Afisi ya Habari
Amerika
| H. 29 Rajab 1447 | Na: 11 / 1447 H |
| M. Jumapili, 18 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutoka Mgawanyiko hadi Umoja
Kongamano la Khilafah 2026
(Imetafsiriwa)
Chicago, IL - Hizb ut Tahrir / Amerika ilifanya kwa mafanikio Kongamano lake la kila mwaka la Khilafah kama sehemu ya kampeni ya kimataifa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kufutwa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab, 1342 H. Kongamano hilo lilitumika kama wito kwa Waislamu kote duniani kutambua na kutimiza wajibu wa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, kama ulivyoamriwa na Mwenyezi Mungu (swt), kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume wetu Muhammad (saw).
Kongamano la mwaka huu, lenye kichwa “Kutoka Mgawanyiko hadi Umoja,” lilihutubia sababu msingi za mgawanyiko ndani ya Ummah na kuchunguza njia ya kikanuni kuelekea umoja uliojengwa katika Uislamu. Kongamano hilo lilihusisha hotuba tatu zikifuatiwa na kipindi wazi cha maswali na majibu.
Ustadh Haitham, katika hotuba ya kwanza, “Nyuma ya Kaulimbiu: Johari ya Umoja wa Kiislamu,” alisisitiza kwamba ingawa Ummah unabaki umeungana sana katika huzuni, huruma, na wasiwasi juu ya migogoro kama vile Gaza, Sudan, na Kashmir, bado umegawanyika kivitendo kutokana na kutokuwepo kwa uongozi ulioungana na muundo mkuu wa kisiasa. Alisisitiza kwamba umoja halisi wa Kiislamu umejengwa juu ya nidhamu, uratibu, na utawala unaotokana na Qur’an na Sunnah. Alieleza zaidi kwamba umoja katika Uislamu si umoja tu, bali ni umoja wa lengo na uwajibikaji, unaoweza kufikiwa tu kupitia uongozi ulioregeshwa na uwajibikaji wa pamoja unaowezesha Ummah kuwalinda watu wake, kudumisha haki, na kutimiza dori yake kama mashahidi juu ya wanadamu.
Ustadh Zaki, katika hotuba ya pili, “Kutoka Kugawanyika Hadi Nguvu: Kujenga Muundo Jumuishi wa Kiislamu,” alielezea kwamba umaskini katika ulimwengu wa Kiislamu unaendelea si kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali, bali kutokana na kugawanyika kisiasa, udhibiti wa uchumi kutoka nje, na mifumo iliyotengenezwa na wanadamu ambayo inazuia usambazaji wa adilifu wa utajiri. Alisisitiza umuhimu wa kimkakati wa ardhi za Waislamu katika nishati ya kimataifa, kilimo, madini, na biashara, akionyesha kwamba mgawanyiko umegeuza wingi kuwa utegemezi. Kwa kutumia kanuni za Kiislamu za haki na umilikaji wa umma, alitoa wito wa umoja wa kiuchumi na kisiasa chini ya utawala wa Kiislamu, akisisitiza kwamba ni mfumo wa Kiislamu pekee unaoweza kuregesha ubwana, kuhakikisha usambazaji sawa wa utajiri, na kulinda Ummah kutokana na unyonyaji.
Dkt. Abu Talha, katika hotuba ya mwisho na ya kuu, “Khilafah: Taswira Mpya ya Uongozi,” alijadili mada kutoka kwa kitabu chake cha hivi karibuni, The Middle East Paradigm. Aliwasilisha uchambuzi kamili wa mizozo inayoendelea katika ulimwengu wa Kiislamu, akielezea kile alichokitaja kama dhana ya “4+2” inayoongozwa na Marekani, ambayo alisema inadumisha kutokuwa na utulivu unaosimamiwa kupitia kipote cha mabepari wa kikanda na miungano teule ili kuhifadhi udhibiti wa nje. Alielezea jinsi nguvu inavyodumishwa bila uhalali, na kuendeleza mgawanyiko na utegemezi. Kwa upande mwingine, Dkt. Abu Talha aliwasilisha mfumo wa “1+0” kama njia badali halali na ya umoja iliyojikita katika uongozi wa Kiislamu, akimalizia kwa wito kwa Waislamu kusonga mbele zaidi ya kukarabati mfumo uliopo na kuelekea kuubadilisha kwa mfumo unaoweza kuregesha ubwana na utulivu wa kudumu.
Kongamano hilo lilimalizika kwa kipindi shirikishi cha maswali na majibu, ambapo wazungumzaji walizungumza moja kwa moja na hadhira.
Ummah unaendelea kuonyesha ustahimilivu wa ajabu na unatamani mustakabali mzuri zaidi. Iman yetu na maadili ya pamoja yanatukumbusha kwamba umoja sio tu kwamba unawezekana bali pia ni Faradhi muhimu. Uislamu hutoa muongozo unaokuza haki, utu, na mshikamano, ukitoa matumaini ya mustakabali uliojengwa juu ya ushirikiano, lengo, na uwajibikaji wa pamoja. Waliohudhuria kongamano hilo walionyesha kwamba walihisi wametiwa moyo kweli na maudhui yaliyowasilishwa. Mwenyezi Mungu (swt) abariki juhudi zetu, aunganishe nyoyo zetu, na azipe mafanikio juhudi zote za dhati.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |



