Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 29 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: HTS 1446 / 63 |
M. Jumanne, 27 Mei 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Al-Kamel Mohammad Khair
[وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ]
“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri” [Al-Baqara 2:155]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, inamuomboleza kwa macho yenye machozi na nyoyo ziliyoridhika na mapenzi ya Mwenyezi Mungu marehemu:
Al-Kamel Mohammad Khair
Ambaye alibeba Da;wah kwa ajili ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, akistahamili maradhi mpaka yakini ilipomjia asubuhi ya leo, Alhamisi, tarehe 29 Dhu al-Qi'dah 1446 H, sawia a na tarehe 27 Mei 2025 huko Al-Kalaklah mtaa wa Khartoum. Marehemu ni kaka ya mbebaji da’wah, Ndugu Adel Mohammad Khair.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwingi wa Rehema, amkubali miongoni mwa mitume, wakweli, mashahidi, na wema, na hao ni marafiki wema walioje.
Tunaipa familia ya marehemu na ndugu zake katika wabebaji dawah, rambirambi za dhati.
Macho yanabubujika machozi, moyo unahuzunika, na tumehuzunishwa sana na kuondoka kwako, ewe Al-Kamel, lakini tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu:
[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara:156].
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |