Jumanne, 19 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  10 Jumada II 1447 Na: HTY- 1447 / 11
M.  Jumatatu, 01 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukamatwa Kupya kwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Yemen na Mahouthi
Je, kauli mbiu “Kifo kwa Amerika” inawezaje kuishi sambamba na Kutetea Mpango wa Trump kuhusu Gaza?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi, 27/11/2025, vikosi vya usalama vya Mahouthi vilimkamata Saddam Ali Qa’id al-Mukirdi, mwenye umri wa miaka 28, kutoka wilaya ya Ṣabr al-Mawadim katika Mkoa wa Taiz ulio chini ya udhibiti wa Mahouthi katikati mwa Yemen. Kukamatwa huku ni kwa pili, kufuatia kukamatwa kwa ndugu Osama na Mohammad Mas’ad Al-Wurafi katika Mkoa wa Ibb mnamo 21/11/2025, baada ya kugawanya toleo lenye kichwa: “Trump Awaongoza Wafuasi Wake Miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mpango wa Fedheha na Aibu, Wanaosujudu Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza ya Hashim Chini ya Udhamini na Ukoloni.” Toleo hilo linafichua dori ya Umoja wa Mataifa katika kutoa Azimio 2803 mnamo 17/11/2025 — kuidhinisha mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kusimamisha vita dhidi ya Gaza, ambavyo Trump alisifu kama “wakati wa kihistoria.” Toleo hilo lilitolewa na Hizb ut Tahrir mnamo 19/11/2025 na kufichua njama ambazo Amerika inazitengeneza nchini Palestina haswa na Mashariki ya Kati kwa jumla, kama sehemu ya sera hiyo hiyo ya vita vya Kimsalaba iliyozinduliwa na George W. Bush mnamo 2001.

Ingawa toleo hilo lilitaja mkutano wa Trump na viongozi wa Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia, na Pakistan, kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo 23/09/2025 – bila kuwataja Mahouthi hata kidogo – lakini yule aliye na manyoya kichwani mwake anawaangalia! Kwa hivyo wale wanaodai wanaunga mkono Gaza na kutafuta kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa kutoka kwa Mayahudi wanawezaje kukubali kwamba Gaza iwekwe chini ya udhamini na ukoloni, na kwamba vikosi vya jeshi vinavyoingia humo vichukue amri kutoka kwa dola za kikoloni – hata kama baadhi yao wanazungumza lugha ya Qur'an?! Na vipi wanawalenga wale wanaofichua kwa Ummah wa Kiislamu kile kilichofichwa katika korido za ukoloni wa Marekani na utaratibu wa kisheria wa kimataifa wa kupinga Uislamu tangu kuanzishwa kwake katika Mkutano wa Westfalia wa 1648 hadi leo?!

Je, Mahouthi wanafikiri kwamba kwa vitendo kama hivyo wamezuia sehemu ambayo ulinganizi wa Hizb ut Tahrir unaibuka – ulinganizi wa kweli unaong'aa na nuru ya ukweli ulio wazi?! Ni tofauti kubwa kiasi gani kati ya malalamiko yao ya dhulma ya Saleh mtawala dhalimu, na leo kizazi chao – na labda kuongezeka – kwa vitendo vile vile dhidi ya mashababu (wanachama) wa Hizb ut Tahrir! Mashababu wa Hizb wametenda uhalifu gani ili kuandamwa na kufungwa?! Je, ni kufichua kwao mpango wa Trump na kutaja kwao uhaini wa watawala katika ardhi za Waislamu?!

Hatujui iwapo Mahouthi wako dhidi ya Amerika – na kwamba “kifo kwa Amerika” ndio kauli mbiu yao kweli – au kama wanaficha mapenzi, utiifu, na ulinzi kwa Amerika, huku wakikabiliana na wale wanaofichua mipango yake katika ardhi za Waislamu! Kwani kwa upande mmoja wao ni “maadui wa Amerika,” lakini wakati huo huo wananyoosha mikono yao kwa amani kwa Umoja wa Mataifa!! Na wanajitosheleza kwa mapigano ya makombora, droni, na mikutano katika Uwanja wa Al-Sabeen – bila mpango wowote au kazi ya kushiriki katika mapigano ya kweli dhidi ya wale walioinyakua Palestina, kuwaangamiza, na kurudisha Msikiti wa Al-Aqsa katika milki ya Waislamu chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, huku takbira zikijaza upeo, zikitimiza bishara njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُوْدَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ»

“Kwa yakini mtapigana na Mayahudi, na kwa yakini mtawaua …” Kisha Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]

“Basi mkifanya wema, mnajifanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra: 7].

Enyi watu wetu nchini Yemen, Enyi watu wa makabila — hasa wale ambao Mahouthi huwategemea katika operesheni zao, hasa katika Sa’dah, ‘Amran, Hajjah, na Dhamar: Je, mnafurahi kwamba wale wanaofichua vitendo vya uhalifu vya makafiri na khiyana ya watawala wa Waislamu wakamatwe? Wale wanaouelimisha Ummah juu ya njia ya kuinuka kwake na heshima yake chini ya Dola ya Khilafah ambayo itawaunganisha Waislamu, kutabikisha Uislamu, na kuubeba duniani — na kwamba tuwe miongoni mwa askari wake, tukishinda katika maisha haya na yajayo? Dola ya Khilafah inarudi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na tutarudi kuwa Umma bora chini yake. Vita vyetu na Mayahudi vinakuja, na tutawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu — hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Wake (saw). Kwa hivyo acheni alama yenu katika kuwanusuru wale wanaolingania kuelekea ushindi wake.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu