- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Amali ya Jioni ya Ramadhan: “Mikataba ya Kimataifa... Mkataba wa Hudaybiyyah kama Mfano”
Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia iliandaa amali ya jioni ya Ramadhan iliyopewa kichwa “Mikataba ya Kimataifa: Mkataba wa Hudaybiyyah kama Mfano” siku ya Jumapili, 8 Machi 2026, saa 4:00 PM kwa saa za Tunisia, katika Kituo cha Makongamano jijini Tunis.
Amali hiyo ya Jioni ilianza kwa kusoma aya kutoka Quran Tukufu, ikifuatiwa na hotuba kutoka kwa Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri. Alianza kwa kuelezea kwamba siasa na utawala wa masuala ya umma katika nchi za Kiislamu hautawaliwi na sheria ya Kiislamu, na kwamba Umma wa Kiislamu uko chini ya utawala na udhibiti wa mfumo mwengine usokuwa mfumo wa Kiislamu unaotokamana na itikadi yake. Alisema kwamba kila nchi ndani ya ulimwengu wa Kiislamu inasimamia mahusiano yake kulingana na maslahi ya nguvu ya nje. Kisha akazungumzia kuhusu mabadiliko ambayo yametokea katika siasa za mfumo wa kimataifa, ambapo Baraza la Usalama wala Umoja wa Mataifa wala mashirika ya haki za binadamu hayana uzito au ushawishi wowote. Badala yake, Amerika leo inatafuta kuweka nguvu zengine za kimataifa, kama vile China, Urusi, na Muungano wa Ulaya, ndani ya mfumo wa sera zake za kupanua udhibiti wake juu ya ulimwengu. Na kwamba watawala wa nchi za Waislamu hawana usemi, msimamo, na hakuna usemi katika mlinganyo huu. Alitoa mfano mkuu wa kadhia ya Palestina, ambayo Trump ameweka kwenye dawati lake, akitoa hukmu na maamuzi, huku kila mtu akitii maagizo yake. Alielezea zaidi kwamba makubaliano yote ya dhahiri na ya siri yaliyohitimishwa na watawala wa Waislamu ndani ya mipaka ya Mkataba wa Sykes-Picot (dola ya kitaifa) pamoja na dola kubwa ni vibaraka tu. Ni kwa madhumuni ya kuutiisha umma na kulazimisha udhibiti wa mkoloni kafiri juu yake. Hatari zaidi ni mabadiliko ya ardhi za Waislamu kuwa hifadhi ya kimkakati kwa Amerika, ambapo vipengee vyote vya nguvu—utajiri, kambi na misingi ya kijeshi, bandari, viwanja vya ndege, na vyenginevyo—vimeunganishwa kutumikia sera ya kigeni ya Marekani.
Alihitimisha kwa kuelezea kwamba makubaliano kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu lazima yawe chini ya hukmu za kisheria zinazotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake. Alitaja Mkataba wa Hudaybiyyah, ambayo ndio mada ya amali hiyo ya jioni, kama mfano. Mkataba huu wa kimataifa, uliohitimishwa katika mwaka wa sita wa Hijra kati ya dola ya Kiislamu, iliyoongozwa na Mtume Muhammad (saw), na Maquraysh, haukuvunja masharti ya hukmu ya sheria ya Kiislamu, na matokeo yake makubwa yalikuwa kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu kama vile utambuzi wa Maquraysh wa dola changa ya Kiislamu, mapambano yake yaliyofuata na dola kuu, na ushindi ambao Mwenyezi Mungu aliwapa Waislamu, kama vile ufunguzi wa Makka, kushindwa kwa viumbe vya Kiyahudi katika Bara Arabu, na ushindi mwingineo.
Kwa hivyo, kwa kuweka mikataba iliyohitimishwa leo kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika mizani ya sheria ya Kiislamu, tunaiona kuwa ya batili na lazima ibatilishwe na kufutwa. Hili linaweza kupatikana tu kwa kiongozi mmoja ambaye anaweza kuwaleta Waislamu pamoja. Yeye ndiye ambaye ameahidiwa utiifu, na atarudisha umma wa Kiislamu katika nafasi yake ya uongozi kama “Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu.”
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Jumapili, 19 Ramadhan 1447 H, sawia 8 Machi 2026 M

https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/5308.html#sigProId75a430021a

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir




