Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 14 Rajab 1447 | Na: HTS 1447 / 75 |
| M. Jumamosi, 03 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Yafanya Mikutano Kadhaa katika Miji mbalimbali nchini Sudan
(Imetafsiriwa)
Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, mnamo Rajab 1342 H, na kuukumbusha Ummah kuhusu tukio la kusikitisha lililosababisha Ummah kumpoteza Imam wake, ngao, umoja wake kuvunjika, na kafiri mkoloni kuutawala, kudhibiti maamuzi yake ya kisiasa, kiuchumi, na kijeshi, na kuhamasisha Ummah kufanya kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, wanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan walifanya mikutano kadhaa katika miji mbalimbali kote Sudan baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 13 Rajab 1447 H, sawia na 2/1/2026 M, kama ifuatavyo:
* Mkutano ulifanyika mjini Port Sudan, mbele ya Msikiti wa Chuo cha Uhandisi, uliohutubiwa na Ustadh Hussein al-Hadi, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.
* Mkutano ulifanyika Kosti, mbele ya Msikiti Mkuu.
* Mkutano ulifanyika Omdurman, katika Soko la Sabreen, ukihutubiwa na Sheikh Fadlallah Ali Suleiman, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.
* Mkutano ulifanyika Wad Madani, mbele ya Msikiti Mkuu, ukihutubiwa na Ustadh Abdul Aziz Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.
Wakati wa mikutano hiyo, wanachama walibeba mabango yaliyoelezea umuhimu wa kumbukumbu ya miaka hiyo na kile kinachohitajika kwa Ummah, kama vile:
1- Kwa kuvunjwa Khilafah, maisha kamili ya Kiislamu yaliangamizwa, na maisha yakashamiri uasi kwa Mwenyezi Mungu.
2- Kwa kuvunjwa Khilafah, umoja wa Ummah wa Kiislamu uliharibiwa, na damu yake ilimwagika kwa misingi ya utaifa, uzalendo, na madhehebu.
3- Khilafah, ni dola ya ufunguzi, inayoongezeka kila mara na isiyopungua kamwe, na inakomesha mgawanyiko na umwagaji damu.
Pamoja na fikra nyenginezo zinazojadili Khilafah, ufaradhi wake, na umuhimu wake kwa Ummah.
Wahudhuriaji katika mikutano hiyo waliingiliana vyema sana, na kusifu kazi ya Hizb ut Tahrir.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



