Jumamosi, 07 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chazindua Kampeni ya Kimataifa “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”

Mgogoro wa kikatili nchini Sudan kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) wanaoongozwa na mtawala mkuu wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), ambaye hapo awali alikuwa naibu wa al-Burhan katika Baraza Kuu, sasa umeingia mwaka wake wa tatu, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia. Baadhi ya makadirio yanaweka idadi ya waliofariki katika vita hivi vya kipumbavu kufikia 150,000, huku kukiwa na ukatili wa kutisha uliofanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kinyama, mateso, ubakaji mkubwa na uhalifu mwingine wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana. Mauaji ya kikabila pia yameripotiwa, huku jamii nzima zikiteketezwa kwa moto na kuangamizwa, na mauaji ya halaiki katika miji mbalimbali, vijiji na kambi za watu waliokimbia makaazi yao.

Soma zaidi...

Al-Waqiyah TV: Kwa Nini Kuwahisabu Watawala ni Faradhi ya Kisheria

Unapomteua mtu wa kutekeleza jukumu ambalo asili yake ulikabidhiwa, hii ina maana kwamba ni wajibu wako wa Shariah kumfuatilia na kumhisabu ikiwa ameghafilika, anafanya makosa, au anadhulumu, na kadhalika. Ni jambo la kawaida kwa Ummah kuendelea kuwa macho juu ya mtawala. Haya ni faradhi yake ya Shariah na Shariah yake kwa wakati mmoja. Maana ya faradhi yake ya Shariah ni kuwa Ummah utakuwa ni wenye dhambi ukilipuuza hili. Haki yake Shariah ni kwamba mtawala atatenda dhambi ikiwa atauzuia kutekeleza wajibu wa kuhisabu, ufuatiliaji, na ushauri, na kadhalika.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan: “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.”

Hii ni hotuba kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Waislamu kuhusiana na faradhi ya Shariah ya kuwanusuru Waislamu walio chini ya mamlaka ya dola za kikafiri na makafiri ambao hawajahamia kwenye Nyumba ya Uislamu (Dar ul Islam), iwe kwa kuwazuia utekelezaji wa ibada zao za kidini au kwa kuwadhulumu.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Matembezi ya Halaiki ya Kuinusuru Gaza “Kuwahutubia wale Wanaohusika!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 21, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake 200,000 Waislamu hadi sasa. Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa matembezi makubwa ya halaiki kote nchini Uturuki licha ya serikali ya Uturuki kuyapiga marufuku.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Matukio Mjini Al-Suwayda

Axios iliripoti kwamba mkutano wa ngazi ya juu ulifanyika jijini Paris kati ya Waziri wa Mambo ya Kimikakati wa ‘Israel’ Ron Dermer na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad Al-Shibani, uliopatanishwa na mjumbe maalum wa Marekani nchini Syria, Thomas Barak, mnamo 25/7/2025. Siku chache zilizopita tangu tarehe 12/7/2025 zimeshuhudia kuongezeka kwa machafuko katika Jimbo la Al-Suwayda [Sweida] kusini mwa Syria, ambalo wengi wa wakaazi wake ni Druze. Umbile la Kiyahudi limetangaza kuingilia kati masuala yao sambamba na kuendeleza uvamizi na mashambulizi yake nchini Syria. Lilishambulia pambizoni mwa kasri la rais, na kuishambulia Wizara ya Ulinzi na Majeshi jijini Damascus.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Serikali za Kijamhuri na za Kifalme Zimeisaliti Gaza... Kwa Khilafah tutainusuru Gaza”

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia ilifanya matembezi makubwa katika mji mkuu wa Tunis, mbele ya Msikiti wa Al-Fath baada ya swala ya Ijumaa, mnamo  tarehe 25 Julai 2025 M chini ya kichwa: “Serikali za Kijamhuri na za Kifalme Zimeisaliti Gaza... Kwa Khilafah tutainusuru Gaza”

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Uvamizi wa Umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran na Athari zake

Al Arabiya ilichapisha kwenye tovuti yake mnamo tarehe 27/6/2025: "Vyanzo vinne vyenye taaarifa vilisema kuwa utawala wa Rais Donald Trump ulijadili uwezekano wa kuisaidia Iran kufikia hadi dolari bilioni 30 ili kujenga mpango wa nyuklia kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya kiraia. Vyanzo hivyo viliongeza kuwa majadiliano haya yaliendelea wiki hii baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano. Maafisa wa utawala wa Trump walithibitisha kwamba mapendekezo kadhaa yamewsilishwa, ya awali pamoja na yaliyoboreshwa, yakiwa na kifungu kimoja kisichobadilika, kisichoweza kujadiliwa : “kukomeshwa kabisa kwa urutubishaji wa urania ya Iran.”

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu