Maneno Hayatoshi Kuuadhibu Utawala wa Modi wenye Chuki na Uislamu
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hivi majuzi, serikali ya Narendra Modi ilijikuta matatani baada ya baadhi ya wanachama wake kutoa matamshi ya dharau dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Katika nia ya kujinasua kutoka kwa ghadhabu inayozidi kuongezeka katika ulimwengu wa Kiislamu, Modi alichukua hatua haraka kuwasimamisha kazi maafisa wa BJP wenye hatia lakini hii haikusaidia kuzuia kashfa dhidi ya serikali yake.