Jumatano, 15 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  22 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: H 1446 / 04
M.  Jumanne, 20 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujerumani Yapoteza Fursa ya Kihistoria

(Imetafsiriwa)

Katika maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na umbile la Kiyahudi, Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani inapoteza fursa yake ya kihistoria ya kujikomboa kutoka katika hatia iliyotungwa dhidi ya Mayahudi. Badala yake, shauku ya kile kinachoitwa "maslahi makuu ya kitaifa" - kisingizio kinachotumiwa kuhalalisha uungaji mkono usio na masharti kwa umbile la Kiyahudi - yamefikia kilele kipya kwa tangazo kwamba kuunga mkono umbile hili ni "msingi wa kuwepo kwa Ujerumani"!

Baada ya Friedrich Merz kuchaguliwa kuwa Chansela wa 10 wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, alisema katika hotuba yake ya serikali mnamo 14 Mei 2025, kwamba uhusiano na umbile la Kiyahudi ni “muujiza na zawadi kutoka kwa Dola ya ‘Israel,’ jambo ambalo sisi katika Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani hatukutarajia. Siku mbili kabla, wakati wa kumpokea Rais wa umbile hilo Herzog, Chansela alitoa shukrani zake na kuelezea urafiki kati ya umbile la Kiyahudi na Ujerumani kama "hazina kubwa ambayo lazima ihifadhiwe baada ya miaka themanini tangu mauaji ya Holocaust yaliyofanywa na Wajerumani." Waziri mpya wa Mambo ya Nje, Johann Wadephul, alieleza kuwa urafiki huu unadhihirika katika uungaji mkono wa changamfu wa sera ya ukoloni ya Kizayuni huko Palestina. Alisafiri hadi Tel Aviv mara tu baada ya kuchukua madaraka na akatangaza: "Usalama wa Israel ni jukumu la Ujerumani na msingi wa sera yake ya nje." Wito wake wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza hautokani na wasiwasi kwa maisha ya Wapalestina milioni 2.1 wanaotishiwa na mashambulizi ya anga na njaa, bali tu kutokana na nia ya kuhakikisha kuwepo kwa umbile la Kiyahudi kunaendelea. Alisema hivi: “Sina hakika kwamba malengo yote ya kimkakati ya [Israel] yanaweza kufikiwa kwa njia hii, wala kama hilo linasaidia usalama wa muda mrefu wa Israel. Hivyo tunatoa wito wa kurudi kwa mazungumzo makini ya usitishaji mapigano.”

Serikali mpya ya shirikisho haijaendelea tu katika njia ya "maslahi makuu ya kitaifa," fahamu iliyobuniwa na Chansela wa zamani Angela Merkel na kuungwa mkono na mrithi wake Olaf Scholz - imeiinua hadi kiwango cha kutokuwa na mantiki kabisa. Katika chapisho kwenye jukwaa X la kuadhimisha mwaka wa 60 wa uhusiano wa kidiplomasia na umbilo hilo, Chansela Merz alielezea wasiwasi huu, akisema: "Kuwepo na usalama wa 'Israel' kunatokana na kiini cha kuwepo kwetu wenyewe." Pia alithibitisha kuwa Benjamin Netanyahu anakaribishwa kuzuru Ujerumani licha ya agizo la kukamatwa lililotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. Kwa ajili hiyo, Chansela atatafuta njia na mbinu na atafanya kila awezalo ili kuepuka kutekeleza uamuzi wa ICC. Upotoshaji huu wa kisheria, kulingana na mtaalam wa sheria Kai Ambos, unaifanya ile inayoitwa sheria ya kimataifa kuwa mchezo mtupu.

Matamshi haya yanajiri licha ya ukweli kwamba mauaji ya halaiki huko Gaza yamesababisha mabadiliko ya kimataifa katika mtazamo wa suala la Palestina. Shaka ya wazi juu ya uhalali wa umbile la Kiyahudi inazidi kuongezeka. Uharibifu kamili wa miundombinu ya kiraia, njaa ya mamilioni, na mauaji makubwa ya wazee, wanawake, na watoto yameweka wazi hali ya ukatili ya umbile hili kwa rai jumla ya kimataifa-na pia imeleta mabadiliko makubwa katika hisia za umma wa Ujerumani.

Fahamu ya "maslahi makuu ya kitaifa," kama inavyofafanuliwa na serikali, imetupiliwa mbali hadharani na wataalam mashuhuri wa sheria: Joachim Wieland ameiita fahamu iliyo kinyume na uhuru wa kisheria, Kai Ambos ameielezea kuwa ya kimabavu na kinyume na sheria, Marietta Auer ameiita fahamu ya kisiasa isiyo na athari za kisheria, na Huduma za Kisayansi ya Bundestag and kuiorodhesha kama kanuni tu ya kisiasa. Hata manusura wa mauaji ya Holocaust wamelaani vita vya umbile la Kiyahudi dhidi ya Gaza kama mauaji ya halaiki. Ikiwa kulikuwa na hatia kwa umbile hilo iliyomo ndani ya utambuzi jumla, ilishavunjwa na matukio ya Oktoba 7, 2023, na mauaji yaliyofuata ya Mayahudi huko Gaza. Ujerumani sasa ina nafasi ya kihistoria ya kujikomboa kutoka katika hatia hii ya milele kwa Mayahudi na kupata mafunzo sahihi kutoka kwa historia yake yenyewe. Utekelezaji wa kweli wa kanuni “Usiwahi tena” lazima imaanishe kuchukua msimamo thabiti dhidi ya uhamishaji na uangamizaji wa watu wote.

Ni upumbavu wa kisiasa kwa serikali ya Ujerumani kuendelea na njia hii potofu. Ikiwa itakosa fursa hii ya kihistoria ya kujikomboa kutoka kwa nira ya umbile la Kiyahudi, lazima iwe tayari kwa matokeo. Iwapo itaendelea kuamini kuwa inawajibika kwa usalama wa umbile hilo, itawahisabiwa. Ni suala la muda tu kabla ya Umma wa Kiislamu kuregesha dhamira yake ya kisiasa na uwezo wake wa kujilinda kupitia Khilafah Rashida, ambao kwa hakika utasambaratisha mfumo wa kikoloni katika Mashariki ya Karibu na ya Kati.

Je, Ujerumani iko tayari kubeba jukumu la jinai za Mayahudi siku hiyo?

[هَذَا بَلَاغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنْذَرُوا بِهِ]

“Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye” [Ibrahim:52]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Nchi Zanazozungmza Kijerumani

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu