Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: India Yaungana na Watawala wa Pakistan Kuipiga Marufuku Hizb ut Tahrir!
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
India yaungana na watawala wa Pakistan kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir!
India yaungana na watawala wa Pakistan kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir!
Mnamo Ijumaa, Oktoba 11, 2024, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia ilifanya Kongamano la kila Mwaka la Khilafah chini ya kichwa: “Khilafah ya Kiislamu… Kuelekea Mfumo Mpya wa Kimataifa”
Hizb ut Tahrir / Indonesia iliandaa amali kubwa katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta, na katika mji mkubwa wa pili nchini Indonesia wa Surabaya, ambapo maelfu ya Waislamu walikusanyika na kutaka kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu ili kuwanusuru Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kuukomboa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na Palestina yote inayokaliwa kwa mabavu.
Baada ya swala ya Ijumaa, matembezi ya hamsini na tatu yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, mbele ya Msikiti wa Al-Fatah, matembezi makubwa yaliyoitishwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia, kwa watu wa Al-Khadra, na yenye kichwa “Kwa Khilafah, Majeshi yatasonga kuikomboa Palestina.”
Kutokana na imani kwa Qadhaa ya Mwenyezi Mungu, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inamuomboleza: Hajj Youssef Mustafa Al-Toubasi (Abu Osama).
Mwaka mmoja umepita tangu Kimbunga cha Gaza, ambacho kimetikisa misingi ya hadhara ya Magharibi na kuponda ponda simulizi ya jeshi lisiloweza kushindwa. Mwaka mmoja wa uchinjaji na mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza yametekelezwa na nchi za Magharibi zenye chuki na zingali zinaendelea kutekeleza kwa kulitumia umbile nyakuzi. Mwaka mzima wa kula njama na kufanya biashara ya umwagaji damu ambayo watawala wa Waislamu wamegeuka kuwa waovu, na kuwaongezea fedheha.
Enyi Waislamu, kwa kuzingatia kimya cha watawala wote na vikosi vyao vya majeshi, tunasisitiza kwamba suluhisho pekee la ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni kusimamishwa Khilafah. Hizb ut Tahrir inakulinganieni kwa dhati na bila kuchoka kushiriki katika kazi hii tukufu na ya dharura. Muna khiari ya ima kunyamaza, kuendelea kuwaunga mkono watawala wenu, au kuungana mikono na Hizb ut Tahrir katika kazi zetu za kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Oktoba 7... Mwaka Kamili na Watu wa Gaza wangali Wanasubiri Nusra ya Majeshi, Basi lini Mtawanusuru?!
Matokeo Makuu ya Vita dhidi ya Gaza!
Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Uturuki iliandaa baada ya swala ya Ijumaa matembezi na visimamo vikubwa katika miji 16 kote nchini Uturuki, kama ambavyo Hizb pia iliandaa makongamano, vikao na mikutano mikubwa chini ya kichwa: “Mwaka Mzima umepita, na Nchi 57 Hazijachukua Hatua Yoyote!”