Jumanne, 18 Safar 1447 | 2025/08/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  9 Safar 1447 Na: 1447 / 01
M.  Jumapili, 03 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sio Taarifa ya Bogotá wala Tangazo la New York litaweza kuliokoa umbile la Kiyahudi!
(Imetafsiriwa)

Wakati sera ya mauaji ya halaiki na njaa huko Gaza ikiendelea huku ukatili wake wote ukionekana na kusikilizwa na dunia nzima, Uturuki vile vile, inaendelea na hatua zake rasmi za kukabiliana na ongezeko la misimamo ya rai jumla nchini Uturuki. Hata hivyo, haikutia saini taarifa iliyotayarishwa na The Hague Group huko Bogotá, mji mkuu wa Colombia, Julai 15–16. Lakini katika kujibu majibu hayo, Wizara ya Mambo ya Nje ilidai kuwa taarifa hiyo huenda ikatiwa saini hadi Septemba 20, na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan alitangaza kuwa wana dukuduku katika muktadha wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari. Hata hivyo, baada ya maandamano ya Gaza kuandaliwa mbele ya makao makuu ya Chama cha Uadilifu na Maendeleo jijini Ankara kwa kushirikisha makumi ya maelfu ya watu mnamo Julai 27, 2025, wakiongozwa na Hizb ut Tahrir, Uturuki ililazimika kutia saini taarifa hiyo pamoja dukuduku hilo.

Ni wazi kwamba kauli hii iliyotolewa na The Hague Group, ambayo ilianzishwa na nchi za dunia ya tatu ili kuokoa hadhi ya mfumo wa kimataifa, haitumiki. Na ingawa haina nguvu ya kisheria, Uturuki kulazimishwa kutia saini taarifa hiyo baada ya wiki mbili inachukuliwa kuwa ushahidi wa kiwango cha utiifu na utumwa wa sera ya kigeni iliyopitishwa. Miongoni mwa dhihirisho jengine la utiifu huu ni kutiwa saini kwa Tangazo la New York lililotangazwa na nchi 16, zikiwemo Umoja wa Ulaya, Umoja wa Nchi za Kiarabu, na Uturuki. Kwa mujibu wa tangazo hili, mujahidina mjini Gaza walitakiwa kuweka chini silaha zao, kuondoka Gaza, na kukabidhi mamlaka kwa vibaraka wa utawala wa Abbas. Kwa kiwango ambacho Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot, alisema: "Kwa mara ya kwanza, nchi za Kiarabu na zile za Mashariki ya Kati zinalaani Hamas, kulaani Oktoba 7, kutoa wito wa kupokonywa silaha kwa Hamas, kutoa wito wa kutengwa kutoka kwa utawala wa Palestina, na kuelezea wazi nia yao ya kuhalalisha mahusiano na Israel katika siku zijazo". Tangazo hili lilidhihirisha wazi kwamba Amerika inatumia serikali hizo juu ya vichwa vyetu kama magavana kwa ukoloni. Kujibu majibu hayo, Uturuki ilitia saini makubaliano hayo pamoja na dukuduku la kifungu kinachohusiana na upokonyaji silaha: "Silaha ziwekwe chini, lakini ima kwa suluhisho la dola mbili au kwa maridhiano kati ya vikundi vya Palestina". Kilele cha khiyana ni hekaya ya suluhisho la dola mbili. Pia inadaiwa kuwa nchi nyingi zitatangaza kuitambua Dola ya Palestina wakati wa mikutano ya Umoja wa Mataifa mwezi Septemba. Hapana shaka kwamba kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina kwenye mipaka ya mwaka 1967 na Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wake ni uwongo uliofichuliwa na udanganyifu unaolenga kucheza na hisia za Waislamu.

Ukweli ni kwamba umbile la Kiyahudi halijaweza kutoka nje ya kinamasi cha Gaza, na bado haijaonja ushindi unaosubiriwa ambao umegharimu mamia ya maelfu ya maisha ya Waislamu wasio na hatia, na hata mlinzi wake Amerika na watawala wanaoshirikiana katika eneo hilo hawajaweza kuliokoa na fedheha hii. Watawala wasaliti ambao hawakuweza kupeleka hata kikombe cha maji kwa ndugu zetu huko Gaza – ambao wameachwa bila makao, bila ulinzi, njaa, maskini, na peke yao – la kusikitisha wanafanya kazi usiku na mchana kulinda mabwana zao kutoka kwa nchi za kikafiri za Magharibi na umbile la Kiyahudi inayofanya matendo yao machafu. Lakini hata wajaribu kiasi gani, hii itakuwa ni huzuni katika nyoyo zao, na kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, watashindwa duniani, na Akhera watapata adhabu kali.

[وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ وَإِنْ يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُسَنَّدَةٌ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ قَاتَلَهُمُ اللّٰهُ أَنّٰى يُؤْفَكُونَ]

Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surat Al-Munafiqun: 4]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-turkiye.org
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu