Uhalifu huo uliambatana uvurugaji wa Mamlaka ya Palestina wa mchakato wa elimu nchini Palestina, kukata mishahara ya walimu na kuvuruga uhudhuriaji wa wanafunzi shuleni, hadi kufikia hatua ya uhudhuriaji kuwa wa kawaida kwa nusu ya siku za shule za kila wiki, katika mchakato wa kimpangilio wa ujinga, kutengwa, na hujuma kwa kisingizio cha ukosefu wa pesa na kuzuiwa kwa fedha na Mayahudi.
Abbas na marafiki zake, baada ya kusalimisha ardhi na kula njama dhidi ya Palestina, sasa wanatafuta kuwakabidhi watu na ardhi hii kwa maadui wa watu wa Palestina. Hakika, wanataka kuwakabidhi watoto wetu kwa kafiri ili awafanyie anavyopenda. Hii ni dhulma kubwa na uovu mbaya unaoitisha msimamo wa pamoja wa Wapalestina wote, kama kitu kimoja, kutetea heshima yao au kufa kama mashahidi.
Umma wa Kiislamu, kwa kukaa kimya kuhusu Mayahudi na Mamlaka ya Palestina ambayo kiasili ni ya Kiyahudi, hubeba mzigo wa mateso ya watu wa Palestina na watoto wao, kama vile unavyobeba mzigo wa damu ya watu wa Gaza. Na mzigo wa wale waliomiliki mamlaka na waliweza kuhamasisha majeshi lakini hawakufanya hivyo ni mzigo maradufu, mzigo ambao unaweza kuondolewa tu kwa kuikomboa ardhi hii, kuifuta Mamlaka ya Palestina pamoja na umbile la Kiyahudi, na kuiregesha Palestina kama sehemu huru na muhimu ya ash-Sham, kitovu cha Uislamu, iliyokombolewa kama ilivyokombolewa na Umar (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) na kama ilivyokuwa kwa Salahudin,
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ الله]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Ar-Rum 30:4].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: 0598819100 www.pal-tahrir.info |
E-Mail: info@pal-tahrir.info |



