Jumanne, 14 Shawwal 1445 | 2024/04/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 10/05/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashidah... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 20 Shawwal 1444 H sawia na 10 Mei 2023 M

Fahari na Heshima Zipo katika Jihad ya Kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu

Mkuu wa Majeshi ameonya juu ya majaribio ya "kuleta msukumo" kati ya watu na jeshi mnamo Aprili 29, kwenye gwaride la kufuzu. Njia pekee ya kuimarisha uhusiano kati ya Ummah na jeshi lake ni kuzika Mafundisho ya Bajwa yanayoungwa mkono na Marekani kwa kusimamisha tena Khilafah. Ni Khilafah ndiyo itakayoisafisha Pakistan kutokana na ushawishi mbaya wa Marekani. Itamaliza vita vya Fitna kwenye mpaka wa Magharibi, huku ikiikomboa Kashmir kupitia Jihad.

14 Shawwal 1444 H sawia na 04 Mei 2023 M

Ni Khilafah Peke Yake ndiyo Inayoweza Kuhakikisha Ustawi wa Fedha

Mnamo tarehe 28 Aprili 2023, Bodi ya Hazina ya Marekani iliibua wasiwasi kuhusu mgogoro wa Benki ya Silicon Valley, kuhusu "udhaifu na kuilazimisha benki kuurekebisha." Hata hivyo, udhaifu halisi hauko katika benki moja pekee, bali katika mfumo wa fedha wa kibepari kwa jumla. Unakopesha kile usichomiliki katika mali halisi kwa sababu ya riba, mfumo wa benki za akiba wenye vitengo na sarafu ya karatasi isiyo na thamani ya dhati (fiat). Kwa kukomesha riba na kutoa sarafu ya dhahabu na fedha, Khilafah itatoa ustawi wa fedha thabiti kwa uchumi.

15 Shawwal 1444 H sawia na 05 Mei 2023 M

Dori ya Majeshi Inaamuliwa na Qur’an Tukufu na Sunnah za Mtume, Sio Katiba ya 1973.

Ikihutubia gwaride ya kufuzu ya PMA, COAS alisisitiza kwamba utiifu wa jeshi uko katika katiba ya Pakistan. Hata hivyo, kwa mujibu wa Uislamu, utiifu wa jeshi la Kiislamu ni kwa Mwenyezi Mungu ﷻ na Mtume Wake ﷺ pekee. Sio kwa dola ya kitaifa au katiba ya kisekula. Kwa mujibu wa Quran na Sunnah, majeshi ya Khilafah yatakomboa maeneo yote ya Waislamu yaliyokaliwa kwa mabavu na kuhakikisha utawala wa Dini kupitia Da’wah na Jihad.

16 Shawwal 1444 AH sawia na 06 Mei 2023 M

Fungeni Kituo cha Ujasusi na Makaazi ya Ufisadi, Kilichojifinika Guo la Ubalozi

Katika hati yake ya ufadhili, "Maendeleo ya Kitaalamu ya Lugha ya Kiingereza ya Pakistan kwa Walimu, Wanafunzi, na Wataalamu Wachanga," Ubalozi wa Marekani unapigia debe uungaji mkono wa mashoga na wasagaji nchini Pakistan, kwa ruzuku ya $500,000. Baada ya kuharibu kitengo cha familia huko Magharibi, masekula wanataka kufanya vivyo hivyo katika Ulimwengu wa Kiislamu. Ubalozi wa Marekani sio tu ni kituo cha kijasusi chenye vifaa vya kutosha, ni chanzo cha uharibifu kwa vijana wetu. Ni Khilafah ndiyo itakayofunga balozi zote za dola zinazotangaza vita dhidi ya Uislamu.

17 Shawwal 1444 H sawia na 07 Mei 2023 M

"Kupambana na Ugaidi" Kunaelekeza Jeshi Letu katika Ulinzi wa Maadui wa Uislamu

Ziara ya waziri wa mambo ya nje nchini India, kwa ajili ya mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, ni hatua hatari. Lengo la taasisi hii ya kikoloni ni kuzuia upinzani wowote wa silaha wa Waislamu dhidi ya uvamizi wa India, Urusi na China. Inalenga jeshi letu katika kulinda ukaliaji kimabavu wa Kashmir na Dola ya kigaidi ya Kibaniani. Khilafah ndiyo itakayozikomboa Ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu, na kukomesha ugaidi halisi.

18 Shawwal 1444 H sawia na 08 Mei 2023 M

Ondoeni Aina Zote za Uwepo wa Marekani ili Kumaliza Ugaidi

Katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 1 Mei 2023, uongozi wa jeshi ulijitolea "kumaliza tishio la ugaidi." Hata hivyo, haumalizi chanzo cha ugaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu, uwepo wa Marekani. Ili kuchochea ugaidi na ukosefu wa utulivu, Marekani hutumia ubalozi wake na afisi zake ndogo za ubalozi, ukanda wa anga wa "Boulevard" na mtandao wa "Raymond Davis". Khilafah itatokomeza papo hapo mitandao ya kigaidi ya dola zote hasimu, ikiwemo Marekani na mshirika wake, Dola la Kibaniani. Kisha itaelekeza ujasusi na jeshi la Kiislamu katika kuzilazimisha dola za kiadui kurudi salimu amri.

19 Shawwal 1444 H sawia na 09 Mei 2023 M

Tunahitaji Khalifah, Anayetawala kwa Uislamu, na sio Bunge la Kidemokrasia, Linalotawala kwa Ukafiri

Uchaguzi ndani ya siku 90 katika Demokrasia sio faradhi ya Kisharia. Hata hivyo, ni faradhi ya Kisharia kumteua Khalifa ndani ya siku tatu, na mikesha yake, baada ya kumpoteza Khalifah. Ummah ulipoteza Khilafah yake zaidi ya karne moja ya Hijri iliyopita. Ummah lazima ujitahidi kuregesha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni lazima upuuze kufanyika kwa chaguzi chini ya Demokrasia, ambayo ni mfumo muovu na wa Kikafiri.

20 Shawwal 1444 H sawia na 10 Mei 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu